Thursday, November 22, 2012

Waasi watishi kuendeleza Mapigano


 Msemaji wa waasi wa M23

 Msemaji wa kundi hilo la waasi wa M23 rLt Col Vianney Kazarama amewaambia watu waliokuwa wamekusanyika mjini Goma kuwa wako tayari kukomba taifa hilo.
Awali Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linalolaani kutekwa kwa mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23.
Azimio hilo pia linamtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuripoti kuhusu madai   ya uungwaji mkono wa mataifa ya kigeni kwa makundi ya uasi yaliyoanza harakati zao nchini Congo miezi minane iliyopita.
Baraza la usalam la Umoja wa mataifa limelaani vikali kitendo cha waasi wa M23 wa cha kuuteka mji wa Goma.
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa tayari limeidhinisha vikwazo dhidi ya mkuu wa kundi hilo na limesema limenuia vikwazo hivyo vitawalenga viongozi zaidi wa waasi .
Wajumbe wa baraza hilo wameelezea hofu kubwa juu ya shutuma kuwa waasi hao wanaungwa mkono kutoka nje hatua iliyopelekea waasi wa M23 kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kijeshi

Katibu mkuu wa UN kuchunguza madai

Baraza hilo limemtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuchunguza ripoti kuhusiana na shutuma hizo.
Raia wakimbia makwao mjini Goma
Raia wakimbia makwao mjini Goma
Wataalamu wa Umoja wa mataifa wamesema kuna ushahidi wa kutosha kuwa Rwanda inawaunga mkono waaasi hao na makundi ya haki za kibinadamu kwa kushindwa kutuma onyo kwa utawala wa Kigali kama wahusika.
Wakati huo huo maafisa wa Uganda wanasema rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na rais Paul Kagame wa Rwanda wamekutana nchini Uganda kujadili Mzozo huo unaoendelea Mashariki mwa Congo .
Mkutano huo wa siku mbili umekuja baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi hao wanaoaminiwa kuungwa mkono na Rwanda , wanasema wako tayari kusonga mbele hadi mji mkuu Kinshasa kwa kile walichokitaja kuwa ni kukomboa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa sasa.
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limelaani kukamatwa kwa mji wa Goma

No comments: