Friday, November 23, 2012

Mkewe Gbagbo kufikishwa the Haque

Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi Simone, Gbagbo.
Bi Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais nchini humo.
Mumewe tayari amekamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo iliyoko The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.
Takriban watu 3,000 waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbo kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Gbagbo na mkewe walikamatwa ndani ya handaki moja Aprili mwaka wa 2011, miezi mitano, baada ya uchaguzi wa urais.
Wanajeshi wa rais wa sasa wakiungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walianzisha msako mkali dhidi yao, baada ya kujificha ndani ya ikulu ya rais.
anatuhumiwa kuhusika na mauaji, ubakaji, dhuluma na ngona na kuwadhulumu wapinzani wa serikali miongoni mwa mashtaka mengine mjini Abidjan.
Licha ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti chochote cha kisiasa, ripoti zinasema kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na kuwa alimshawishi mumeo kutokubali matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo, 67, alihamishwa hadi The Haque mwaka uliopita, na kuandikisha historia ya kuwa rais anayeondoka wa kwanza kufikishwa mbele ya mahakama hiyo ya ICC.
Rais huyo wa zamani amekanusha madai hayo yote.
Kabla ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na mkewe mwenye umri wa miaka 63, walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast kuhusiana na uhalifu wa kiuchumi, ikiwemo mdai ya kupora mali, wizi wa nguvu na kutumia rasilimali za umma kwa njia mbaya
Mahakama hiyo ya ICC sasa imetoa wito kwa serikali ya Ivory Coast, kumusafirisha Bi Gbagbo ili afunguliwa mashtaka huko the Haque.


 MWONGOZO WA UANDISHI WA HABARI
 
Watangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC

Chuo cha Uandishi Habari cha BBC (BBC College of Journalism ) kwa kushirikiana na Idhaa ya Dunia ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC World Service) wanafurahia kuzindua mwongozo maalum wa uandishi wa habari katika lugha Kiswahili.
 
Kiswahili ni miongoni mwa lugha sita zinazohusika na awamu hii, nyingine ni kiindonesia, kipashto, kiuzbek, kiazeri na kikyrgyz.
Matoleo haya mapya yanaongeza lugha zaidi ya zile ambazo tayari zilizindua mwaka mmoja uliopita: kiarabu, kichina, kiurdu, kirusi na kifaransa.
Miongozo hii inatumia uzoefu mkubwa na utaalam wa miaka mingi kutoka miongoni mwa waandishi wa BBC, na sasa tunayo furaha kuweza kutoa fursa kwa waandishi wa habari kote duniani kunufaika kwa utaalam huu.
Miongozo hii inatoa msisitizo kuhusu, pamoja na mengine yote, jinsi gani uandishi wa habari unategemea sana lugha kujitosheleza.
Kuweza kujadili misingi ya uandishi habari, inabidi kwanza kuelewa nafasi ya lugha katika kubainisha mawazo fulani katika misingi hiyo.
Hii ni hatua ya kwanza, tungependa kurasa hizi zikiongezeka na kuwa miongozi kamili ya uandishi habari na lugha.
Pata maelekezo jinsi ya kutumia
kwa ajili ya kurekodi sauti.

No comments: