Saturday, March 8, 2014

HIZI NDIZO HOTEL 10 BORA ZAIDI DUNIANI...NI NZURI BALAA


Hizi ni hoteli kumi ambazo kama ukipata bahati ya kulala walau kwa siku moja tu, unaweza kuhisi umeingia peponi kabla ya muda wako. Tazama picha za hoteli 10 zinazovutia zaidi duniani.
1. Marina Bay Sands, Singapore
Mpaka kukamilisha kuijenga hoteli hii, bajeti ya dola bilioni 8 zilitumika.
2. Sheraton Huzhou Hot Spring Resort
3. Resorts World, Sentosa, Singapore
Dola bilioni 6.5 zilitumika kujenga hoteli hii na ndani kuna hoteli sita zinazojitegemea.

 ENDELEA KUSOMA HABARI HII KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 
4. Mardan Palace, Lara, Antalya, Uturuki
Hoteli hii ilizinduliwa mwaka 2009, na uzinduzi wake ulikuwa mkubwa zaidi katika historia ya uzinduzi wa hoteli duniani.
5. City Of Dreams, Macau, China
Kama panavyoitwa, ‘Jiji la Ndoto’ hapa utakutana na hoteli 3 kubwa, Hard Rock Hotel, Grand Hyatt Macau, na Crown Towers.
6. The Venetian, Macau, China
Panahusu mazungumzo ya casino, basi The Venetian, Macau ni baba lao. Ikijengwa kwa dola bilioni 2.4, ilipomalizka ilikuwa na casino kubwa zaidi duniani.
7. The Cosmopolitan, Las Vegas
Hii ni sehemu ambayo maceleb hujivinjari zaidi. Ilijengwa kwa gharama ya dola bilioni 4.9.
8. Emirates Palace, Abu Dhabi
Ujenzi wa kiota hiki ulitumia gharama ya dola bilioni 5 na kuifanya kuwa miongoni mwa majengo aghali zaidi.
9. Burj Al Arab, Dubai
Ukiitaja ‘Dubai’, kulitaja jina Burj Al Arab huwezi kuliepuka. Ujenzi wake ulitumia miaka sita kwa gharama ya dola milioni 650. Na ilipofunguliwa mwaka 2000, jengo hili likawa refu kuliko majengo yote duniani.
10. Atlantis, The Palm, Dubai
Ujenzi wa jengo hili uligharimu dola bilioni 1.5

Tuesday, March 4, 2014

MAAJABU YA DUNIA ! MTOTO WA MIAKA 5 ALIYEBEBA UJAUZITO NA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME NCHINI PERU.






World's Youngest MotherLINA akiwa amelezwa mara baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji.























LINA MEDINA
 
LINA AKIWA MJAMZITO.
  
LINA AKIWA NA MTOTO NA MMOJA WA MADAKTARI WALIOMFANYIA UPASUAJI NA KUJIFUNGUA MTOTO HUYO KATIKA KITANDA CHA WATOTO CHA MATAIRI MANNE.

LINA Medina aliyezaliwa tarehe 27 Sept. 1933, huko Ticrapo, mkoa wa Huancavelica, nchini Peru, anatajwa kua Mama mwenye umri mdogo kuwahi kutokea katika historia ya Ulimwengu.

Tarehe 14 Mei 1939 Lina akiwa na umri wa miaka 5 na miezi 7, alijifungua mtoto wa Kiume aliy

e mpa jina la Gerardo Medina.

Ilianzaje? 

Mwanzoni mwa mwezi Machi 1939 wazazi wa Lina ~ Tiburelo Medina na Victoria Losea waliamua kumpeleka Hospitali baada ya kuona tumbo likiongezeka kupita kiasi.

Wazazi wa Lina walidhani huenda ana uvimbe tumboni, lakini madaktari waligundua kua alikua ana ujauzito wa miezi 7. 

Dr. Gerardo Lozada aliamua kumpeleka Lina kwa wataalam zaidi nao wakathibitisha kua ni kweli alikua mja mzito.

Alizaaje ?.

Mwezi mmoja na nusu baada ya kupelekwa hospitali kwa mara ya kwanza, Lina alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji, kutokana na njia yake ya uzazi kua ndogo. 

Upasuaji ulifanywa na Dr. Lozada, Dr. Busalleu, na Dr. Colareta.

Alivunja Ungo lini?.

Dr. Edmundo Escomel alitoa ripoti kamili juu ya kesi ya Lina kupitia jarida maalum la maswala ya kiafya na matibabu liitwalo La Presse Médicale. 

Ripoti hii ilibainisha kwamba Lina alianza kupata siku zake tangu akiwa na umri wa miezi 8, alitofautiana na ripoti ya awali iliyosema kua amekua akiona siku zake tangu alipokua na umri wa miaka 3. 

Ripoti hii pia ilisema kua Lina alianza kuota maziwa akiwa na umri wa miaka 4, alipofikisha miaka 5 nyonga yake ilikua imesha tanuka.

Alizaa mtoto gani ?.

Mtoto alizaliwa na uzito wa kilo 2.7 na alipewa jina la daktari wake Gerardo.

Gerardo alilelewa akijua kwamba lina ni dada yake lakini alikuja kujua ukweli akiwa na umri wa miaka 10.


Gerardo aliendelea kukua akiwa mtoto mwenya afya njema lakini alifariki mwaka 1979 akiwa na miaka 40 kwa ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalam la Bone marrow.

Nani Baba wa mtoto ?.

Lina hajawahi kumtaja baba wa mwanae wala mazingira yaliyopelekea yeye kupata mimba. 

Dr. Escomel alipendekeza kwamba inawezekana hata Lina mwenyewe alikua hajui, na kusema kuwa hakutoa majibu yanayojitosheleza.

Tuhuma kwa baba mzazi: 

Hata hivyo Baba mzazi wa Lina alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Unyanyasaji wa kingono wa mtoto (Child Sexual Abuse) lakini aliachiwa baadae baada ya kukosekana ushahidi wa kutosheleza. 

Na hivyo basi Baba halisi aliyempa mimba Lina hakuwahi kujulikana.

Maisha ya Lina baadae:
Miaka kadhaa baadae Lina aliolewa na Raúl Jurado ambaye mwaka 1972 walipata mtoto wa kiume. 


Lina yupo hai mapaka sasa na anaishi maisha ya kimasikini huko Lima nchini Peru

UTAFITI !!!!: KUKOSA KIFUNGUA KINYWA ASUBUHI NI MOJA YA SABABU 5 ZA KUUDHURU UBONGO WA BINADAMU.


  1. Kukosa Kifungua Kinywa asubuhi
    Watu wanaokosa kifungua kinywa asubuhi wanapata upungufu wa kiwango cha sukari kwenye damu. Hii husababisha upungufu wa madini (nutrients) kwenye ubongo na hatimaye ubongo hudhoofika.
  2. Kula kupita kiasi:
    Inasababisha kukaza kwa misuli au mishipa ya Ubongo na hatimaye hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa fahamu.Afya ya Ubongo
  3. Kuvuta Sigara:
    Kwenye sigara kuna kitu kinaitwa Nikotini ambayo ndani yake kuna chembechembe ambazo zina sababisha makunyanzi kwenye ubongo na kisha kudhoofu.
  4. Kutumia Sukari nyingi:
    Matumizi ya sukari nyingi husababisha matatizo katika mfumo wa unyonyaji wa Protini na Madini joto mwilini na kusababisha ugonjwa wa Utapiamlo ambao pia huingilia mfumo wa fahamu
  5. Kuvuta Hewa chafu:
    Ubongo ndio mtumiaji mkubwa wa Oxijeni tunayo ivuta. Unapovuta hewa chafu unapunguza mgawo wa Oxijeni kwenye Ubongo na hatimaye kupunguza ufanisi wake

WATANI WAFANYA MZAHA KATIKA MSIBA WA MCHEZAJI WA ZAMANI NA MMOJA WA WAANZILISHI WA TIMU YA MAJI MAJI YA SONGE

Watani wa Kiyao wakimfuatisha marehemu alivyokuwa akitembea enzi ya Uhai wake. Mfiwa uruusiwi kufuta huo unga ukifuta tu wanakuja na debe zima wanakumwagia bora uwe mpole. MZEE Abdala Alli alikuwa mmoja wa waanzilishi wa timu ya Majimaji ya Songea wana Lizombe, yeye na wenzake watatu ndiyo walianzisha timu hiyo, Alikuwa mzee Mbegambega, Mzee Mshamu wakiongozwa na Mhe, Laurensi Mtazama Gama hao wote kwa sasa ni marehemu. Mmoja wa watani wa Kabila la Wayao akimpaka unga usoni mtoto wa Kwanza wa kiume Hamisi Abdala Alli, Siyo Igizo ni utani kati ya Wamwela na Wayao. Mfiwa... more »