Tuesday, May 28, 2013

HII NDIO INAYODAIWA KUWA NI SABABU YA KUSABABISHA KIFO CHA NGWAIR SOUTH AFRICA.



http://3.bp.blogspot.com/-WhLAsO1Z0Cg/TftKo0GeYeI/AAAAAAAAAkY/Z6SKc0_7gz0/s1600/NgweaWEB.jpg 
ALBERT MANGWEA.
 
RIPOTI KAMILI
TAARIFA Nilizo Pata Kutoka South Africa Kutoka Kwa Hussein Original Ambaye Yupo Pretoria Amesema Ngwear Amefariki Leo Asubuhi. 
Alikuwa Ghetto Moja Na Msanii M To The P.
Walivyokwenda Kuwagongea Asu

buhi Walikuta Ngwear
Amefariki Na M To The P Amepoteza Fahamu Kabisa. 
Pia Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa Watu Wa Karibu Wa Ngwear Huko South Africa.  
Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi Dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.

ADAIWA KUKUTWA ANAUZA SEHEMU ZA SIRI ZA WANAUME !.


JUMA MTANDA at JUMA MTANDA - 3 hours ago
*Mtuhumiwa Samuel Banda* *Foster Mangani* * * * * * * * JESHI la polisi nchini malawi wanamshikilia kijana mmoja baada ya kumkuta akiuza sehemu ya siri ya mwanaume.* kijana huyo mwenye miaka 24 alikamatwa baada ya wananchi kutoa ripoti kituo cha polisi kuwa kunamzee kalala relini huku akiwa anatokwa damu nyingi ndipo polisi walipofika eneo la tukio na kumkuta mzee huyo akiwa hio na kuamua kumkimbiza hosipitali. Baada ya kufikishwa hosipitali ndipo madaktari walipo gundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri,mara moja madakt... more »

Monday, May 27, 2013

AJALI YA GARI KUACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO



Watu nane wamefariki dunia  baada ya gari walilokuwa wanasafiria kutoka kijiji cha mputa wilaya ya Namtumbo kwenda Songea  kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Hanga eneo la Bombambili wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma .

Roli hilo lilikuwa limebeba magunia ya ufuta, mpunga wakiwemo na abiria

 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma  Deusdedit  Nsimeki amesema ajali hiyo imetokea jana Tarehe 26.05.2013 majira ya saa nne na nusu( 4:30 usiku  katika kijiji cha Hanga eneo la bombambili mkoa wa Ruvuma, chanzo cha ajili hiyo ni mwendokasi na dereva kuendesha gari akiwa amelewa,
Ajali hiyo  imehusisha gari lenye namba za usajili T.677 ADL  aina ya Isuzu lori , mali ya mfanyabiashara wa mazao maarufu kwa jina la Mtazamo. likiendeshwa na dereva aitwae CHRISTIN NYONI mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa LIHULI SONGEA,
Baada ya ajali hiyo kutokea dereva wa gari hilo amekimbia na kutelekeza gari porini hadi sasa jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya jitihada za kumtafuta ili sheria ifuate mkondo wake.

Kamanda wa Polisi amesema gari  hilo liliacha njia baada ya kugonga daraja na kupinduka na kusababisha vifo vya watu nane(8)  na majeruhi kumi na moja (11) ambao
wote wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa matibabu.

Kutokana  na ajali hiyo mbaya kamanda wa polisi wa  Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Nsimeki ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya mizigo kutopakia mazao pamoja na abiria na atakayekiuka atachukiliwa hatua kali za kisheria.
Pia ametoa wito kwa wamiliki/wasimamizi wa magari kuwa wanatakiwa kuhakikisha magari ya mizigo,mazao hayapakii abiria na atakaye kiuka agizo hili hatafikishwa mahakamani mala moja 
ambapo

OMBAOMBA ANAYETAPELI WATU KWA KUIGIZA MLEMAVU NA KUWA HANA MKONO MMOJA NA MGUU MMOJA, AONJA JOTO YA JIWE WANANCHI WAMSHUSHIA KIPIGO CHA NGUVU.


Wananchi eneo la Miyomboni  wakiwa  wamembana omba omba  huyu tapeli kuonyesha  mikono yake  yote
'' Huwa  unasema wewe  ni  mlemavu  huna mkono mmoja   hii nini ....nyosha  juu  watu waone utapeli  wako"
Hapa  ni  kipigo  kikiendelea
Tapeli  huyo akitaka  kujinasua  kutoka  mikono ya  wananchi  wenye hasira  kali
Hapa  baada ya  kupata upenyo akivaa nguo  zake
Hapa  akiwa ameachiwa  na kuanza kutimua mbio
Baada ya  kuchezea kichapo  tapeli huyo  sasa anajaribu  kuficha aibu

OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO KWENYE TUKIO LA KWANZA

Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo
Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya mtandao huu leo 
AMA Kweli  mwisho  wa  utapeli ni aibu  kubwa na   wahenga walinena   kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo kwa  wakazi  wa Miyomboni mjini Iringa wamepata  kushuhudia  kituko cha mwaka  baada ya watu  waliochoka  kuvumilia vitendo vya  kitapeli  vinavyofanywa mzee  mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
 
Tapeli  huyo  mbali ya  kuumbuliwa kwa  kutakiwa  kuonyesha miguu  yake  yote  pamoja na mikono  yake  yote  bado amepata  kuchezea  kichapo  kiasi cha  kunusurika  kuuwawa na wananchi  hao wenye hasira  kali.
 
Tukio la mzee  huyo  kubainika kama ni tapeli kwa mara  ya kwanza  mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com ndio ulipata  kufichua siri  hiyo ya omba omba  huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano  wa mlemavu .
 
Kutokana na kufichuliwa kwa  siri  hiyo ya  kujiigiza  kuwa ni  omba omba mlemavu wananchi wamekuwa  wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na  kumtimua  mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua  kumkimbiza  kutoka eneo la Hazina  Ndogo  hadi miyomboni na kuanza  kumpa  kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo  vyote kuwa  si mlemavu
Tapeli  huyo mbali ya  kujifanya ni mlemavu  wa  viungo  wakati mwingine huwa anajifanya  ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama  mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu  mmoja na  kuwaomba  watu fedha za matibabu .
 
Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu).
 
Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo  kutokana na  kichapo alichokipata  na kuumizwa  vibaya usoni .
 
Hata  hivyo  inasemekana  mzee  huyo  amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali  mbali kutokana na mbinu yake ya  kufuru anayoifanya  kuwa ni mlemavu  wakati si mlemavu na  kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya  kiuchumi kuliko  kuwaigiza  walemavu na  kuwa iwapo atarudia na  kukutwa akifanya  hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema  wananchi hao ambao hata hivyo mtandao huu uliwaomba kufanya  hivyo.
 
Aidha  anadaiwa chanzo cha  kichapo  cha  leo kwa mzee  huyo tapeli ni mmoja kati ya  mpenzi  wake ambae  alikuwa amemsusa na  kuhamia kwa mpenzi mwingine  kuueleza umma kuwa  huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi  wake ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea  wananchi kufanya udadisi.
 
Kabla kufukuzwa na kuchezea  kichapo tapeli huyo alifukuzwa  eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya  vijana  wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona  viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
 
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada.
CHANZO: FRANCIS GODWIN WA MATUKIO DAIMA

Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka


 

Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako


*******
Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
Matokeo ya awali ndiyo chimbuko la kupitiwa upya baada ya wadau kuyalalamikia na kumlazimisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuunda tume ya kuyachunguza Februari 23, mwaka huu.
Kabla ya tume hiyo kuhitimisha shughuli zake, ilitoa taarifa ya awali ambayo ilipendekeza kufutwa kwa matokeo hayo kwa maelezo kwamba Necta ilitumia kanuni mpya ya kukokotoa matokeo bila kushauriana na wadau.
Serikali ilitoa taarifa bungeni kwamba imeamua kufuta matokeo ya 2012 na kuamuru yapangwe upya kwa kufuata madaraja yaliyotumika mwaka 2011.
Ratiba ya Bunge
Wakati hayo yakiendelea, ratiba ya vikao vya Bunge la bajeti imefanyiwa marekebisho na kusogeza mbele zamu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo awali, ilikuwa imepangwa kusoma hotuba yake ya makadirio ya matumizi leo, badala yake nafasi hiyo imepewa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wizara ya Elimu sasa imepangiwa kuwasilisha hotuba yake Juni 4 mwaka huu, hatua ambayo inatajwa kwamba lengo ni kusubiri kutangazwa kwa matokeo hayo ya kidato cha nne na kidato cha sita.
Wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alipokutana na wabunge wa chama chake Mei 19, mwaka huu mjini Dodoma, walisema hawako tayari kujadili hotuba ya wizara hiyo hadi matokeo ya kidato cha nne na sita yatakapotangazwa.


MWANANCHI

FREEMASONS NA HARAKATI ZA KIDINI DUNIANI


KUTOKANA na familia ya Freeman Illuminati bloodline kuanzisha chama cha ‘Priory de Sion’kilichokuwa na lengo la kuingiza mafundisho machafu ndani ya imani ya kweli, dunia ililazimika kusubiri awamu nne za utawala wa serikali moja kabla ya kuunganisha dini na serikali na kuwa kitu kimoja. Kumbuka kwamba Mungu hutumia namba 1 hadi 12 ambapo namba 4 humaanisha ‘ukomavu na kuvunwa kwa mazao’ – rejea Marko 4: 26 kwa mbegu njema na Yakobo 1:14,15.

Rais Nimrodi wa serikali ya awamu ya kwanza ndiye aliyepanda mbegu ya ‘tamaa’ ya kuanzisha serikali na dini moja itakayoitawala dunia nzima. ‘Tamaa’ ya rais Nimrodi ilitengeneza ‘mimba’ na kupelekea awamu ya pili ya serikali moja ya dunia chini ya Waamedi na Waajemi wakati huo Dario akiwa ndiye rais na ikulu ya serikali hiyo ikiwa katika eneo la Iran ya leo. Baada ya miongo kadhaa kupita, ‘Mimba’hiyo ilileta mtoto aliyepewa jina la ‘dhambi’ wakati wa awamu ya tatu ya serikali moja ya dunia iliyoitwa Uyunani chini ya rais Alexander mkuu aliyeweka ikulu yake huko Ugiriki. Historia inatuambia kwamba rais Alexander mkuu alikuwa katili na aliyefanikiwa kuua mamia kama sio maelfu ya watu duniani kote.

Hatimaye mbegu ya ‘tamaa’ iliyopandwa na rais Nimrodi wa serikali ya awamu ya kwanza ilipotengeneza‘mimba’ na kuzaa mtoto ‘dhambi’, mtoto huyo alikomaa baada ya kufikisha umri wa utu uzima. Sasa hakuitwa ‘mtoto’ tena bali jina lake lilibadilika na kuitwa‘mauti’. Kumbuka kwamba kuna hatua nne za kukua na kukomaa kwa mbegu hadi wakati wa kuvunwa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati dunia yetu iliposhuhudia awamu nne za serikali moja ya dunia ambapo katika awamu ya nne palitokea mavuno yaliyoleta mazao ya muungano wa serikali na dini.

Ulikuwa ni utawala wa serikali ya awamu ya nne (Roman empire) chini ya rais Constantine aliyeweka ikulu yake huko Roma ndipo imani ya kweli ilipokufa baada ya rais huyo kuanzisha dini iliyochanganya ukweli na uongo kwa kutumia kanuni ya‘Thesis x Antithesis = Synthesis. Imani ya kweli ilikuwa ni ‘Thesis’ wakati imani ya kipagani iliyoanzishwa na Nimrodi ilikuwa ni ‘Antithesis’. Imani hizi mbili zilichanganywa na rais Constantine na kuzaa kitu kinachoitwa ‘Synthesis’ yaani mchanganyiko wa ukweli na uongo. Hiyo ilikuwa ni baada ya miaka mingi kupita tangu rais Nimrodi alipotamani kuanzisha mfumo wa utawala uliunganisha serikali na dini na kuwa kitu kimoja. Hiyo ilikuwa ni awamu ya nne ya utawala wa serikali moja ya dunia. Naam! Dini iliyoanzishwa huko Roma wakati wa awamu ya nne ya utawala wa serikali moja ya dunia chini ya rais Constantine ilikuwa ni matokeo ya mbegu ya ‘tamaa’ ya rais Nimrodi ya kuanzisha mfumo wa serikali iliyoungana na dini katika utawala wa dunia nzima.

Jambo hilo la kuunganisha serikali na dini pamoja na kuchanganya ukweli na uongo lilipigwa vita vikali na ‘waprotestant’ ambao hawakuwa tayari kuona ukweli wa neno la Mungu ukichanganywa na uongo. Hata hivyo ‘waprotestant’ hao hawakufanikiwa kutenganisha serikali na dini na ndipo wakamua kujitenga na dini iliyokuwa imeungana na serikali ili wapate kumuabudu Mungu katika roho na kweli.

Ilipofika mwaka 1798 kulitokea badiliko katika serikali iliyoungana na dini baada ya rais na kiongozi wa dini kukamatwa na kuuawa huko ufaransa. Baada ya kifo cha rais na kiongozi wa dini wa serikali moja ya dunia, ilionekana kana kwamba ndio mwisho wa mfumo wa utawala uliounganisha serikali na dini. Lakini haukuwa mwisho kwa sababu liliundwa taifa moja katika mji wa Roma likiwa linaendeleza mfumo wa kuunganisha serikali na dini. Taifa hilo likapewa jina la Vatican. Ndioo! Vatican ni nchi inayotawalaiwa na Papa akiwa ndiye rais na kiongozi wa dini pia. Sasa jina la serikali hiyo likaitwa ‘Roman Catholic’ yaani ‘ulimwengu wa Kirumi’. Maana ya neno ‘catholic’ ni ‘universal’ au iliyoenea dunia nzima. Serikali hii imeenea dunia nzima kutokana na uwepo wa wawakilishi (mabalozi) wa taifa hilo duniani kote. Ukilinganisha na mataifa mengine katika eneo la mraba, inawezekana taifa hili ndilo dogo kuliko mataifa mengine duniani kote lakini ni taifa lenye nguvu kubwa kuliko mataifa yote – usishangae!

Zimekuwepo juhudi za kuhakikisha kwamba dunia nzima inarudi kwenye mfumo wa utawala wa serikali na dini. Freemasons wamekuwa kwenye mipango ya muda mrefu latika kuhakikisha kwamba serikali moja ya dunia itakayounganisha dini na uchumi kwa pamoja inaundwa haraka iwezekanavyo. Serikali hiyo itakuwa imejengwa kwenye msingi uliowekwa na rais wa kwanza katika awamu ya kwanza ya utawala wa serikali moja ya dunia. Itakumbukwa kwamba rais Nimrodi alianzisha dini iliyoabudu miungu (sayari) 36 ambapo jumla ya miungu hao ilileta namba 666.

..... Safari ijayo tutaitazama namba 666 na uhusiano wake na Freemasons .... Endelea kuwa na NDGSHILATU BLOG mahala popote na wakati wowote .....

FREEMASONS NA HEKA HEKA ZA MWISHO WA DUNIA
Naam! Disemba 21, 2012 imepita; Sayari yetu haikugongwa na kupasuka na Hatukuona mwisho wa dunia! Lakini ni nini kimetokea? Ilifanyika mikutano kadhaa katika pande nne za dunia. Moja ya mikutano hiyo ni ule uliofanyika Vatican siku 18 (6+6+6) kabla ya Disemba 21. Mkutano huo ulifanyika siku ya Disemba 3, 2012 ukiwahusisha wakuu wa kanisa Katoliki katika kile kinachojulikana kama ‘Pontifical Council for Justice and Peace’ ambapo kiongozi mkuu wa kanisa hilo Papa Benedict xvi ndiye aliyehutubia mkutano huo. Akihutubia makumi ya makadinali waliohudhuria kwenye mkutano huo Papa Benedict xvi alitoa wito wa kuundwa kwa serikali ya dunia (world government) itakayokuwa na mfumo mpya wa dunia (New world Order) kwa ajili ya kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi. Kiongozi huyo wa kanisa alikaririwa akisema kwamba kuna umuhimu wa kuundwa kile alichokiita: “construction of a world community, with a corresponding authority,” Kisha akaongeza kusema:The proposed body (World Government) would not be a superpower, concentrated in the hands of a few, which would dominate all peoples, exploiting the weakest. Maneno hayo yanamaanisha kuundwa kwa chombo cha dunia kitakachokuwa na mamlaka ya umma ambacho hakitakuwa chini ya watu wachache watakaowanyonya wanyonge. Itakumbukwa kwamba mwaka 2010 Papa Benedict xvi alitoa wito wa kuundwa kwa ‘Central World Bank’ itakayoshughulikia maswala ya fedha duniani kote.

Sasa msikilize muumini wa freemason na mfanyabiashara za kibenki bwana Paul Warburg akisema kwamba "We will have a world government whether you like it or not. The only question is whether that government will be achieved by conquest or consent." (maneno hayo aliyasema siku ya February 17, 1950, alipokuwa akilihutubia baraza la Seneti nchini Marekani).Warburg alimaanisha kwamba serikali ya dunia lazima ianzishwe, utake au usitake. Swali ni kama serikali hiyo itaanzishwa kwa makubaliano au kwa vita.

Mwaka 1992, Dr. John Coleman aliandika kitabu kinachoitwa ‘Conspirators Hierarchy: The Story of the Committee of 300’. Katika kitabu hicho Dr. Coleman anaainisha watu wanaohusika na mchakato mzima wa kuundwa kwa serikali moja ya dunia au New World Order. Katika ukurasa wa 161 Dr. Coleman anaelezea malengo ya kamati ya watu 300 (mwenyekiti wake akiwa ni mkuu wa kanisa duniani) na kusema:"A One World Government and one-unit monetary system, under permanent non-elected hereditary oligarchists who self-select from among their numbers in the form of a feudal system as it was in the Middle Ages. In this One World entity, population will be limited by restrictions on the number of children per family, diseases, wars, famines, until 1 billion people who are useful to the ruling class, in areas which will be strictly and clearly defined, remain as the total world population.

There will be no middle class, only rulers and the servants. All laws will be uniform under a legal system of world courts practicing the same unified code of laws, backed up by a One World Government police force and a One World unified military to enforce laws in all former countries where no national boundaries shall exist. The system will be on the basis of a welfare state; those who are obedient and subservient to the One World Government will be rewarded with the means to live; those who are rebellious will simply be starved to death or be declared outlaws, thus a target for anyone who wishes to kill them. Privately owned firearms or weapons of any kind will be prohibited."

Kwa ufupi maneno hayo yanamaanisha kwamba kutakuwepo na serikali moja na mfumo mmoja wa kifedha ambapo kiongozi wa serikali hiyo atachaguliwa na watu 300 wanaounda kamati kuu ya serikali hiyo. Idadi ya watu duniani itapunguzwa kwa kuanzishwa sharia za kuwa na idadi maalumu ya watoto katika familia ambapo mbinu itakayotumika kutekeleza lengo hilo ni kusababisha magonjwa, vita, njaa hadi idadi ya watu ifikie bilioni moja duniani kote. Kutaanzishwa mfumo mmoja wa kijeshi utakaosimamia sharia katika nchi zote ambapo mipaka yote ya nchi zote itaondolewa. Wale watakaokuwa watiifu katika serikali hiyo watawezeshwa kuishi; wale watakaokuwa wapinzani na waasi wataanchwa wafe kwa njaa au kuhumiwa kama wavunja sharia. Haki ya kumiliki silaha za aina yoyote itaondolewa’. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni watoto 20 na waalimu wao 6 waliuawa kwa kupigwa risasi katika shule moja huko Marekani. Baada ya tukio hilo serikali ya Marekani imeanza kupitia upya sheria za umiliki wa silaha kwa watu binafsi.

Rais Barack Obama aliyeshinda uchaguzi ulioshirikisha vyama 6 nchini Marekani amekwisha saini mabadiliko kadhaa ya sheria. Rais Obama amesaini sheria inayoitwa TARP (Troubled Asset Relief Program) ambapo chini ya sheria hiyo mabenki yote (Wall street) pamoja na mabenki ya kigeni yanakuwa katika dhamana kwa serikali. Sheria nyingine ni H.R 347 (House Resolution) au “Federal Restricted Buildings and Grounds Improvement Act of 2011,”. Sheria hii inazuia maandamano ya kwenda kwenye majengo ya serikali ikiwa ni pamoja na zuio la kuendeleza majengo na ardhi. Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Marekani (American Civil Liberties Union –ACLU)) wanaipinga vikali sheria hiyo kwamba inawagandamiza wanyonge. Sheria nyingine ni‘National Defense Authorization Act’ – NDAA. Sheria hii inampa nguvu na mamlaka rais wa Marekani kuamuru kukamatwa na kufungwa gerezani kwa mtu yeyote bila hata ya kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka. Kama ulikuwa unafikiri kwamba rais Morsi Mohamed wa Muslim Brotherhood Misri amejipatia madaraka makubwa kupita kiasi, basi yupo pia rais wa Marekani chini ya NDAA!

Najua wengi watanishangaa ninaposema kwamba uchaguzi wa rais Marekani ulishirikisha vyama 6 na sio viwili. Ili usiniulize maswali juu ya hilo, vyama hivyo ni: 1)Democratic –Baraka Obama; 2)Republican – Miti Romney; 3)Libertarian Party - Gary Johnson; 4) Green Party- Jill Stein; 5) Constitution Party - Virgil Goode; na 6) Justice Party - Rocky Anderson.Kwa nini vyama 6 – ni namba ya utawala wa freemason.Kwa nini vyama vingine havikusikika? Ni kwa sababu Illuminati ndio walioshikilia ‘media’ na wao ndio waamuzi wa nani atangazwe na nani hapana.

Nini maana ya wito wa kuundwa kwa ‘world community’ pamoja na ‘Central World Bank’ kutoka kwa Papa Benedict xvi? Ni kutimizwa kwa unabii wa Ufunuo 13:17. Haitawezekana kuzuiwa kuuza na kununua kama hakuna chombo kinachosimamia uchumi na fedha. Chombo hicho ni ‘Central World Bank’ (CWB). Lakini pia CWB haitakuwa na nguvu za kusimamia shughuli za kifedha kama hakuna serikali nyuma yake. Serikali hiyo ni ‘World Community Authority’ au ‘World Government’ yaani serikali ya dunia.

Wakati Papa Benedict xvi akitoa wito wa kuleta ‘haki na amani’ duniani, chuo kikuu cha Kiislamu (Sunn Al - Azhar University) kimetoa shukrani kwa Vatican kutokana na juhudi za kanisa Katoliki kwa kukemea vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani duniani, kutetea imani za watu wote pamoja na kuziwezesha dini zote kutumia alama na nembo kama utambulisho wa dini husika.

Akihojiwa na waandishi wa habari, Mahmoud Azab ambaye ni mshauri wa Sheikh anayesimamia kitengo cha mahusiano ya kidini (interfaith Dialogue) katika chuo kikuu cha Al-Azhar, aliwashukuru wote wanaotetea ukweli na heshima ya dini. Mahmoud Azab alikuwa akijibu hotuba iliyotolewa hapo kabla na msemaji wa Vatican Fr. Federico Lombardi. Kwa nini Mahmoud atoe shukrani kwa Papa kutokana na matumizi ya alama/nembo katika dini? Unaweza kuchunguza alama/nembo kwenye jengo la chuo kikuu cha Al-Azhar na jengo alipokaa Papa Benedict xvi akihutubia baraza la haki na amani Vatican. Unazikumbuka kanuni 3 wanazotumia freemasons kufanya kazi zao? Tafakari!

Itakumbukwa kwamba baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Benghazi na kuuawa kwa aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya kutokana na hasira za waumini wa kiislamu zilizotokana na kutolewa kwa sinema inayomkashifu SAW Mohammad (Innocence of Muslims), Fr. Federico Lombardi alitoa matamko na kusema kwamba: “profound respect for the beliefs, texts, outstanding figures and symbols of the various religions is an essential precondition for the peaceful coexistence of peoples”akiwa anamaanisha kwamba ili pawepo na amani kwa watu, kunatakiwa pawepo na kuheshimu imani, maandiko pamoja na alama/nembo mbalimbali zinazotumiwa na dini kama utambulisho wao.

Akielezea kwa nini pamekuwepo na mjadala kati ya Al-Azhar University na Vatican, Abdel Muti al-Bayoumi, mjumbe wa ‘Islamic Research Academy’ katika chuo kikuu cha Al-Azhar alisema kwamba mjadala huo hauhusiani na kauli ya Papa Benedict xvi aliyoitoa kwa kuwatetea Wakristo wa dhehebu la Christian Copts wa Misri ambao wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na kushambuliwa kwa sababu ya imani yao. Alipoulizwa kutoa kauli juu ya mjadala kati ya pande hizo mbili, Mahamoud Azab alisema, ““I have nothing to say on the subject at this present time” akimaanisha kwamba hawezi kusema juu ya mjadala huo kwa wakati huu. Hata hivyo Azab alikemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya waumini kwa kuchoma Biblia wakati wa maandamano yaliyofanyika kupinga sinema ya ‘Innocence of Muslims’.Aliwataka waislamu wote kuheshimu Torah, Injili na maandiko Matakatifu kwa sababu ndivyo alivyofanya mtume Mohammad SAW.
 
Kwa nini pawepo na mfululizo wa mijadala kati ya Al-Azhar University na Vatican; serikali ya Iran na Vatican na hata serikali ya Saud Arabia na Vatican?

Wiki jana nilielezea vyanzo vya baadhi ya makanisa. Sikuelezea historia ya kanisa la Roman Katoliki na lini lilianza.Lakini pia sikuelezea historia ya dini ya Kiislamu.

Kwa uchache kanisa la Roman Catholic ni kanisa la Roma, kama linavyojulikana, kanisa la Roma.Roma ni mji mashuhuri uliopo Italia. Mji wa Roma una historia ndefu katika dunia na ni mji uliotabiriwa na Mungu pia.

Dunia yetu imewahi kushuhudia ikitawaliwa na serikali moja katika awamu nne. Awamu ya kwanza ilikuwa ni serikali ya dunia iliyopewa jina la Babeli. Rais au mfalme wakwanza katika serikali hiyo alikuwa ni Nimrodi akifuatiwa na Nebukadneza pamoja na marais waliomfuata. Asili ya serikali hii ni mnara wa Babeli uliojengwa na mfalme wa kwanza wa Babeli, rais Nimrodi. Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya serikali ya dunia awamu ya kwanza ni Iraqi.

Awamu ya pili ya serikali ya dunia iliitwa Mede/Uajemi ambapo mmoja wa marais wa serikali hii aliitwa Dario.Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya serikali hii ni Iran ya leo. Awamu ya tatu ya serikali ya dunia iliitwa serikali ya Uyunani au Greece government. Mmoja wa marais mashuhuri katika serikali hii alikuwa ni Alexander mkuu (Alexander the Great). Awamu ya nne ya serikali ya dunia iliitwa‘Roman Empire’ au himaya ya Roma. Mmoja wa marais wa serikali hii alikuwa ni Constantine. Serikali hii ndiyo iliyotawala kwa muda mrefu kuliko serikali zote zilizoitangulia.

Wakati serikali hizo zinatawala dunia, dini ya kweli ilikuwa haijatikiswa hadi serikali ya Roma ilipoanza kutawala. Je, dini ya freemasons ilianza lini? Ukiondoa dini aliyoianzisha Mungu katika bustani ya Edeni, dini ya freemasons ndiyo dini iliyoanza siku nyingi kuliko dini nyingine.Dini hii ilianzishwa pia kwenye bustani ya Eden mwanzilishi wake akiwa ni Shetani. Alimtumia Kaini anayejulikana kwa freemasons wa leo kama ‘first freemason’ yaani mjenzi huru wa kwanza.

Hatimaye rais Constantine kwa nusu aliamua kuachana na ibada za kipagani na kujiunga na Ukristo. Hii ilikuwa ni kutimizwa kwa andiko la 2 Wathesalonike 2:3,4 maana ulikuwa ni ukengeufu wa kanisa la mitume sehemu ya kwanza uliopelekea kuanzishwa kwa dini iliyochanganya ukweli na uongo. Kwa nini dini hii ilisubiri hadi awamu ya nne ya serikali ya dunia? Pengine nizungumzie kidogo maana ya namba nne kama inavyotumiwa na Mungu. Namba nne sio namba maalumu kwa freemasons lakini ni muhimu sana kwa Mungu. Namba nne inamaanisha kukomaa kwa mavuno na kuvunwa. Tazama hapa: “Akawaambia ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi…..Maana nchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena(pili)suke, kisha(tatu),ngano pevu katika suke. Hata (nne)matunda yakiiva mara aupeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika” Marko 4:26 –kwenye mabano ni ufafanuzi wa mwandishi. Hizo ni hatua nne kufika kuvunwa kwa mbegu njema. Vipi habari ya mbegu mbaya? “Lakini kila mmoja hujaribiwa(kwanza)kwatamaa yake mwenyewe. Halafuile tamaa ikisha kuchukua mimba(pili), huzaa dhambi (tatu),na ile dhambi ikiisha kukomaa, huzaa mauti(nne)”Yakobo 1:14,15. Unaweza pia kujua ni kwa nini waisraeli walitumia miaka 40 (4x10) kutoka Misri hadi Kanaani; kwa nini Yesu, Musa walifunga kwa siku 40 (4x10). Kumbuka kwamba namba 10 kwa Mungu inawakilisha ‘ukamilifu wa Mungu’ na namba 7 inawakilisha ‘utimilifu wa Mungu’.Kuna tofauti kati ya ‘ukamilifu’ – ‘perfection’ na ‘utimilifu’ – ‘fulness’.Kitu kinaweza kuwa ‘timilifu’ lakini kisiwe ‘kamilifu’ lakini kitu hakiwezi kuwa ‘kamilifu’ bila ya kuwa ‘timilifu’. Kwa mfano mapigo 7 ni utimilifu wa ghabu ya Mungu lakini ukamilifu wa hukumu yake utafikiwa wakati Shetani, dhambi na wadhambi watakapoangamizwa motoni. Mungu alitoa amri 10 kwa wanadamu ikimaanisha kwamba amri hizo zinawakilisha tabia ya Mungu ambayo ni ‘kamilifu’. Lakini pia tunasoma “….Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima na ‘ukamilifu’ wa uzuri” kisha anaanza kutaja ni kwa namna gani alikuwa ‘mkamilifu’ wa uzuri akisema “1)Akiki, 2)Yakuti manjano, 3)Almasi, 4)zabarajadi, 5)shohamu, 6)Yaspi, 7)yakuti samawi, 8)zumaridi, 9)baharamani na 10)dhahabu. Lusifa alikuwa‘mkamilifu wa uzuri’ kutokana na kuvikwa aina 10 za madini ya thamani kubwa. Mungu ni‘mkamilifu’ kutokana na kuwa na tabia inayoelezewa kwenye amri 10katika Kutoka 20:4-17. Je wewe ni mkamilifu wa tabia kama ya Mungu kwa kuzitunza amri 10? Tafakari!

FREEMASONS NA FAMILIA 13 ZA ILUMINATI


NI chama cha Prieure de Sion (Priory de Sion) kilichoanzishwa na familia ya 11 ya Illuminati inayoitwa Freeman Illuminati bloodlines ndicho kilichosababisha kuanzishwa kwa ‘Uprotestant’ au ‘Upinzani’ ndani ya dini. Wakainuka mashujaa wengi waliopinga mafundisho machafu yaliyoingizwa ndani ya imani ya kweli ili kutetea neno la Mungu litawale tofauti na mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Miongoni mwa mashujaa walioinuka kupingana na mafundisho ya chama cha Prieure de Sion alikuwa Martin Luther. Kumbuka kwamba wapinzani ‘Protestants’hawa walikuwa wanapinga mafundisho wakiwa ndani ya mifumo ya dini zao. Hata hivyo hawakufanikiwa kuleta matokeo mazuri ya upinzani wao na hivyo wakaamua kutoka na kujitenga na dini wakiwa na baadhi ya mafundisho machafu waliyoyarithi kutoka kwenye mifumo potofu ya kidini. Wakiwa wamejitenga, sasa waliamua kufanya ‘matengenezo’ kwa lengo la kuondoa mafundisho machafu na kubaki na mafundisho safi kama ilivyoagizwa na Mungu. Hivyo jina lao wakaitwa‘Reformers’ au ‘Wanamatengenezo’ badala ya ‘Protestants’ au ‘wapinzani’.‘Waprotestants’ wa awali walijua maana ya kanisa na ndio maana hawakuona shida kujitenga na mifumo iliyokuwa inadhaniwa kuwa ndiyo kanisa.Lakini je, nani aliyeanzisha ‘Uprotestant’na ‘matengenezo’? Ellen White anasema: “Christ was a protestant...The Reformersdate back to Christ and the apostles. They came out and separated themselves from a religion of forms and ceremonies. Lutherand his followers did not invent the reformed religion. They simply accepted it as presented by Christ and the apostles." E.G. White, Review and Herald, vol. 2, 48, col. 2.Hapo anamaanisha kwamba ‘Kristo (Yesu) alikuwa ni Mprotestant….wanamatengenezo waliiga kutoka kwa Kristo na mitume. Walijitenga na dini ya desturi na sherehe. Luther na wafuasi wake hawakuanzisha dini ya matengenezo. Waliikubali kama ilivyoonyeshwa na Kristo na mitume’ [rejea: R&H, Vol. 2, 48, col.2].

Ni kwa namna gani Kristo alijitenga? E. White anaendelea kusema: “Pharisees and Sadducees were alike silenced. Jesus summoned His disciples, and prepared to leave the temple, not as one defeated and forced from the presence of his adversaries, but as one whose work was accomplished. He retired a victor from the contest”. {DA 620.2}

‘Mafarisayo na masadukayo walinyamazishwa. Yesu aliwakusanya wanafunzi wake, na akawaandaa kuliacha hekalu, sio kama aliyeshindwa na kulazimishwa kuondoka kwa maadui zake, bali kama ambaye kazi yake ilikuwa imekamilika. Alikuwa ni mshindi katika mashindano”. {DA 620.2}

Biblia inasema kwamba Yesu alijitahidi kupingana na mafarisayo na masadukayo akiwa ndani ya mfumo wa dini ya kiyahudi na sasa alikuwa amefikia mwisho wa upinzani wake na akaamua kujitenga moja kwa moja na mfumo wa dini hiyo ili awafundishe vizuri wanafunzi wake ambao walikuwa tayari kukubali mafundisho safi. E.G. White anasema:" Hitherto He had called the temple His Father's house; but now, as the Son of God should pass out from those walls, God's presence would be withdrawn forever from the temple built to His glory. Henceforth its ceremonies would be meaningless, its services a mockery. {DA 620.4}Hatimaye Yesu na wanafunzi wake walijitenga na hekalu lililokuwa mpendwa wao. Lakini kwa sababu viongozi wa hekalu walikataa kufuata mafundisho ya neno la Mungu peke yake, Mwana wa Mungu hakuona sababu ya kuendelea kubaki ndani ya hekalu ingawa “Alikuwa akiliita hekalu kuwa ni nyumba ya Baba yake; lakini sasa, kama Mwana wa Mungu ambavyo akipita kutoka katika kuta hizo, uwepo wa Mungu ungeondolewa milele usionekane ndani ya hekalu lililojengwa kwa utukufu Wake. Hivyo sherehe zilizofanyika ndani ya hekalu hazikuwa na maana, huduma zake zikawa dhihaka”. {DA 620.4}. Hivyo ndivyo alivyofanya Martin Luther na wafuasi wake.

Baada ya kifo cha Martin Luther, wafuasi wake waliendelea katika kufanya matengenezo. Hata hivyo kwa sababu freemasons hawakati tamaa, matengenezo yalikoma na kuanza kurudi nyuma taratibu ambapo leo hii wale wanaoitwa ‘Walutheri’ wameungana tena na mfumo ambao mwanzilishi wao, Martin Luther, aliuiita ‘mfumo mchafu’.

Wakati matengenezo yanaendelea, ulikuwa ni wakati wa kutimizwa kwa unabii wa siku 1260 sawa na miaka 1260 kama ilivyotabiriwa na nabii Yohana. Wakati huo kulianzishwa matengenezo mengi na kupelekea kuanzishwa kwa mifumo mingine ya makanisa. Baadhi ya makanisa yaliyoanzishwa yalikuwa haya:

Anglican: Lilianzishwa huko England na mfalme wa Uingereza ili kupinga kanisa la Roma. Kiongozi mkuu wa kanisa hilo ni Malkia wa Uingereza. Hata hivyo wachunguzi wa dini ya freemasons wanasema kwamba familia ya Malkia ni familia mojawapo kati ya familia 13 za waumini wa Freemasons.

Presbyterian: Mwanzilishi ni John Calvin mwaka 1509 – 1564 na John Knox 1505 – 1572. Kanisa hili lilijitenga na Roma likiwa na motto “Chunguza maandiko” maana liliona kwamba kanisa la Roma linakwenda kinyume na maandiko. Hata hivyo wafuasi wa John Calvin na John Knox wameshindwa kufikia malengo ya kuyachunguza maandiko na kufuata kile asemacho Mungu na badala yake wamekubali kurudi walikotoka!

MENNONITE: Lilizaliwa rasmi mwaka 1525 – 1530 na Conrad Grebel na wenzake akiwemo Zwingli Ulrich aliyetofautiana na Martin Luther juu ya somo la pasaka. Hawa walikataa ubatizo wa Roma wa kunyunyizia maji na jina jingine wanaitwa “Meno Knights” majina ambayo yanafanana na vikundi vya Freemason kama vile “The knights of Eulogia”(Skull and Bones), “The knights of Malta”. Ingawa lengo la Zwingli Ulrich lilikuwa zuri, baada ya kifo chake wafuasi wake walikubali kuingiliwa na freemasons na hivyo kushindwa kufikia lengo lililokusudiwa.

LUTHERAN: Mwanzilishi ni Martin Luther mwaka 1517. Alikuwa ni Mjerumani aliyesomea ukasisi wa kanisa la Roma na mwaka 1511 akapata Phd katika chuo kikuu cha Wattenberg. Alipingana na kanisa lake la Roma na kuandika sababu 95 zinazopinga mafundisho ya Roma ndipo akajitenga na Roma na hivyo wafuasi wake wakaendelea kutumia jina la Lutheran, yaani wafuasi wa Luther. Wafuasi wa Luther hawakuendelea mbele na sasa wamerudi kwenye makosa aliyokuwa akiyapinga Luther. Je, Lutheran wa leo wanafuata kweli nyayo za Martin Luther? Au wametekwa kwa matumizi ya njama ya “Following Gurus”yaani kufuata kila wasemacho viongozi? Tafakari!

Moravian: Mwanzilishi ni John Huss aliyezaliwa mwaka 1366 na kuchomwa moto na papa hadi kufa mwaka 1416 baada ya kulipinga kanisa la Roma. Wafuasi wake hadi leo wanaitwa kanisa la Moravian. Kwa bahati mbaya wafuasi wa John Huss hawakuendelea kufanya matengezo ili kusonga mbele zaidi ya Huss na kibaya zaidi ni kwamba wanarudi nyuma badala ya kusonga mbele. Leo Huss akifufuka atashangaa kuona jinsi wafuasi wake walivyoacha kanuni alizozianzisha. Je, wamoravian wa leo wako tayari kuchomwa moto kwa kutetea ukweli kama John Huss? Tafakari!

Baptist: Ni kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa Martin Luther ambao walijitenga na Lutheran mwaka 1600 huko Uholanzi na Uingereza baada ya kuona kwamba wafuasi wenzao wameacha kanuni alizoziweka Martin Luther. Hata hivyo kanisa la Baptist la leo haliendeleza jitihada za Luther na sasa badala ya kusonga mbele linapiga ‘marktime’ likiwa limegeuka nyuma.

Salvation Army (Jeshi la Wokovu): Mwanzilishi ni Booth mwaka 1878. Kanisa hili lilianzishwa na wafuasi wa freemasons kwa lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Kumbuka kwamba Shetani hutumia fursa inayotolewa na Mungu akiwa na lengo la kuwafanya watu washindwe kujua kipi ni cha kweli na kipi sio. Katika kila matengenezo ya kweli, pamekuwepo na matengenezo bandia.

Marmon church: Mwanzilishi ni Joseph Smith (1805 – 1844). Kanisa hili linajulikana pia kama The church of Jesus Christ of later day saints. Kanisa la Mormon lilianzishwa na wafuasi wa freemason wakiwa na lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Mitt Romney ni muumini wa kanisa la Mormon.

Methodist: Kiongozi Mwanzilishi ni John Wesley. Lilianzishwa na watu 17 wa familia moja mwaka 1738 likiwa na lengo la kupinga mafundisho ya freemasons. Kanisa hilo halijakamilisha lengo la matengenezo kutokana na ukweli kwamba wafuasi wake hawana mwamko aliokuwa nao John Wesley.

Watch Tower: Mwanzilishi ni Charles T. Russel 1852 – 1916 na mwenzake J. Lutheford 1869 – 1942. Baba yake Charles T. Russel alikuwa ni mchungaji wa Prebyterian. Mnamo mwaka 1932 huko Marekani jina la kanisa hilo lilibadilishwa na kuitwa Mashahidi wa Yehova. Markus Mpangala ameelezea kwa kirefu chanzo cha dhehebu hili akiainisha kwamba waanzilishi walikuwa ni Freemasons kutoka kwenye familia ya Illuminati inayoitwa Russel illuminati bloodline ambayo nimeshaielezea kwenye makala zilizopita.

Brethen Assemblies: Mwanzilishi ni ndg. Dabi 1800 – 1882 ambaye alikuwa ni muumini wa Anglican na akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake. Dabi aliamua kujitenga na Anglican kutokana na kanisa hilo kutawaliwa na familia ya freemasons.

Makanisa ya Kipentekoste au kilokole: Ni makanisa yaliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni. Makanisa haya yalianzishwa huko Kansas City Marekani mwaka 1901kwa lengo la kupata nguvu ya kile kinachoaminiwa kuwa roho mtakatifu. Je, unajua uhusiano uliopo kati ya muziki wa‘rap’ au ‘kufoka’ na uvuvio wa kunena kwa lugha kutoka kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni nguvu za roho mtakatifu wakati waumini wa kilokole wanapokuwa wakiomba? Kumbuka kwamba Muziki wa rap ulianzia huko Kansas City Marekani, mahali ambako makanisa ya kipentekoste yalianzishwa. Panapo majaaliwa, nitakuwa na makala ndefu kuhusu asili, lengo na nguvu inayoonekana kwa viongozi wa makanisa ya kilokole kama akina T.B Joshua wa SCOAN la huko Nigeria. Kwa wakati huu nasema,‘Soma Biblia na Tafakari’!

Gospel terbenacle: Mwanzilishi ni Pastor A.B. Simpson mwaka 1881 akitokea Presybiterian.

Christian Churches: Mwanzilishi ni Thomas Chapel mwaka 1807 akitokea Presybiterian.

Seventh –Day Advetist Church: Mwaka 1844 baada ya kutokurejea kwa Yesu duniani kama ilivyohubiriwa na muhubiri mashuhuri aitwaye William Miller, watu wengi walivunjika moyo isipokuwa watu 50 tu ndio walioendelea kujifunza Biblia miongoni mwao akiwa ni Ellen G. White. Watu hao waliendelea kuchunguza makosa yaliyofanywa na William Miller maana wao pia waliamini juu ya marejeo ya Yesu tarehe 22/10/1844. Hatimaye mwaka 1863 kanisa hilo likapewa jina la Seventh –Day Adventists Church huku likiwa na motto au kauli mbiu ya “Amri za Mungu na imani ya Yesu na Ujumbe wa malaika watatu” na baadaye kanisa hilo likawa chini ya rais wa General Conference ya SDA makao makuu yake yakiwa huko Marekani. Rais huyo ndiye kiongozi (kichwa) mkuu wa kanisa hilo duniani na huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wakati viongozi wa kanisa walipokutana ili kujadili mambo ya kanisa, palikuwa na ‘Mwenyekiti’(Chairman of General Conference) ambaye aliongoza kikao hadi mwisho. Baada ya kikao kumalizika, mwenyekiti huyo alimaliza muda na kazi yake. Hata hivyo kulitokea mabadiliko kutoka mwenyekiti wa baraza kuu hadi na rais wa kanisa ulimwenguni. Kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kumpata rais wa kanisa hilo. Tofauti na makanisa mengine, kanisa hili linaabudu siku ya Jumamosi wakati makanisa mengine yanaabudu siku ya jumapili. Sasa hivi kuna makanisa mengi ya SDA ambayo yametoka ndani ya kanisa la ‘General conference of Seventh-Day Adventists’(GCSDA) kwa madai kwamba kanisa hilo limeingiliwa na freemasons. Wengi wa waumini wa SDA waliojitenga na GCSDA wanasema kwamba walikuwa wakipinga‘protest’ mafundisho machafu huku wakiendelea kuwa ndani ya GCSDA lakini hawakuweza kuleta mabadiliko yoyote maana hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya. Hatimaye waumini hao waliamua kufuata nyayo za akina Luther za kujitenga na sasa wanafanya ‘reformation’ au ‘matengenezo’ hatua kwa hatua maana walitoka na mafundisho machafu ambayo waliyapokea kama kweli wakiwa ndani ya GCSDA.Waumini hao wanadai kwamba walijitenga na GCSDA kwa sababu


Je, madai hayo ni kweli? Tafakari!

Msingi wa kanisa la SDA au ‘Wasabato’ kama inavyojulikana kwa wengi,kuabudu siku ya jumamosi, ni kile kilichoandikwa na Mungu wakati wa uumbaji, kwamba aliumba kwa siku 6 na siku ya 7 akastarehe, akaibariki na akapumzika kisha akawaambia waisraeli: “Ikumbuke siku ya Sabatouitakase….” Kutoka 20:8.

Kutokana na kazi ya chama cha Priory de Sion kwa kuingiza mafundisho machafu ndani ya imani safi, kulitokea utitiri wa makanisa mengi ambayo yanadai kupinga uchafu huo. Hata hivyo wengi wa waumini wa madhehebu hayo ama hawajui asili ya dhehebu lao au hawajui asili ya kile wanachokiabudu. Wengi wamefundishwa na waalimu wa dini na kuwaamini bila hata ya kutaka kuhakikisha kwa akili zao kile wanachofundhishwa. Mungu ametoa nafasi ya kufahamu ukweli kwa kila mmoja wetu bila ya kutegemea viongozi wa dini. Umewahi kufikiri kwamba kama ungekuwa unaishi duniani wewe peke yako, ungemtegemea nani? Tafakari!



UJUE UNDANI WA FREEMASON
HISTORIA KWA UFUPI


Freemason ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.


Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.

Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.


1. Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).


Niliambiwa walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs).


Niliambiwa wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.


2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k


3. Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.


3. Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani. Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki.


Ndio maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama Jesuits.


Jesuit Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa katoliki.


4.Kuhusu imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu na Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila Lucifer aonekane mbaya.


4.Kinachoendelea ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja ambazo muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu kabisa ni nyuzi ya 33 (33rd degree)


5. Kwa hiyo ijapokuwa wanatumia biblia wanapoongelea “Bwana” huwa hawamaanishi Yesu bali huwa wanamaanisha Lucifer ambaye ndiye wanayemwabudu.


6. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi.


Wafuasi wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.


7. Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri, yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya utawala.


WALIOSHIRIKI KUPINGA FREEMASON NA UASI WA
LIONS CLUB NA ROTERY CLUB

Kanisa la Katholiki wakati moja waliwahusisha Rotarians (Lions Club) moja kwa moja na Freemasons. Mwaka wa 1928 Maaskofu wa kihispania walitangaza wazi kwamba Rotary Club si chama tu cha kawaida bali ni Muungano au chama kipya cha kuabudu mashetani wakiwa na katiba, tabia na kila kitu chao kufanana na zile za Freemasons wakawatahadharisha waumini wao wajichunge sana na Chama hicho, na baada ya muda mfupi wakuu wa Vatican walitoa amri kwamba maaskofu wa kanisa la katoliki hawaruhusiwi kujiunga na vyama hivyo (Rotary, Lions Club).


Mohammed Sayed Tantawi

Katika miaka ya 1970 kiongozi wa juu na Sheikh wa Chuo kikuu cha kiisilamu huko Misri (Egypt) inasemekana alitoa fatwa kuwakataza waisilamu wasijiunge na chama cha Rotary Club na wakati mambo haya yalikua yakikatazwa na dhehebu la sunni Chama cha rotary pia kilisikika kukatazwa na Ayatollah Khomeini.


Ayatollah Khomeini

katika mwaka wa 1798 Mwandishi Mmoja wa Kiingereza aliejulikana kwa jina la john Robbinson aliandika kitabu kijulikanacho kama Proofs of a Conspiracy Against All the Religions and Governments of Europe, Carried On in the Secret Meetings of Free Masons, Illuminati, and Reading Societies (Uthibitisho wa njama dhidi ya Dini zote na Serikali zote za Ulaya ilipangwa katika mikutano ya siri ya Freemasons, Illuminati, na vyama vinginevyo vya Reading)

John Robbinson


Kitabu hicho kinaelezea Ari na hamasa za Freemason walivyokuwa wakipanga kisiri jinsi ya kupinduwa mipangilio mizuri ya Maisha (Serikali) na ndio waliosababisha mapinduzi nchini Marekani na Ufaransa.


Shuku za kuenea kwa Freemasons zilienea hadi kufikia miaka ya 1800 ambapo

Rais Wa 13 Millard Fillmore wa Marekani
alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la Marekani (Congress) kama mgombea aliyekuwa akipinga mambo ya Freemasons na akafikia kilele katika karne ya 20 (20th Century)


Sergiei Nilus Mwandishi Kitabu cha Protocol

Kitabu cha The Protocols of the Elders of Zion sio kuhusu mayahudi kutawala dunia lakini ni kuhusu njama za freemason wa kiyahudi kubadili mfumo wa dunia.


Hitler Reinhard Heydrich
Hitler alizungumzia kuhusu njama za Mayahudi-Bolshevik-Freemason na kiongozi mwingine wa Ujerumani kwa jina la Reinhard Heydrich aliunda kikosi maalum (Special Section SS) kuangamiza ushawishi wa freemason nchini Ujerumani.


Moqtada al-Sadr Al Hawza

Nchini Irak, Gazeti la Moqtada al-Sadr lijulikanalo kama Al Hawza lilichapisha picha ya George H.W. Bush na Bill Clinton na akaelezea kwamba ishara ya mikono yao ilikuwa ni alama ya waandamizi wa kizayoni na freemason, na kama walivyo Wakatoliki Waisilamu pia waliwahusisha wanchama wa Rotary moja kwa moja na Freemasons na kusema vyama vyote viwili ni laana.


Rais Bush Rais Clinton

Freemasons wamehusika moja kwa moja katika jitihada za kutawala Mashariki ya kati jitahada ambazo zilibuni uhasama kati ya Mashariki ya Kati na Jumuiya ya Magharibi.

Freemason walitoa fursa ya wafanyabiashara kuunda mtandao mmoja, hii ni katika malengo ya wafanyabiashara wanachama wa Freemason wa Ulaya wafungue ofisi za Freemason nje ya nchi na kuwaalika wanainchi wa Ulaya kujiunga nao.


Kwa ujumla sio Wafanya biashara wa Wakiingereza au Mashariki ya kati ndio waliowengi tu kama anavyoeleza bwana Hamid Algar wa Berkeley ambaye ni Mwanachuoni maarufu duniani wa historia ya Kiisilamu:-


Hamid Algar
Freemason imeweza kuhudumika katika uisilamu tangu kijitambulisha kwa waisilamu katika karne ya 18 kama njia ya kukuza utawala wa fikra za wa Magharibi kisiasa na kimawazo; Mojawapo wa Ofisi za Freemason huko Istambul nchini Uturuki, ilikuwa na Balozi wa Uingereza kama mkuu

WANACHAMA WA FREEMASONS NCHINI TANZANIA







Sir Andy Chande akiwa na wenzake wakipanda Miti jijini Tanga kama moja ya shughuli zao za kijamii

Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa kada mbalimbali wakiwemo maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni mwao hakuna viongozi wakuu wa serikali.
Hayo yalibainishwa na Kiongozi wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande.
Kiongozi huyo Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema licha ya Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama duniani inapungua tofauti na inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka kutokana na kuibuka maneno mengi kuhusu kundi hilo.
Alisisitiza kuwa si rahisi kumjua mwanachama wa kundi hilo, bali wenyewe ndio wanaofahamiana, akisema ni siri na kwamba wenyewe wanakutana katika vikao mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.
Alisema nchini kuna wanachama zaidi ya 600 wakiwemo wafanyabiashara, watumishi serikalini, walimu pamoja na wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana na kusisitiza kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo, ambayo siyo ya kweli.
Alisema idadi ya wanachama wake duniani inazidi kupungua kutoka milioni nane hadi sasa wako milioni sita, tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo inaongezeka.
Chande alizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema duniani kuna watu wazito wengi ambao ni wanachama wa kundi hilo kama majaji wakubwa na hata Binamu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ni kiongozi mkubwa wa kundi hilo.
Akizungumzia masharti ya kujiunga na kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama huyo awe anaamini katika Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au Muislamu.
Alisema pia ni lazima anayetaka kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio chini ya umri huo hawaruhusiwi kujiunga na lazima familia ya anayetaka kujiunga na wanandugu wafahamu kuwa umejiunga na kundi hilo.
“Unajua katika imani hii kuna michango mbalimbali ambayo unatakiwa kutoa ambayo ni zaidi ya dola milioni sita (karibu Sh bilioni 10), hivyo ni lazima ndugu wafahamu ili kuepuka matatizo utakapotakiwa kutoa,” alisisitiza.
Alisema si kweli kuwa wenye fedha wengi ni wanachama wa kundi hilo huku akikanusha wanachama wanajiunga kwa ajili ya kupata fedha, bali ni dini kama imani nyingine.
Alisisitiza kuwa hakuna ukweli kwamba wanaopata mafanikio katika maisha wakiwa ndani ya imani ya Freemasons kuwa wanatoa kafara watu wao wa karibu kwa lengo la kupata utajiri.
Chande pia alisema hairuhusiwi kutumia jina la kundi hilo kwa nia ya kujipatia nafasi sehemu mbalimbali au kuongeza nafasi katika chuo au shule.