Maskofu
wakipita kuaaga mwili wa marehemu Askofu Pascal Kikoti wa jimbo la
mpanda aliyefariki hivi karibuni katika hospitalia ya Bungando jijini
Mwanza alikokuwa akitibiwa.
(Picha zote na Kibada Kibada Fullshangwe- Katavi)
(Picha zote na Kibada Kibada Fullshangwe- Katavi)
Waziri
mkuu Pinda akiwa miongoni mwa waumini wa kanisa katoliki jimbo la
Mpanda katika ibada ya mazishi ya Askofu Pascal Kikoti misa katika
iliyofanyika leo jumamosi septemba mosi 2012.Askofu mkuu jimbo kuu la Dar es salaam Kadnari Pollycarp Pengo akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Askofu Kikoti.Waziri
mkuu Mh. Mizengo Pinda akiweka shada la maua kwenye kaburi la askofu
Kikoti katika mazishi yaliyofnaya kanisa la Mt. Maria Emakulata jimbo
la Mpanda.
Na Kibada Kibada Fullshangwe-Mpanda
Waziri mkuu Mizengo Pinda leo
ameongoza mamia ya waombolezaji wa jimbo katoliki la mpanda kuuaga mwili
wa marehemu Askofu wa jimbo la Mpanda Askofu Pascal Kikoti
aliyefairiki dunia kwa shinikizo la damu.
Akitoa salaamu za serikali waziri
mkuu Pinda amesema kanisa limepoteza nguzo kubwa na tegemeo la kanisa
na jamii kwa kuwaalikuwa mtu wa pekee kutokana na juhudi zake alizokuwa
akizionesha za kuleta maendeleo katika jimbo la mpanda na jamii ya
watanzania kwa ujumla hususani waumini wa kanisa la katoliki jimbo la
mpanda na Tanzania kwa ujumla.
Waziri mkuu Pinda alisema Mhashamu
Askofu kikoti alifanya kipindi cha maisha yake ya uinjilisti hapo
jimboni na kutoa mchango wake mkubwa ambao uligusa jamii nzima na siyo
tu katika kutoa huduma za kiroho, balipia huduma za kijamii zilizolenga
kuleta maendeleo kwa wananchi katika jimbo la mpanda na nchini kwa
ujumla
nyota ya Askofu wa jimbo katoliki
la mpanda Mhashamu Pascal Kikoti imezimika leo alipohitimisha safari
yake hapa duniani pale kwenye kanisa katoliki na kuacha vilio simanzi na
majonzi mazito kwa wakazi wa mpanda na waumini wote wa wilaya ya mpanda
mkoa wa katavi kwa ujumla.
Mhashamu baba Askofu Kikoti
ametutoka hiyo ni kauli yake waziri mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa wakati
akitoa salaamu kwa niaba ya serikali mara baada ya kumalizika kwa ibada
ya maziko iliyoongozwa na kadinari Polcapy Pengo askofu mkuu wa jimbo
kuu la Dar es salaam.
.
“Mimi binafsi nimefanya kazi kwa
karibu sana na Mhashamu Askofu Kikoti, tangu alipowekwa wakfu na
kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo la mpanda mwaka 2001, na hata
kabla.nilifairijika sana na uongozi wake, maono yake na shauku yake ya
kutoa huduma za kiroho na za kijamii kwa jumla ,hivyo basi ni dhahiri
kwamba kifo hiki ni pigo kubwa siyo kwangu, au kwa waumini wa kanisa
katoliki, au wanampanda tu, bali wananchi wote nchini kwa jumla” alisema
waziri mkuu Pinda.
“Mhashamu Askofi Kikoti ametutoka
akiwa na umri mdogo sana wa kiuchungaji wa miaka 55,utumishi wake
ulitukuka bado ulikuwa unahitajika sana, kwa maneno mengine
,badoangeendelea kutoautumishi kwa miaka mingine mingi zaidi,kabla ya
kifo chake alikuwa na malengo mengi mazuri yakiwemo yakufungua seminari
ndogo ya jimbo,kujenga kituochakiuchungaji na jamii na kupanua shule ya
sekondari ya mtakatifu Maria ya hapa Mpanda,lakini mungu ameamua
amuchukemapema “alisema waziri mkuu Pinda.
Alisema anatambua machungu
waliyowapata wanampanda kwa kupoteza kiongozi nguzo ya jimbo la mpanda
,kikubwa ni kumunzi kwa kuendeleza yale mazuri aliyoaanza marehemu
Kikoti na kwa njia hiyo watakuwa wameendeleza ile kauli mbiu yake
inayosema kwamba “katika imani na upendo “alisema panda hiyo ilikuwa
kauli mbiu ya mhashamu Askofu Kikoti.
Hata hivyo waziri mkuu Pinda
alisema mungu atawaongoza katika kumpata mrithi wake ambaye ataendeleza
kauli mbiu hiyo pamoja na kukamilisha malengo aliyokuwa nayo.muhimu nni
kumwombea kwa mwenyezi mungu aipumzishe Rohpo ya Marehemu mahali pema
peponi.
Awali Akisoma salama za rambirambi
zilizotumwa na mhe,Rais Jakaya Kikwete kwa Rais wa baraza la maaskofu
Tanzania Askofu Tarcirius Ngalalekumtwa salaamu zilizosomwa na katibu wa
maaskofu Padri Anton Makunde mhe, Rais katika salamu zake alisema
kanisa limpoteza mtu muhimu ambaye utumishi wake kwa kanisa taifa na
jamii kwa umla bado vilikuwa vinahitajika sana.
Alisema yale yote mema
aliyoyafanya Askofu Kikoti ni vyema yaendelezwe na kuenzi ili kumuenzi
Mhashamu Askofu Kikoti na wao kamaviongozi wa Taifa wataendelea
kuyaenzi.
Akisoma wasifu wa marehemu Askofu
Mkuu wa Jimbo kuu la Tabora Paulo Ruzoka alisema marehe Kikoti alizali
wilayani Kilolo katiaka kijiji cha —-na kusoma elimu ya msingi mkoani
iringa kasha kujiunga na seminari ya mafinga,
Tungamo,Peramiho,kiparapala, Nyegezi kasha kwenda roma italia kwa ajili
ya kusomea historia ya mababa wa kanisa na aliporejea alikuwa
akifundisha seminari ya peramiho hadi alipoteuliwa kuwa Askofu wa kwa
jimbo la mpanda hadi kifo cha alikuwa askofu wajimbo lampanda ambapo
ametumikia miaka kumia na moja.
Misa ya maziko imeongozwa na
kadri Pengo ambapo katika misha hiyo Askofu wa Jimbo la Sumbawanga
Damian Kyarusi aliteuliwa na Baba mtatifu Benidikto wa kumi na sita kuwa
mwangalizi wa jimbo la mpanda hadi hapo taratibu nyingine
zitakapofanyika.
Kwa upande wake Askofu Kyarusi
naye alimteua Padri Patrick Kasomo kuwa msaidizi wake kwaambapo awali
Padri Kasomo alikuwa msaidizi wa Askofu Kikoti aliyefariki
dunia.kuteuliwa kwa Askofu Kyarusi ni kutokana na kuwa awali alikuwa
akitumika hadi mpanda kwabla haijapewa hadhi ya kuwa jimbo.uteuzi
huoulitamuka na Balozi wa Papa hapa nchini Askofu Franssco Padino.
No comments:
Post a Comment