Waandamanaji wamekesha usiku
kucha katika medani ya Tahrir mjini Cairo kuelezea hasira zao dhidi ya
tangazo la rais wao anayezingatia itikadi za kiislamu Mohammed Morsi
kujipatia madaraka makubwa.
Walikesha wakiimba nyimbo za kumlaani rais pamoja na vuguvugu lake la kiislamu la Muslim Brotherhood.Jana Jumanne, maelfu ya waandamanaji walifurika katika medani hiyo wakiandaa mandamano kadhaa huku wakisema watamkiuka rais Mursi huku wakipinga mamlaka aliyojilimbikizia.
Maandamano mengine ya kumpinga rais Morsi yamefanyika katika maeneo mbali mbali nchini humo.
Bwana Morsi amejaribu kumaliza mzozo huo kwa kuahidi kuwa madaraka yake yatakuwa na kikomo.
Vuguvugu la Muslim Brotherhood, ambalo bwana Mursi ni mwanachama, liliakhirisha mkutano wao siku ya Jumanne likisema linataka kuzuia taharuki kutanda miongoni mwa wanachi.
Wanaomuunga mkono bwana Mursi wanasema kuwa sheria hiyo inahitajika ili kulinda mafanakio yaliyotokana na mapinduzi ya kiraia dhidi ya utawala wa Mubaraka na idara ya mahakama ambayo ilikuwa na watu wanaomuunga mkono rais aliyng'olewa mamlakani.
Waandamanaji wanasema kuwa vuguvugu la Muslim Brotherhood limeyateka nyara faida zilizotokana na mapinduzi ya kiraia
No comments:
Post a Comment