Michezo



 Mshambuliaji wa Barcelona, Leo Messi amesema ameshangazwa na watu wanaosema amechangia kwa kocha mpya Gerardo Martino kujiunga na timu hiyo.

"Sijui lolote kuhusu kocha, nimesikia wakisema nilishawishi aje, lakini hilo lilikuwa ni suala juu ya uwezo wangu na uongozi ndiyo ulikuwa na uamuzi kwa kila kitu kilichokuwa kinaendelea.

"Naweza kusema simjui kocha na sijawahi kukutana naye hata mara moja. Ninachojua amekuwa kocha mwenye mafanikio akiwa na Newell Old Boys na timu ya taifa ya Paraguay. Kwangu ni jambo zuri,” alisema Leo.


Kabla ya kocha huyo maarufu Tata, kujiunga na Barcelona kulikuwa na taarifa kuwa Messi alikuwa akimpigia debe ajiunge na timu hiyo kwa kuwa ni raia wa Argentina lakini pia alikuwa anafundisha timu iliyomlea ya Newell Old Boys.

Lakini Messi aliondoka Argentina akiwa na miaka 13 kabla ya kocha huyo hajaanza kuifundisha na akapelekwa Hispania kwa matibabu na baadaye kujiunga na Barcelona.



HABARI NA MATUKIO ZAIDI, KABLA NA BAADA YA MECHI HIYO YA THE CRANES NA STARS, SOMA CHAMPIONI JUMATATU








BOBAN..
Simba imeondoka leo kwenda Tanga kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.

Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amethibitisha Simba kuondoka mapema jijini Dar leo na kikosi cha wachezaji 25 kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo huo.

Mechi hiyo itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na Juma Nyosso na Haruna Moshi wataivaa timu yao ya zamani kwa mara ya kwanza.
NYOSSO

Boban na Nyosso wamejiunga na Coastal Union baada ya kuonyesha kutoelewana na uongozi wa Simba.

Boban aliachiwa aondoke ikionekana hana uelewano na viongozi wa Simba ambao hata hivyo hawakutoa ufafanuzi kwa nini wanamuacha.

Lakini Nyosso aliamua kuvunja mkataba mwenyewe baada ya kuona haelewani na uongozi wa Simba na haukuonyesha unataka kuendelea naye au la.

Mechi hiyo ya kesho huenda ikavuta watu wengi zaidi kutokana na wachezaji hao kucheza dhidi ya Simba.
Lakini Simba na Coastal Union zimelenga kujiimarisha zaidi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013-14.







Matumaini ya Watanzania kwa Taifa Stars huenda ingeweza kubadili matokeo mjini Kampala na kusema mbele kucheza Kombe la Chan mwakani nchini Afrika Kusini, yameishia hewani.
Stars imelalala kwa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wake The Cranes mjini Kampala na kufanya iwe imepoteza kwa jumla ya mabao 4-1.
Stars ambayo ilipoteza mechi ya kwanza kwa bao 1-0 jijini Dar, leo ilikwenda mapumziko ikiwa na inaongoza kwa bao moja lililofungwa na Amri Kiemba.
Lakini kipindi cha pili Waganda walionekana kubadilika na mapema tu wakapata bao la kwanza na bao la pili lililofungwa kwa mkwaju wa penalti.
Kosa la kuzubaa na mpira wakati Stars inashambulia kuliifanya Uganda ifanye shambulizi la kushtukiza na kufunga kwa ulaini bao la tatu.
Baada ya hapo, wenyeji walionekana kupoteza muda huku wachezaji wa Stars wakimlalamikia mwamuzi kutokana na kuonyesha wazi alitaka wenyeji washinde.
Mara ya mwisho The Cranes kupoteza mechi katika Uwanja wa Namboole ilikuwa ni mwaka 2004 walipofungwa na Afrika Kusini na baada ya hapo wamekuwa wakishinda au kutoka sare.
Hata hivyo, Stars pia ilionekana kukosa mipango kila ilipofika mbele kama ilivyokuwa katika mechi ya kwanza jijini Dar.
Wachezaji wa Stars waliendelea kucheza kama wale waliokata tamaa kabisa na mara nyingi walipokonywa mipira karibu kila mara.

Baada ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho, Kocha Mkuu, Sredojevic Milutin 'Micho' aliyewahi kuinoa Yanga alionekana kuchanganyikiwa kwa furaha na kukimbia kama mwendawazimu.
Mara ya mwisho Stars ilicheza michuano ya Chan mwaka 2009 nchini Ivory Coast na ikatolewa katika hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Zambia mjini Bouake.

No comments: