RAIS KIKWETE AKIWA WILAYANI KARAGWE
Wananchi
wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani
Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (1)
Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa.
Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu Jumamosi Julai 27, 2013.
SIMANZI FAMILIA ZA ASKARI JWTZ
Vilio na simanzi vimetawala katika baadhi ya
familia za askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao
waliuwawa katika eneo la Darfur, Sudan ambako wanashiriki katika ulinzi
wa amani.
Mamia ya waombolezaji
walionekana katika makazi ya familia za marehemu; Songea mkoani Ruvuma
na Nachigwea mkoani Lindi ambako ziko kambi ambazo baadhi ya askari hao
walikuwa wakifanya kazi.
Imefahamika kuwa wanajeshi
waliouwawa Jumamosi iliyopita wanatoka katika vikosi vya, 42KJ Chabruma,
Songea, 44KJ Mbeya, 36KJ Msangani, 92KJ Ngerengere, 94KJ cha
Mwenge,
Dar es Salaam, 41KJ Nachingwea na Makao Makuu ya JWTZ- Upanga, Dar es
Salaam.
Jana gazeti hili lilibaini
kuwapo kwa maombolezo katika baadhi ya familia za wanajeshi hao baada ya
kupokea taarifa za vifo vyao kutoka JWTZ. Hata hivyo bado majina ya
waliofariki hayajawekwa hadharani.
Msemaji Mkuu wa JWTZ, Kanali
Kapambala Mgawe juzi aligoma kutaja majina hayo akisema kuwa majina hayo
hayajatolewa rasmi na kwamba familia za marehemu zilikuwa
hazijajulishwa.
“Hayo majina yanayotajwa kwenye
mitandao ni ya uongo. Kwa sasa mimi sijaletewa majina na utaratibu
uliopo ni hadi ‘next of kin’ (ndugu) wao wajulishwe kwanza,” alisema
Kanali Mgawe.
Hata hivyo kupitia katika maeneo
ilikokuwa misiba hiyo jana, gazeti hili lilifanikiwa kufahamu majina ya
baadhi yao, ambayo yanafanana na yale yaliyotangazwa kwenye mitandao ya
kijamii pamoja na baadhi ya magazeti.
Katika Kambi ya Chabruma, Songea
mkoani Ruvuma kulikuwa na umati wa waombolezaji nyumbani kwa mmoja wa
wapiganaji hao, Koplo Oswald Chaula ambaye alikuwa katika Kikosi cha
Mizinga Chabruma na ndugu zake walikiri kupokea taarifa za msiba huo.
Hali kama hiyo ilikuwa nyumbani
kwa Koplo Mohamed Chukilizo katika Kambi ya Majimaji, Nachingwea ambako
baadhi ya ndugu na jamaa za zake wakiwamo mkewe na baba mkwe wake
walikutana jana jioni kujadiliana kuhusu msiba.
Mwananchi pia lilishuhudia
waombolezaji wakiwa wamekusanyika eneo la Mjimwema, Songea Mkoani Ruvuma
ambako ni nyumbani kwa Komandoo Rodney Ndunguru aliyetoka kikosi cha
92KJ Ngerengere, Morogoro, baada ya kupokea taarifa za msiba huo.
Vilio, Simanzi
Katika kambi ya Chabruma, mke wa
marehemu Koplo Oswald aliyejitambulisha kwa jina la Maria alikuwa
akilia kwa simanzi baada ya kupata taarifa kuwa miongoni mwa waliofariki
ni baba watoto wake
“Ninamuomba Mungu ampumzishe mume
wangu...nimekosa nini jamani, mume wangu kaondoka...alikuwa tegemeo
langu. Sijui kama wanangu watasoma, dunia imenigeuka... imekuwa ghafla
mno, Chau kaondoka bado nampenda,” alisikika akisema Maria huku akiwa
amewakumbatia wanawawe. Ndugu na jamaa walikuwa wakimfariji.
Maria anatarajiwa kuondoka
Songea leo kwenda katika kijiji cha Kilolo, mkoani Iringa kusubiri mwili
wa mume wake ambaye atazikwa huko. Chaula ameacha watoto wanne, mmoja
akiwa na umri wa miezi minne.
Katika eneo la Mjimwema mama wa
marehemu Ndunguru, Lucy Ndunguru aliyekuwa akilia muda wote, alisema:
“Mwanangu Rodney kaniacha...nilikuwa namtegemea, alikuwa ananitunza na
mimi ni mjane sasa kaniacha...ee Mungu nimekosa nini mimi....”
Sauti yake ya mitetemo na kwikwi
za simanzi viliwafanya baadhi ya waombolezaji nao kujikuta
wakibubujikwa na machozi, huku kukiwa na taarifa kwamba wanapanga
marehemu kama atazikwa Kijiji cha Myangayanga alikozikwa baba yake.
Mwananchi iliyokuwa nyumbani kwa
marehemu na kushuhudia vilio na simanzi na wengi wamekuwa wakizidisha
vilio hasa kutokana na mke wake kuwa na kichanga kwani alikwenda
kujifungua nyumbani kwao Zanzibar.
Kwenye Kambi ya Majimaji,
Nachingwea ilifahamika kuwa Koplo Chukilizo ambaye alikwenda Darfur kama
fundi wa magari ya deraya, ni mwenyeji wa Kigoma na kwamba huenda
akasafirishwa kwenda huko.
Baba mkwe ambaye marehemu alizaa na mwanawe alisema: “Taarifa nimezipata jioni hii, tulikuwa na wasiwasi lakini tukathibitisha
RAIA WAMIMINIKA NA VIKOMBE KUNYWA MAZIWA
Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony.
Ama kweli ustaa kazi! Mrembo Wema Sepetu kakumbwa na kasheshe kutoka kwa
mashabiki wake baada ya kutupia picha instagram akiwa kapozi na wengine
kuanza kumlamu kutokana na mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Japo
alijitetea na kusema picha hizi alipiga kabla ya mwezi huu wengine hata
hawakumuelewa!
NEW SONG / Ostaz Juma na Musoma ft Young Killa & Mo Music - Muziki Kazi
RAIA WAMIMINIKA NA VIKOMBE KUNYWA MAZIWA
Wakazi
wa jiji la Dar es salaam wakikinga maziwa kwenye kontena la kampuni ya
maziwa ya Tanga Fresh baada ya kichwa cha kontena hilo kuchomoka na
kuacha njia eneo la ubungo mataa leo Julai 24, 2013.likitokea Mkoani Tanga hakuna aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Kila siku tunanunua: Ustadhi naye akijipatia maziwa bila kujali yana usalama au hapana
Jeshi la polisi likiwa kwenye eneo la tukio.
Kichwa
chenye namba za usajili T 787 AFX lilobeba kontena la maziwa likiwa
pembeni ya barabara mara baada ya kuacha njia likitokea Mkoani Tanga.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
PICHA 5 / ZA WANAJESHI WA TANZANIA WALIO UAWA DARFUL
Prayers from a chaplain.
Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers.
Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers.
Military salute as the 'Last Post' rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes.
PICHA / WEMA APATA KASHESHE BAADA YA KUTUPIA POZI TATA INSTAGRAM
Kweli umaarufu kazi na unahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment