Friday, November 30, 2012

KAULI YA DAVID KAFULILA KUHUSU MKUU WA MKOA WA KIGOMA.


David Kafulila.
Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini DAVID KAFULILA amesema anakusudia kupeleka hoja binafsi kwenye kamati ya maadili ili iweze kumchukulia hatua mkuu wa mkoa wa Kigoma luteni kanali mstaafu ISSA MACHIBYA kwa madai ya kulidhalilisha Bunge ambalo ni muhimili wa serikali.
Akiwa kwenye kongamano la kujadili masuala ya uwekezaji katika kanda ya ziwa Tanganyika lililofanyika mkoani Katavi hivi karibuni, mkuu huyo wa mkoa wa Kigoma anadaiwa kutoa kauli kuwa wabunge ambao hawatafuata maelekezo yake kama mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya watapigwa pingu kama raia wa kawaida.
Kanali mstaafu Issa Machibya.
Kauli hiyo imeonekana kuwakwaza wabunge wa mkoa wa Kigoma ambao wamesema huko ni kukiuka sheria na kuudhalilisha mhimili wa Serikali na hivyo mbunge huyo wa Kigoma kusini amemtaka mkuu huyo wa mkoa kuomba radhi vinginevyo atamshitaki.
Mbunge Kafulila Amesema anashangaa ni kwa nini spika wa bunge bi.Anne Makinda amekaa kimya bila kusema lolote juu ya kauli hiyo.

No comments: