Monday, November 26, 2012
Msiba Luton Uingereza
It
is with great sadness that the family of Maria Goreth Ndangio announce
her passing away in the early hours of 25/11/12 at the Keech Hospice,
Luton. Details of meetings venue will be advised shortly to facilitate
funeral arrangements. Maria's family sincerely thank each and everyone
for their visitations, kind words and continued support to the very end.
Let us continue to uphold her family especially her little son Derek in
prayer.
2 Timothy 4:7 I have fought the good fight, I have finished the race, I
have kept the faith
RIP Maria sadly missed, fondly remembered.
Eternal rest give to them,O Lord,
and let perpetual light shine upon them.May they rest in peace.
May their souls,and the souls of all the faithful departed,
through the mercy of God,rest in peace.Amen
As we are planning to transport the body back to Tanzania for
funeral,We ask all good people to help the family at this difficult
time.
You can contribute through ; Elly Njau Benichou. Bank;Loyds TSB Acc;77164860 SC;77 49 01 For more details contact: Daniel 07445318792 Elly 07908213431
You can contribute through ; Elly Njau Benichou. Bank;Loyds TSB Acc;77164860 SC;77 49 01 For more details contact: Daniel 07445318792 Elly 07908213431
Dkt.Bilal Azindua Mkoa Wa Katavi
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa
wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa
kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya
kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha
Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la
mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji
wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda
katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali
za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na
sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa Katavi
Makamuwa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza
Na Fullshangweblog
Makamuwa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza
Na Fullshangweblog
Tabia, Mienendo Na Mawazo Yetu Ni Adui Zetu Wakubwa(1)
Na:
Meshack Maganga-Iringa.
Katika
makala yangu ya wiki iliyopita ya ‘Uwezo Wa Kujua Kama Tutakufa Maskini Tunao’,
nilizungumzia kwa kirefu uwezo wa binadamu hasa katika mawazo yake ya kina. Baadhi
ya wasomaji walitoa maoni yao kwa barua pepe, na wengine walitoa maoni yao
kwenye ukurasa wa maoni wa MjengwaBlog. Napenda kuwashukuru walionishauri, na
maoni yao ndiyo yaliyo pelekea kuzaa mada ya leo ambayo ni ya wiki hii.
Aidha,wiki
iliyopita pamoja na mambo mengine, nilibahatika kusoma vitabu na makala
mbalimbali,moja ya makala niliyoisoma ni ile ya mwandishi maarufu Jack Canfield
aliye andika kitabu kinacho tamba
duniani katika ‘sheria ya mvuto’ (The law of attraction) kiitwacho ‘The Success
Principles’. Kwenye moja ya makala yake Jack Canfield anasema, watu wote wenye mafanikio duniani,
ambao huonekana kana kwamba wamebarikiwa hutafuta maana ya wao kuwa wao, uwezo
wao wa kipekee na kutumia upekee walionao na kuishi maisha yao kimafanikio
watakavyo wao. Dunia hii inayo nafasi kwa mwanadamu ambaye anatafuta maana ya
maisha yake mwenyewe, haijalishi umezaliwa katika familia ya aina gani bali
ukikubali ukweli kuwa unayo hazina ya maisha ndani yako basi maisha yako
yatapata maana.
Katika makala hii ya
leo,nitazungumzia juu ya tabia zetu na maamuzi yetu mabalimbali ambayo hutuletea
taaifa ‘feedback’ ambazo wengi wetu huziita mikosi au bahati mbaya.
Mbu anapokuuma nakupata
malaria huwa unamhesabu kama adui yako.? Zipo Ngo na kampeni mbalimbali za kitaifa
na kimataifa ambazo zipo kwenye kampeni ya kupambana na malaria. Lakini je, ni kweli mbu ndiye adui yetu?
Siku hizi kuna virusi va HIV
ambavyo vinahesabiwa kama maadui wa watu wote. Kila kona hapa duniani kuna
juhudi za kila aina katika kupambana na virusi hivi.
Ukimuuliza mtu atakwambia,
virusi hawa ndiyo adui zetu katika suala la maradhi haya, lakini je, kuna
ukweli wowote katika hili? Kila mtu anafahamu vizuri mazingira ya aina
mbalimbali ambayo kwake huyaita adui, kila mtu anawafahamu watu wa aina mbalimbali
ambao kwake kwa sababu mbalimbali anawaita adui zake na kila mtu anafahamu
vizuri vitu Fulani maalum ambavyo kwa sababu Fulani anaviita na kuamini kwamba
ni adui zake.
Lakini huenda hakuna ambaye
anajua ni kwa kiasi gani tabia, mienendo na mawazo yake ni adui zake wakubwa.
Ni mara chache sana na ni watu wachache sana ambao wako tayari kujiuliza na
kukiri kwamba, tabia mienendo na mawazo yao kwa kiasi kikubwa sana huenda
vinawadhuru na kuwaumiza, kuwaharibia mipango yao na maisha kwa ujumla, kuliko
wanvyodhani kwamba athari hizo hutoka nje yao.
Ni wachache kwa sababu,
binadamu hujipenda sana kiasi ambacho huogopa kufunua macho zaidi na kuukabili
udhaifu alionao. Ukweli ni kwamba, kama mtu atataka kuishi bila kujidanganya,
atagundua kuwa hata mbu na virusi vya ukimwi siyo adui zetu. Atagundua kwamba,
tabia mienendo na mawazo yetu ndiyo adui zetu.
Kama mtu ataamua kujikinga dhidi
ya mambo yote yanayoweza kumwambukiza virusi vya ukimwi au kuishi katika
mazingira ya mbu wengi na kuchukua
tahadhari dhidi ya wadudu hao, anakuwa amemkwepa kwa karibu asilimia
tisini huyu au hawa anaowaita adui zake.
Kila siku, hata pale ambapo
tunatangaza kwamba akina Fulani na
Fulani ni adui zetu, huwa tunafanya hivyo kwa makosa kwa sababu tu ya kujipenda
na hivyo kujipendelea katika kuutazama ukweli. Tunapofilisika tunajitahidi sana
kutafuta maadui wa hali hiyo, huku tukiwa tumesahau kwamba tabia zetu ndizo zilizotufilisi.
Kwenye
kitabu
chake cha ‘Kichwa chako ni Dhahabu’, Geoffrey Tenganamba anasema kuwa,
Janga kubwa duniani si kifo wala ajali, Bali Ni maisha ya
mwanadamu aliyekubali kuishi maisha ya bora liende, asiyetaka kubadilika
Na
kukua, anayeishi leo kama jana na atakayeishi kesho kama leo.
Tunaposhindwa kupata
tunachokitafuta maishani, hatuzitazami tabia, mitazamo, mienendo, imani na
mawazo yetu, bali tunatazama nje yetu ili kumpata adui. Ilivyo ni kwamba, kama
tunamtafuta adui, kwa sababu tunataka kumpata ni Lazima tutampata. Hivyo
tukishampata tutaamini kabisa kwamba huyu ni adui yetu na kuziweka nguvu zetu hapo
kujaribu kupambana naye.
Inachukua muda, na wakati
huo tunakuwa tumechelewa sana tunapokuja kugundua kwamba tuliyemdhani ni adui
alikuwa ndani mwetu. Lakini kwa bahati mbaya sana ni kwamba huwa hatufanikiwi
kung’amua kwamba huyu tunayedhani ni adui yetu siyo adui yetu. Kwa hali hiyo,
huwa tunaishi katika dhiki, misukosuko na nuksi zisizokwisha tukijaribu
kupambana na adui ambaye siyo, huku adui yetu akiwa ni sisi wenyewe.
Kupigana
huku na adui asiyekuwepo popote bali ndani mwetu huweza hata kutupotezea maisha
yetu.
Kwa nini basi kabla
hatujatangaza au kudhani Fulani ndiye adui yetu, tusitazame au kuzikagua kwamba
tabia zetu, mienendo, imani na mawazo yetu? Wanasema wataalamu wa Nyanja zote
za kimaisha katika nadharia zao nyingi kuhusu maisha kwamba, adui wa mtu ni mtu mwenyewe.
Eckhart Tolle, katika kitabu
chake cha ‘The Power Of Now’ anasema
kuwa, watu wengi hawabadiliki kwasababu wamefungwa, na ni watumwa wa mifumo ya
zamani, yenye akili ileile, kanuni zilezile, mawazo yaleyale, tamaduni
zilezile, vipato vilevile na vipimo vilevile.watu wa aina hii wanatembea lakini
hawaishi.
‘Sikiliza zauti za dunia lakini sikiliza sana sauti yako ya ndani kwani’...ITAENDELEA.
Michoro Ya Kampasi Ya Muhimbili Itakayojengwa Mloganzila Kisarawe
Michoro
ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila iliyo kijijini Kwembe katikati ya
Wilaya za Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam. Hii
ni sehemu ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) inayojengwa kwenye eneo la ekari 3800 kwa ajili ya kutolea
mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya wapatao 15,000 kwa
mwaka, na pia itakua sehemu ya kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na
ya kawaida nchini.
Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili, ujenzi wa Hospitali hii, ambayo pesa ya ujenzi wake
imeshapatikana, unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na
unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi kuanza. Kwa maneno
mengine Kampasi ya Muhimbili ya Mloganzila inategemewa kuanza kazi
mwanzoni mwa mwaka 2015.
Tayari wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika
kampasi ya Mloganzila wameshaanza mafunzo ndani na nje ya nchi. Mara
hospitali hiyo kubwa na ya kisasa itakapokamilika itakua na uwezo wa
vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita (600).
Sambamba na kampasi ya MUHAS ya Mloganzila pia ujenzi wa Kampasi ya Afya
ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umeshaanza na kufikia hatua ya juu na
ambapo pia hospitali hiyo inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka
2015.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health
Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba mchakato wa kufanikisha
uanzishaji wa Chuo Hospitali hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu
wakiwemo Madaktari na watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa
ajili ya masomo na mafunzo mbalimbali.
Chuo hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi
mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa, ikiwa ni
mikakati kabambe ya serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha nchi
ina wataalamu wengi na huduma za kisasa za afya ili kuondokana na adha
ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Kwa sasa MUHAS inachukua takriban wanafunzi 2442 wa udaktari na huduma
za afya kwa mwaka. Hivyo ujio wa kampasi ya Afya Mloganzila na Kampasi
ya afya ya UDOM utaharakisha mpango wa serikali wa kupunguza wastani
wa wagonjwa kwa daktari mmoja kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa wastani ni
daktari mmoja anahudumia wagonjwa 30,000.
Na Michuzi
Na Michuzi
Ugeni Kutoka Sweden Umeingia Iringa!
Madam
Lisa, Mkuu wa Idara ya Miradi kwa Tanzania kutoka Shirika La Misaada Ya
Kimaendeleo La Forum Syd la nchini Sweden. Ameingia Iringa jioni hii.
Atakuwa na ziara ya siku mbili kufuatilia miradi ya maendeleo ambayo
Shirika lake linafadhili. Jioni ya leo tulimkaribisha nyumbani kwa
chakula cha jioni.
Sunday, November 25, 2012
Anne Makinda Ashiriki Msiba Wa Mzee Rajani.
Spika wa
Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza waombolezaji kuweka maua katika mwili
wa Mzee Jayantlal Rajani ikiwa ni ishara ya kutoa heshima za mwisho kwa
marehemu wakati wa kuaga mwili wa marehemu Mzee Rajani nyumbani kwake
upanga jijini Dar es salaam leo.
Spika wa
Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee
Philip Mangula wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa mzee Rajani
.
(Picha na Owen Mwandumbya).
Jukwaa la Katiba Lamwaga Katiba Mkutano wa Jinsia Morogoro
Na: Mwandishi wa Thehabari.com Morogoro
TAASISI ya Jukwaa la Katiba Tanzania imelazimika
kugawa nakala ya Katiba ya Tanzania kwa washiriki wa Mkutano wa Jinsia
Ngazi ya Wilaya uliofanyika nje kidogo ya Mkoa wa Morogoro kabla ya
kuanza kuelezea umuhimu wa Tanzania kuingia katika mchakato wa kuundwa
kwa Katiba Mpya unaoendelea hivi sasa.
Tukio hilo lilitokea juzi Kijijini Mkambarani ulipokuwa ukifanyika
Mkutano wa Jinsia ngazi ya Wilaya ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP), ambapo Jukwaa la Katiba lilialikwa kutoa mada juu ya
umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Katiba mpya.
Idadi kubwa ya wananchi kutoka vijiji mbalimbali walisema hawajawahi
iona Katiba hivyo, hivyo Mratibu wa Jukwaa la Katiba, Bi. Diana Kidala
kulazimika kutoa nakala ya Katiba kwa wananchi wote kabla ya kuanza mada
yake.
Bi. Kidala aliwataka wananchi hao kushiriki kikamilifu katika kutoa
maoni juu ya uundwaji Katiba Mpya ili katiba itakayopatikana iweze
kuleta mabadiliko kwa kila mwananchi pasipo na ubaguzi wa aina yoyote.
“Tushiriki kwa namna yoyote tutoe maoni yetu ili yaingizwe kwenye
Katiba mpya. Katiba ndiyo msingi wa sheria zote…Katiba iliyopo sasa
inamapungufu mengi, tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa kuona dosari
hizo na kuridhia kuanza kwa mchakato wa uundwaji Katiba Mpya,” alisema
kiongozi huyo.
Hata hivyo wakichangia wananchi hao katika mkutano huo walioneshwa
kushangazwa zoezi la ukusanyaji maoni mkoani kwao (Morogoro) kupita huku
wengi wakiwa hawajui chochote wala kushiriki kutoa maoni, jambo ambalo
Bi. Kidala alitoa maelekezo kuwa bado wananafasi kushiriki katika zoezi
hilo kwa nafasi nyingine.
“Kwa sasa bado mnanafasi ya kutoa maoni kwa kuandika barua kwenye
vikundi kwenda Tume ya Katiba, kushiriki katika upendekezaji wawakilishi
kwenye mabaraza ya katiba ili wawakilishe maoni yenu, na pia
kupendekeza wajumbe na wabunge wa Bunge la Katiba…tuelimishe,
tuelimishane na tusichoke kutoa maoni kwani hakuna mtaalamu wala
mbumbumbu katika suala hili,” alisema Kidala.
Kwa upande wake TGNP iliwataka wananchi kuunganisha nguvu katika
utoaji maoni ili sauti zao ziweze kusikika ipasavyo katika uwasilishaji
wa maoni yao kwenye mchakato mzima wa uundaji Katiba mpya.
Tanzania Ready To Send Troops To DRC
Tanzania is ready to send troops to the Democratic Republic of Congo to fight M23 rebels who are making advances to the capital Kinshasa, a minister has said.
Foreign Affairs and International Cooperation
minister Bernard Membe said Thursday that the country would, however,
only send its troops if the UN headquarters in New York immediately
mandated the Southern Africa Development Community (SADC) to deploy
troops in DRC.
Presidents from the Great Lakes Region are meeting
in Kampala Friday for a crisis summit during which they will discuss
the deteriorating situation in eastern DRC where the rebels have
captured Goma and Sake, 20km away, and vowed to press on with their
offensive to take the South Kivu provincial capital of Bukavu, 300km
south of Goma.
Mr Membe said leaders within the region under
their chairman, Ugandan President Yoweri Museveni, had called a crisis
summit to discuss the matter and see how they could arrest the
situation.
The minister said the UN was currently using
Chapter 6 of its resolutions, which basically allowed peacekeeping and
not peace enforcement. In peace enforcement, the UN troops would, if
need be, use force to execute their mandate.
Presently, there were over 17,000 troops under the
UN who were not doing much to protect the Congolese people and instead,
they were only “observing things”.
“We condemn what the rebels are doing in eastern
Congo….it is unacceptable to Tanzania. But there is an International
Conference of the Great Lakes Region (ICGLR) in Kampala tomorrow
(today), which was called expressly to discuss the matter,” Mr Membe
said.
He said the situation in eastern Congo had huge
impact on all East African states and, if left unchecked, would result
in huge numbers of refugees and internally displaced people.
Source: http://www.africareview.com
Source: http://www.africareview.com
Chadema Uongozi Balaa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitafutia dawa migogoro
inayotokana na baadhi ya makada wake kuonyesha nia ya kuwania urais na
ubunge mwaka 2015, baada ya kuanzisha utaratibu maalumu wa wanachama
wake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gageti hili, mpango huo unakuja wakati Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ametangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, kitendo ambacho kiliwashtua vigogo wa chama hicho akiwamo mwasisi wake, Edwin Mtei.
Mara kadhaa Mtei amekuwa akimwonya Zitto kuwa kitendo chake cha kutangaza nia yake ya kugombea urais kitasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho. Mtei amekuwa akisema kuwa Zitto anatakiwa kuwaunganisha wanaChadema na siyo kuwagawa, au kuwavuruga na kwamba siyo shida kuonyesha hisia za kuwania urais, lakini tatizo ni kuwa hali hiyo inatengeneza mzozo mkubwa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gageti hili, mpango huo unakuja wakati Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ametangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao, kitendo ambacho kiliwashtua vigogo wa chama hicho akiwamo mwasisi wake, Edwin Mtei.
Mara kadhaa Mtei amekuwa akimwonya Zitto kuwa kitendo chake cha kutangaza nia yake ya kugombea urais kitasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho. Mtei amekuwa akisema kuwa Zitto anatakiwa kuwaunganisha wanaChadema na siyo kuwagawa, au kuwavuruga na kwamba siyo shida kuonyesha hisia za kuwania urais, lakini tatizo ni kuwa hali hiyo inatengeneza mzozo mkubwa.
Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu (BOT) enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.
Akizungumza wakati akijibu hoja mbalimbali katika mtandao wa Jamii Forum katikati ya wiki hii, Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema viongozi wa chama hicho walikutana mjini Morogoro hivi karibuni na kutengeneza utaratibu wa watu kutangaza nia wanapotaka kugombea nafasi yoyote ya uongozi.
“Nadhani huu ni uamuzi mzuri wa chama maana watu wengine wana wasiwasi usio na msingi wowote kwamba kuwa na wagombea wengi kwenye chama ni kuvuruga chama,” alisema Zitto na kuongeza:
“Lakini watu haohao wanashangilia kweli wakiona demokrasia inavyotekelezwa kwenye nchi nyingine kama Marekani. Alisema kuwa tatizo la Watanzania wanapenda kuona demokrasia inatekelezwa, lakini wao wanaogopa kuitekeleza, hivyo mwongozo kwa wagombea ambao walipitisha Morogoro utasaidia sana.“Uamuzi wa Morogoro kuhusu mwongozo kwa wagombea utatusaidia sana kuondoa mashaka kama haya,” alisema Zitto.
Mwananchi Jumapili lilipomuuliza Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika kuhusu jambo hilo alionyesha kutofahamu lolote kuhusu utaratibu huo, wala ulipofanyika huo mkutano wa Morogoro.
“Mkutano upi wa Morogoro?” alihoji Mnyika. Alipoelezwa kuwa suala hilo lilizungumzwa na Zitto katika Mtandao wa Jamii Forum alisema: “Muulize kwanza Zitto akupe ufafanuzi ni kikao gani cha chama, pia juu ya huo utaratibu, akikueleza ndiyo urudi tena kwangu.”
Juhudi za kumpata Zitto kueleza kwa undani kuhusu utaratibu huo hazikuzaa matunda, kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu, baadaye kuzimwa kabisa. Akizungumzia azma yake ya kuachana na ubunge kama alivyoahidi mwaka 2005 kuwa, atagombea vipindi viwili pekee Zitto, alisema kuwa aliwaambia wapigakura wake kwamba nia yake ni kuwa rais wa nchi.
“Nia yangu ni kupisha wengine nao wakimbize kijiti cha maendeleo ya jimbo letu na mkoa wetu,” alisema Zitto na kufafanua, “ Nimeshasema mara kwa mara kwamba ukiachana na siasa kazi ninayoipenda zaidi ni ualimu.”
Alisema kuwa akiachana na ubunge atakwenda kufundisha kwa kuwa anapenda kufanya tafiti, kusoma, kuandika na kufundisha.
“Hivi sasa tunaandaa mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu cha Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) mkoani Kigoma, nitafurahi kama nitakuwa mmoja wa wahadhiri wa mwanzo wa chuo hiki,” alisema Zitto.
Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe alisimama kugombea nafasi ya urais akishindana na Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akisimama kwa mara ya kwanza.
Mwaka 2010, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbrod Slaa aligombea nafasi hiyo na kuibuka mshindi wa pili kwa kupata asilimia 26.34 nyuma ya Rais Kikwete ambaye alipata asilimia 61.17.
Hivi sasa tayari kumetokea maneno ya chinichini miongoni mwa wabunge waliopo madarakani wakiwatuhumu baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao wameaanza kuingia katika majimbo yao kutaka kugombea viti hivyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Wabunge hao wanahoji kama wanachama hao wanaofanya hivyo wanataka kugombea ubunge katika uchaguzi ujao ili kukifanya chama kiongeze idadi ya wabunge bungeni, kwa nini wasiende kugombea katika majimbo ambayo hayana wabunge wa chama hicho?Vilevile, chama hicho kilipata msukosuko katika mchakato wa kupata wabunge wa Viti Maalumu katika uchaguzi uliopita na kulazimika kuweka vigezo ambavyo viliondoa manung’uniko hayo.
Baadhi ya vigezo hivyo ni elimu, mchango wa mgombea katika chama, wanawake waliogombea katika majimbo na uzoefu katika ubunge.
Makubwa Haya: ‘Nauza Dawa Ya kukuwezesha Kufaulu Mitihani’
Na Manyerere Jackton
Ukisoma mabango haya niliyokuwekea kwenye ukurasa huu leo, hutapata shida kutambua kuwa matatizo mengi ya Watanzania, si tu kwamba yanasababishwa na wanasiasa. Ndiyo maana nimejiepusha kujadili Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uteuzi wa viongozi wapya wa Sekretarieti ya chama hicho.
Kwa ufupi ni kwamba matatizo ya Tanzania na Watanzania ni zaidi ya siasa na wanasiasa. Ukisoma ujumbe ulio kwenye mabango haya unauona upumbavu unavyotamalaki katika jamii yetu. Bahati nzuri kwa wanaosambaza upumbavu huo ni kwamba wapo wanaouamini, na .... Soma zaidi... http://www.kwanzajamii.com
Ukisoma mabango haya niliyokuwekea kwenye ukurasa huu leo, hutapata shida kutambua kuwa matatizo mengi ya Watanzania, si tu kwamba yanasababishwa na wanasiasa. Ndiyo maana nimejiepusha kujadili Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na uteuzi wa viongozi wapya wa Sekretarieti ya chama hicho.
Kwa ufupi ni kwamba matatizo ya Tanzania na Watanzania ni zaidi ya siasa na wanasiasa. Ukisoma ujumbe ulio kwenye mabango haya unauona upumbavu unavyotamalaki katika jamii yetu. Bahati nzuri kwa wanaosambaza upumbavu huo ni kwamba wapo wanaouamini, na .... Soma zaidi... http://www.kwanzajamii.com
Makubwa Haya;Jengo Lajengwa Mtwara Jiwe La Msingi Lawekwa Dar
Habari ya jumapili ndugu zangu, ni matumaini yangu siku imeanza vyema
ila poleni kwa wote ambao siku ya leo haijanza vizuri kwao ila naamini
itaisha vizuri kwao.
Leo nimewasili majira ya saa mbili mkoani mtwara nikitokea Jijini Dar
kikubwa ambacho nimekiona katika mkoa huu ni mandahari ya kuvutia ya
uwanja wa ndege ambao sehemu kubwa ya jengo la uwanja limekarabatiwa
,sina budi kuwapa sifa mamlaka zinazohusika na viwanha vya ndege kwa
kazi nzuri na ni wito wangu kazi ya ukarabati iendelee na kwa viwanja
vingine pia.
Nikiwa bado nashangaa mjini wa mtwara, niliweza kumuuliza maswali wawili
matatu mwenyeji wangu kuhusu historia ya mkoa huu ukiachilia mbali yale
ninayoyafahamu ambayo nimesoma kwenye Somo la jiografia nikiwa shule.
Swali kubwa lilikuwa kwanini watu wa mikoa ya kusini wamekuwa
wakilalamika kuwa wametengwa na shughuli za kimaendeleo, mfano
miundombinu nk, jibu likikuwa jepesi sana mwenyeji wangu aliniambia
Historia ndio inayofanya mikoa hii kuwa nyuma aliweza kuniambia mengi
kuhusu historia.
Swali hili linipa jibu ambalo sikutegemea kulisikia ila lilinistua na
kunifanya nisahau kuuliza kwa undani je ni historia ipi iliyoitenga
mikoa ya Kusini na maendeleo nikajikuta naama nje ya mada, na kudadadisi
kitu kingine na swali lilikuwa hivi, JE GAS IMEINUFAISHA VIPI MKOA
HUU?, hapa ni kama niliweka chumvi kwenye kidonda kibichi, jibu
lilikuwa gas imekuwa kilio cha wananchi wa eneo ili maana walitegemea
miaka yote waliyosaauliwa katika maendeleo baada ya eneo lao kutumika
uwanja wa mapambano wakati ukombozi kusini mwa bara la africa hasa nchi
za Msumbiji,zimbabwe, labda gas hiyo ingeziba matundu ya simanzi
yaliyopo mioyoni mwao labda gas ingekuwa fidia ya kucheleweshewa fursa
za maendeleo.
Hayo ni maswali ambayo wananchi wa kusini wamekosa majibu ya
kuwaridhisha leo hii wanahoji iweje Rais azindue mradi wa Gas jijini dar
wakati Gas ipo mtwara, ni kufikia kutoa mfano ni sawa jengo linajengwa
Mtwara kisha Jiwe la Msingi linaweka Dar hapa wananchi wanahisi hatua
hii itazidi kuchelewesha maendeleo zaidi katika mkoa wao maana wanahoji
kama gas itakuwa ianpatikana dar je wawekezaji wataona umuhimu gani wa
kuja kuwekeza Mtwara?
Binafsi sipendi kuwa jaji katika jambo hili kuhukumu kama nia ya
serikari ni mbaya au la labda wananchi wanaona wamesalitiwa wanatamani
hiki walichobarikiwa na Mungu kiwatoe katika hali ya umasikini nadhani
hii ni fursa sasa ya serikari kuona ni namna gani wananchi wa maeneo
haya hawapotezi imani na Serikari ya , yapo mambo muhimu serikari
inaweza kufanya ili wananchi hawa wasizidi kusononeka zaidi mi nashauri
kama yawekena hata kama Gas itasafirishwa kwenda popote ila nadhani
wananchi wa maeneo haya wangepewa kipaumbea maana tunaambia Gas
inakwenda kuzalisha umeme hivyo nadhani wananchi wa mikoa ya kusini
wangefikiriwa hata kupunguziwa gharama ya nishati ya umeme kwangu mimi
hii naona itakuwa moja ya jawabu .
Huu ni mtazamo wangu kama mtanzania
(Pamoja Tuijenge Nchi Yetu)
MKAMI JR - Mjengwa Blog -Mtwara
Washia Dar Wamkumbuka Mjukuu Wa Mtume
Pichani Juu na Chini Waumini wa
dhehebu la Shia wakiwasili na kukusanyika katika eneo la makaburi ya
Washia Kisutu jijini Dar es Salaam wakijiandaa kuanza maandamano ya
kuadhimisha siku ya Ashura kukumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Mohammed
(S.A.W) Imam Hussein yaliyofanyika
jana
Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamaat Shia Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa waandishi wa habari amesema katika kuadhimisha siku hii Waislam wa dhehebu la Shia watafanya matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo ndani yake kutakuwa kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za maombolezo tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi kujipa uhai kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa watu wake na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya wenzake
Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi.Amesema kifo cha Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo haki ilizimwa na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka batil isimame , kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.Aidha Sheikh Salum amesema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo, kutetea wanyonge, kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna yoyote ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.
Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamaat Shia Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa waandishi wa habari amesema katika kuadhimisha siku hii Waislam wa dhehebu la Shia watafanya matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo ndani yake kutakuwa kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za maombolezo tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi kujipa uhai kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa watu wake na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya wenzake
Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi.Amesema kifo cha Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo haki ilizimwa na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka batil isimame , kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.Aidha Sheikh Salum amesema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo, kutetea wanyonge, kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna yoyote ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.
No comments:
Post a Comment