Taarifa kutoka Somalia zinaeleza
kuwa watu kama 12 wameuwawa katika mapigano baina ya jeshi la serikali
na wapiganaji wa Al Shabaab karibu na mpaka wa Kenya.
Kila upande unadai kuwa upande wa pili umepata hasara kubwa zaidi.
Al Shabaab bado wanadhibiti maeneo mengi ya kusini na kati mwa Somalia ingawa wamekimbizwa Mogadishu awali mwaka huu.
Mabomu yaripuliwa kambini Kaduna
Jeshi la Nigeria linasema kuwa mabomu yaliyotegwa kwenye magari mawili yameripuliwa ndani ya kambi ya karibu na mji wa Kaduna, kaskazini mwa nchi.
Mshambuliaji wa kwanza alikuwa kwenye basi lilojaa mabomu na aligonga kanisa wakati ibada ya Jumapili ikimalizika.
Dakika 10 baadae gari lilotegwa bomu liliripuka nje ya kanisa.
Jeshi la Nigeria limelaumu kundi la wapiganaji wa Boko Haram.
Msemaji wa jeshi alisema mashambulio hayo ndani ya kambi ilioko Jaji, yatia aibu.
Boko Haram inapigana kuipindua serikali ya Nigeria, ili kuweka sheria kali za Kiislamu.
No comments:
Post a Comment