Monday, November 26, 2012

Kabila ataka M23 waondoke Goma


Serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo inasema haitazungumza na wapiganaji wa M23 hadi waondoke mji wa Goma ambao waliuteka juma lilopita.
Wanajeshi wa serikali kabla ya mji wa Goma kutekwa
Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu mjini Kampala, Uganda, kuwasihi wapiganaji waondoke Goma.
Msemaji wa wapiganaji, Kasisi Jean-Marie Runiga, alisema wapiganaji wataondoka Goma baada ya mazungumzo ya amani lakini siyo kabla.
Rais Joseph Kabila wa Congo alikutana na wawakilishi wa wapiganaji mjini Kampala Jumamosi.
Wakuu wa Uganda wanasema yamekuwapo mawasiliano baina ya pande hizo mbili.

No comments: