Monday, November 26, 2012

MATUKIO NA PICHA

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKOA MPYA WA KATAVI LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa Katavi PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM.
Makamuwa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said.
Mkuu wa mkoa wa Katavi akimkaribisha Makamu wa Rais Dt. Gharib Bilal ili kuongea na wananchi wa kijiji cha Kabungu.Msafara wa magari ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal ukiwasili katika eneo lilipowekwa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa mkoa wa Katavi katika kilima cha kijiji cha Kabungu Mkoani Katavi.
Wazee waasisi wa kijiji cha Kabungu wakinyanyua matawi ya miti juu kama ishara ya kumpokea Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati alipowasili katika kijiji hicho leo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa mkoa wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili kulia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt. Mary Nagu.
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya wakiwa katika sherehe za uzinduzi huo.
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili.
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
Mama Aisha Bilal akisalimia wananchi wa katavi katika sherehe hizo.
Kwaya ya Vijana ya Moravian mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.
Martha Mbogo mwimbaji wa kundi la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika uzinduzi huo mjini Mpanda.
Wananchi wa Mpandawakinyanyua mkono yao juu kama ishara ya kushangilia kuazinduliwa kwa mkoa wao wa Katavi uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
Wananchi wakiwa wanashangilia
Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Veta Chuo cha Veta Mpanda Trojemsi Bashato wakati alipotembelea banda la Veta.
Makamu wa Rais akisikiliza maelezo kutoka kwa Thomas Lemunge mfanyakazi wa kampuni ya simu ya TTCL wakati alipotembelea Banda la kampuni hiyo, kulia ni Bw Huphrey Ngowi mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa huduma Mwandamizi wa benki ya Wanawake TWB BiMargaret Msengi wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
Makamu wa Rais Akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea katika banda hilo leo njini Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.

SHILINGI BILIONI 86 ZAIBWA WIZARA YA NISHATI/TANESCO, GRIDI YA TAIFA HATARINI

Na Zitto Kabwe
Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.
Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).
Katika mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1.      Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.
2.      Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama. Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86 za kununua mafuta ya IPTL.
3.      Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya fedha kwa Serikali.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha
Dar es Salaam. Novemba 25, 2012
1

"ASANTENI WASAMALIA… KWA MSAADA WENU"

Na Devota Mwachang’a
 
Hatimaye Beatrice Shimende Kantimbo (48) pichani amefanikiwa kusafiri kwenda nchini  India kutibiwa mguu katika hospitali ya Apollo, kutokana na michango ya wasamalia wema pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Beatrice, aliyeambatana na Mumewe Emmanuel Kantimbo aliwashukuru sana wale wote walioguswa mara baada ya kupata taarifa zake, na kuamua kumsaidia kwa pesa, ushauri na kwa sala, pia vyombo vya habari.
Beatrice amesumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, vipimo vya kitabibu vimegundua kuwa ni ugonjwa wa matende (elephantiasis).
Mwanamke huyu alikuwa ni 'mchakarikaji' kweli,  aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa wa ikiwemo biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele pia  aliyekuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC) kwenye sherehe akifahamika kama MC Kimbaumbau,
Hapa alisimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana wala hapakuwa na alama yoyote.
"Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na malaria.
"Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha. Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali. Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba. Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"
Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka kuvimba na maumivu makali yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza.
Anasema: "Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali kukatwa mguu. Wanasema ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007 iligunduliwa tatizo kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.
"Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.

JUMAPILI NJEMA: AIC CHANG'OMBE - JINSI ZILIVYO

WAISLAM WA DHEHEBU LA SHIA JIJINI DAR WAADHIMISHA SIKU YA ASHURA KUKUMBUKA KIFO CHA MJUKUU WA MTUME MOHAMMED (S.A.W)

Pichani Juu na Chini Waumini wa dhehebu la Shia wakiwasili na kukusanyika katika eneo la makaburi ya Washia Kisutu jijini Dar es Salaam wakijiandaa kuanza maandamano ya kuadhimisha siku ya Ashura kukumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) Imam Hussein yaliyofanyika jana.

Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamaat Shia Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa waandishi wa habari amesema katika kuadhimisha siku hii Waislam wa dhehebu la Shia watafanya matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo ndani yake kutakuwa kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za maombolezo tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi kujipa uhai kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa watu wake na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya wenzake.
Imamu wa Msikiti wa Imam Ali wa Magomeni Mapipa Msabaha Shaaban Ali Mapinga akizungumza na waandishi wa habari amesema siku hii ni siku ya kukumbuka na kuadhimisha miaka 1473 ambapo katika nchi ya Iraq kwenye mji wa Karbala aliuwawa mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) aliyekuwa akijulikana kwa jina la Imam Hussein Bin Ali Bin Abutwalib.
Amesema katika nyakati hizo alitokea mtawala dhalim aliyekuwa akitetea dhulma na kukiuka haki za binadamu kitendo ambacho mjukuu wa Mtume Imam Hussein hakukubaliana nacho na kuunda jeshi lake dogo kutetea haki na kupinga Batili.
Kwakuwa Imam Hussein alikuwa na dhamana ya kutetea haki alikataa kuwa chini ya mtawala huo ndipo alipotumiwa jeshi la watu kama 30,000 naye akiwa na jeshi la watu 72 walipambana katika mji huo na mjukuu wa Mtume aliuwawa kifo cha kikatili cha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi.
Amesema kifo cha Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo haki ilizimwa na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka batil isimame , kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.
Aidha Sheikh Salum amesema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo, kutetea wanyonge, kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna yoyote ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.
Waumini hao wakiwa wamejipanga tayari kuanza maadamano kutoka makaburi ya Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia.
Pichani juu na chini msafara wa waumini wa Shia umeanza.




Hisia na Majonzi vilionekana.
Ni jambo jema watoto kujua dini mapema, kama inavyoonekana pichani mtoto akiwa ameambatana na mzazi wake katika maandamano ya siku ya Ashura.
Bango lenye Ujumbe maalum wa siku ya Ashura.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA MKOA MPYA WA KATAVI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwanja huo iliyofanyika mkoa Mpya wa Katavi, leo Nov 24, 2012 katika uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 30. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Miundombinu, Omar Chombo na  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.Charles Tizeba. Picha na OMR

ONYESHO LA KHANGA ZA KALE 2012 LILIVYOFANA JIJINI DAR

Mgeni Rasmi katika Onyesho la Khanga za Kale, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jisnia na Watoto Mheshimiwa Sophia Simba akisoma hotuba yake fupi wakati wa kufungua rasmi Onyesho la Mavazi ya Khanga za Kale 2012 linaloratibiwa na Mamaa wa Mitindo Asia Idarous Khamsin (kushoto) chini ya Kampuni yake ya Fabak Fashion. Onyesho hilo lilifanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa Onyesho la Mavazi ya Khanga za Kale 2012, Mamaa wa Mitindo Asia Idarous Khamsin akizungumza machache kabla ya kuanza Rasmi kwa Onyesho katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
Kiki fashions nao hawakukosa.
 Mwanamitindo Martine Kadinda nae hakuwa nyuma kuonyesha vazi lake alilobuni.
Wanahabari nao hawakuwa nyuma kupata matukio.
Meza kuu wakishangilia.
 Wageni wakifuatilia.
 Vimwana wa Unique Modoz nao walikuwepo.
Wageni waalikwa wakiteta.  
Mbunifu wa mavazi Gabliel Mollel akipita jukwaani na vazi alilobuni.
Mbunifu wa Mavazi Gymkhana Hilali anayemiliki Paka Wear akipita na vazi lake.
Mama wa Mitindo House Khadija Mwanamboka nae hakukosa.
 Mshiriki wa shindano la EBBS 2012, Salma akitoa burudani.
Moja ya picha iliyofanyiwa mnada.
 Muandaaji wa Onyesho la Mavazi ya Khanga za Kale 2012, Mamaa wa Mitindo Asia Idarous Khamsin akiwa na mumewe mzee Khamsin wakiwapungua wageni waliohudhuria. Mavazi hayo yanayofuata katika picha za chini yamebuniwa yeye.
 Mmiliki wa Blog hii, Cathbert Angelo Kajuna nae alipata nafasi ya kupanda jukwani akiwa amevaa vazi la shati ya khanga aliyobuniwa na mama Asia Idarous Khamsin.
 Pozi kidogo...
 Mmilikiwa wa Blog ya Missie Popular, Bi. Mariam Ndaba nae alipita na vazi lilibuniwa na mama wa Mitindo Asia Idarours Khamsin.
  Mmilikiwa wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, Othman Michuzi nae hakuwa nyuma kuvaa vazi lilibuniwa na mama wa Mitindo Asia Idarours Khamsin.
 
 Matukio Chuma nae hakuwa nyuma.
Sarah mke wa Raqey Mohammed mmiliki wa I-View Media nae alipata nafasi.
 Taji Liundi hakukosa.
 Baby Madaha...
 Magesa mwendeshaji wa shindano la Unique Modo nae alikuwepo.
 Wageni wakishangilia.
Modoz wakipita kwa steji, wakiongozwa na Mtangazaji wa Star Tv, Sauda Mwilima (kwanza Kulia), Mmiliki wa Mtaa kwa Mtaa Blog, Othman Michuzi (kati) na Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo (kwanza kushoto).

No comments: