Monday, July 29, 2013

RAIS KIKWETE AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI KAGERA

 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani BiharamuloRais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo. 
Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo  Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani NgaraRais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (1)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya KyerwaRais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (2)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu jana Jumamosi Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu  Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto RusumoKivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Jumamosi Julai 27, 2013Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Rais Kikwete akihutubia umati NgaraRais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe Rais Jakaya Kikwete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku nane.Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (2)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (3)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya KyerwaUmati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (4)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa .(PICHA NA IKULU).

RAIS KIKWETE WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA

Rais Kikwete akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara wakati akiwasili kwenye kiwanja cha kijiji hicho tayari kwa kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera
Rais Kikwete akiwapungia mkono wakazi wa kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara wakati akiwasili kwenye kiwanja cha kijiji hicho tayari kwa kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera
Rais Kikwete akihutubia umati mkubwa wa wananchi wa Wilaya ya Ngara,Mkoani Kagera wakati wa Muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Kagera.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Prof Anna Tibaijuka akielezea baraza la ardhi.Kushono ni Rais Kikwete akisikiliza kwa Makini.
Waziri wa Kilimo,Inj. Christopher Chizza akielezea mipango kabambe ya kilimo kwa wakazi wa Ngara.Kushono ni Rais Kikwete akisikiliza kwa Makini.
Waziri wa Maji,Prof. Jumanne Maghembe akilieleza mipango kabambe ya maji.Kushono ni Rais Kikwete akisikiliza kwa Makini.
Waziri wa Nishati na Madini,Prof. Sospeter Muhongo akieleza mikakati mbali mbali ya nishati ya Umeme.Kushono ni Rais Kikwete akisikiliza kwa Makini.
umati wa watu ukimsikikliza Rais Kikwete kijiji cha Rulenge,Wilayani Ngara.PICHA NA IKULU.

RAIS KIWETE AKIWA WILAYANI MULEBA

Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera
Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni
Rais Kikwete akisalimiana na mama wa Profesa Anna Tibaijuka
Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba
Rais Kikwete akiongea na viongozi wa wilaya ya Muleba baada ya kupokea taarifa ya maendeleo, akiwa na mawaziri watano anaoongozana nao katika ziara hiyo
Mbunge wa Muleba akitoa  maoni na kero za jimbo lake
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiwahakikishia viongozi wa Muleba juu ya mipango ya serikali kuleta meli za abiria mpya mbili katika ziwa Victoria
Rais Kikwete akipata maelezo ya mpango kabambe wa maji wilaya ya Muleba
Rais Kikwete akizindua mradi mkubwa wa maji wilayani Muleba
Rais Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa maji
Rais Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Muleba baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji kwa wilaya hiyo
Mwananchi mwingine akitwishwa maji
Ngoma ya utamaduni ikimlaki Rais Kikwete alipowasili katika mkutano wa hadhara
Rais Kikwete akisalimia wananchi
Rais Kikwete akiangalia mazao yatokanayo na uzalishaji mbegu ya kampuni ya Itente ya Muleba
Rais Kikwete akipozi na wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji mbegu ya Itente
Rais Kikwete akifurahia ngoma
Umati wa wananchi Muleba ukimsikiliza Rais Kikwete
Rais Kikwete akiongea na wananchi wa Muleba
Rais Kikwete akihutubia wana Muleba
Sehemu ya umati mkutanoni
Rais Kikwete akiendelea kungea na wananchi
Umati  katika mkutano wa hadhara
Umati katika mkutano wa hadhara
Rais Kikwete akijiunga na waumini wa Muleba kusali swala ya Magharibi kabla ya kufuturu
Dua ikisomwa baada ya futari aliyoandaa Rais Kikwete kwa wananchi wa Muleba
Dua ikiombwa baada ya futari
Dua
Wananchi wa Muleba katika futari aliyoandaa Rais Kikwete wilayani Muleba

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA KAMBI YA KABOYA, BUKOBA, MKOANI KAGERA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mkuki katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013
Viongozi wa dini wakisoma dua kwenye maadhimisho hayo. Pembeni ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu
Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.Katika maadhimisho haya alikuwepo pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman MakunguPICHA NA IKULU
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wazee waliopigana vita miaka ya zamani wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ulinzi,Mh. Shamsi Vuai Nahodha wakati walipokutana na kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera Julai 25, 2013.Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali na wa pili kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Davis Mwamunyange. PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AWASILI MJINI BUKOBA LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba leo Julai 24, 2013.
Rais Jakaya Kikwete pamoja na Viongozi mbali mbali wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Kagera Coperative Union leo Julai 24, 2013
mjini Bukoba.
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Bukoba baada ya ufunguzi wa jengo la Kagera Coperative Union leo Julai 24, 2013 mjini Bukoba.
Picha ya pamoja.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa Mji wa Bukoba,waliofika kumuona jioni ya leo.PICHA NA IKULU.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAKAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TANZANI,IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi na Bw. Manoj Kohli wa Airtel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Pamoja wa chama hicho alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Beatrice Singano, mmoja wa wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na wajumbe wa Chama cha Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA TONY BLAIR IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwonesha mandhari mbalimbali Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe Tony Blair na mkewe Cherrie Blair
alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.PICHA NA IKULU.

RAIS KIKWETE AWAONGOZA WANANCHI KUAGA NA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MIILI YA ASKARI 7 WALIOFARIKI HUKO DARFUR,SUDANI

 Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam. 
 Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnard Mengi, akiwa na baadhi ya viongozi, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Majeneza yenye miili ya Askari wa kulinda Amani, wa jeshi la Ulinzi la Tanzania, waliokufa huko Darfur Julai 13, 2013, wakati wa zoezi la kuagwa miili hiyo lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi, Upanga jijini Dar.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Bilal, na viongozi wengine wakiwa katika shughuli hiyo ya kuagwa miili ya askari hao leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga Dar es Salaam. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. Kulia ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
 Majeneza yenye miili yakiwa eneo la tukio tayari kuagwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Mkuu wa Majeshi,Jenerali Davis Mwamunyange, akizungumza wakati wa zoezi hilo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.
 Baadhi ya Askari pia wakiwa na nyuso za huzuni.PICHA NA OMR.

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA SIKU MOJA WA TROIKA YA SADC JIJINI PRETORIA, AFRIKA KUSINI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijibu maswali toka kwa wanahabari wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku. Kutoka kulia ni Rais wa Afrika Kusini Mhe Jacob Zuma, Rais wa Msumbiji ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC Mhe Armando Guebuza, Katibu Mtendajji wa SADC Dkt Tomaz Augusto Salomão na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.
Mwenyekiti wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Armando Guebuza baada ya mkutano wa kamati ya Troika katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation). Kutoka kulia ni Mwenyeiti wa Chama cha Wataalam Watanzania waishio Afrika Kusini, Dkt Hamza Mokiwa, Mwenyekiti wa Tanzania Women in Gauteng (TWIGA), Mama Scholastica Kimario, Rais Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe Radhia Msuya, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Afrika ya Kusini Bw. Deusdedit Rugaiganisa na Bw. David Mataluma, mratibu wa Vijana katika Jumuiya ya Watanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na balozi pamoja na maofisa wa ubalozi muda mfupi kabla ya kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomndoka leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Radhia Msuya leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation).PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WA JWTZ CHUO CHA MAFUNZI YA KIJESHO MONDULI, LEO

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika uwanja wa gwaride wa Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, tayari kwa kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali V.K. Mritaba. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Ofisa Kadet Ngodoke kwa kuibuka mwanafunzi bora wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Ofisa Kadet D.G.L. Wong- Pool toka Visiwa vya Ushelisheli kwa kuibuka mwanafunzi bora wa kigeni wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa katika Chuo cha Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na
Visiwa vya Shelisheli.
Meza kuu wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na
Visiwa vya Shelisheli.
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange baada ya sherehe za kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.PICHA NA IKULU

SHUGHULI MBALIMBALI ZA RAIS KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi wa Sweden nchini Mhe Lennarth Hjelmaker aliyeonana naye kwa ajili ya kuwasilisha Ujumbe kutoka Serikali yake leo Ikulu, jijini Dar es salaam. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Hamisi Amir Msumi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Hilda A. Gondwe kuwa Mjumbewa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Celina Augustine M. Wambura kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakipiga picha ya pamoja na Mwenyekiti mpya wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Serikali Mhe Hamisi Amiri Msumi pamoja na wajumbe wapya Mhe Hilda A. Gondwe na Mhe Celine Augustine M. Wambura na viongozi wa Tume hiyo leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na  Mhe Hamisi Amir Msumi na familia yake baada ya kumuapisha kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya kumbukumbu na  Mhe Hilda A. Gondwe  na familia yake baada ya kumuapisha kuwa Mjumbewa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha na Mhe Celina Augustine M. Wambura na familia yake baada ya kumuapisha kuwa Mjumbe wa Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma leo Ikulu jijini Dar es salaam. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Mansoor Daya Chemicals alipokutana naye leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa  Irrigation System Ltd Bw. Choudhari Pramot na ujumbe wake aliokutana nao leo Ikulu  jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Kikwete Mkurugenzi Mkuu wa  Irrigation System Ltd Bw. Choudhari Pramot baada ya maongezi naye leo Ikulu  jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

JK atembelea viwanja vya Saba Saba

 JK akilakiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda alipotembelea maonesho ya SabaSaba Barabara ya Kilwa Road jijini Dar es salaam. Kati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema
 Akisalimiana na maafisa waandamizi wa wakala wa Biashara TANTRADE
 Akipata taarifa fupi
 Dkt Kigoda na Katibu Mkuu wake Mhe Joyce
 Wadau wa FNB
 Banda la China
 Mdau akijaribui mgolole wa kimasai
 Mvinyo toka Dodoma katika banda la EOTF
 JK akijadiliana jambo na Mama Anna Mkapa, Mwenyekiti wa EOTF
 JK akipata maelezo katika banda la Taasisi ya saratani ya matiti
 JK akitembelea mabanda
 JK akiwasili banda la JWTZ
 JK akisalimiana na komandoo katika banda la JWTZ
  JK akiwa na waziri wa Maliasili na Utalii balozi Kagasheki na naibu wake Mhe Lazalo Nyalandu
 Banda la Asali
 Banda la Nyuki
Wadau wa TANTRADE

MAPOKEZI YA RAIS OBAMA IKULU, NA MKUTANO WAKE NA WANAHABARI JIJINI DAR LEO

Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam mchana wa leo.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokewa kwa Shangwe Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mgeni wake,Rais Barack Obama wa Marekani wakati walipokuwa wakielekea sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Waandishi wa habari Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa maelezo ya mti wa mpingo anaotaka kuupanda katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Barack Obama wa Marekani na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakizungumza na waandishi wahabari Ikulu,Jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa maelezo ya mti wa mpingo aliotaka kuupanda Rais wa Marekani,Barack Obama katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais Obama akipanda mti aina ya mpingo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho kikwete akimsindikiza mgeni wake baada ya kumpatia mapokezi ya kihistoria leo Ikulu.PICHA NA ISSA MICHUZI,IKULU.

Rais Kikwete ampokea Rais wa Marekani,Barack Obama

 Rais Barack Obama wa nchini Marekani na Mkewe Michelle Obama wakiwa sambamba
na watoto zao,wakiwasili chana huu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Nyerere,jijini Dar es Salaam mchana huu kwa ziara ya siku
mbili hapa nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Barrack Obama wa Marekani
muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam mchana wa leo. Kulia ni Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani
muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana.nyuma ya Rais na
mgeni wake ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mke wa Rais wa Marekani
Mama Michelle Obama.

Rais Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani Rais wa Zanzibar Dr.Ali Mohamed Shein muda mfupi baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam leo mchana.Huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa
Rais wa Marekani Michelle Obama Wakiangalia.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya
Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku
mbili.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kwa Rais Barrack Obama wa
Marekani makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi muda mfupi baada ya
Rais huyo wa Marekani kuwasili nchini kwa Ziara ya kikazi ya siku
mbili.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akisalimiana
na Rais Barrack Obama katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es Salaam leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwaongoza wageni wao Rais
Barrack Obama wa Marekani na mkewe Michelle kuangalia ngoma mbalimbali
za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ziara ya siku mbili nchini.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Barrack Obama wa Marekani
wakifurahia na kufuata mapigo ya ngoma za utamaduni katika uwanja wa
Ndege wa Mwalimu jijini Dar es Salaam leo mchana wakati wa mapokezi ya
kiongozi huyo wa Marekani na ujumbe wake.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwatambulisha baadhi ya viongozi waandamizi
wa serikali kwa Rais Barrack Obama na mkewe katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha na Freddy
Maro,Ikulu.

RAIS KIKWETE AFANYA UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP JIJINI DAR

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013
Rais Kikwete na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Mjadala ukiendelea
Rais wa Sri Lanka akishiriki mjadala na vijana wa CPTM 29ers
Rais Omar Bongo katika mjadala huo
Kijana akichangia
Vijana wakichangia mjadala
 
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala
 
Kijana akichangia katika mjadala
Rais wa Sri Lanka na Dkt Mihaela Smith wakifuatilia mjadala
 
 
 
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
Rais Kikwete akisalimiana na vijana hao
Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
Wageni mbalimbali katika mkutano huo
Ujumbe wa Swaziland
Ujumbe wa Tanzania
Meza kuu
Meza kuu
Vijana nwa THT wakitumbuiza
 
 
Viongozi mbalimbali
THT wakitumbuiza
Meza kuu wakifurahia onesho la THT
Wanafunzi wakiimba kwa furaha
 
Meza kuu wakishangilia
Sehemu ya wageni

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI SINGAPORE KWA KUTEMBELEA MAENEO MBALIMBALI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji Upya wa Miji Upya ya Singapore leo Juni 6, 2013 ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembelea Taasisi ya Elimu ya ufundi (Institute of Technical education) iliyo sawa na VETA kwa Tanzania leo Juni 6, 2013.ambapo pamoja na mambo mengine walijionea jinsi wanafunzi wake wanavyofundishwa kuunda vipuli vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vya ndege.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakitembezwa kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Ustawishaji mijini ya Singapore leo Juni 6, 2013.ambapo wanajionea mfano wa jiji hilo ukiwa umetengenezwa mahususi kwa kuhakikisha mji unapangwa na kusimamiwa kisayansi kwa mipango miji ya muda mfupi na muda mrefu.
Baadhi ya wafanyabiashara walioongozana na Rais Jakaya Kikwete katika ziara ya kikazi nchini Singapore wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mawaziri walio katika msafara huoleo Juni 6, 2013. . Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe (wa tatu) kulia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Upya ya Miji ya Singapore leo Juni 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Elimu ya Ufundi ya Singapore baada ya kutembelea kampasi yao jijini Singapore leo Juni 6, 2013.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AWASILI SINGAPORE KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Bw. Laurence Bay, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Singapore. Kushoto ni Balozi wa Tanzania India na Singapre Injinia John Kijazi na mbele yao ni Naibu Mkurugenzi wa Itifaki wa Singapore Bi. Christine Tay.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe,akifuatiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara,Mh. Abdallah Kigoda pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mh. Anne Tibaijuka wakati Rais akiwasili nchini Singapore leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kasulu mjini Mhe Moses Machali pamoja na wadau wengine wakati akiwasili Singapore.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea jijini Singapore leo wakati alipokutana na wafanyabaishara za ujenzi wa nchi hiyo marav tu baada ya kutua kutoka Japan alikokuweko kwa ziara ingine ya kikazi. Katika mkutano huu Rais Kikwete aliwakaribisha wafanyabishara hao wa Singapore Tanzania kuwekeza katika sekta ya nyumba wakati wa chakula cha jioni kilichiandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).PICHA NA IKULU

PRESIDENT KIKWETE MEETS PRIME MINISTER OF JAPAN SHINZO ABE IN TOKYO

 President Dr Jakaya Mrisho Kikwete is  received by the  Prime Minister of Japan Mr Shinzo Abe for official talks in Tokyo this morning. President Kikwete who is Japan for a working visit is scheduled to attend the Fifth Tokyo International Conference on African Development (TICAD V) to be held in Yokohama Photos by Freddy Maro
 President Dr Jakaya Mrisho Kikwete being invited by the  Prime Minister of Japan Mr Shinzo Abe for official talks in Tokyo this morning.
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in official talks with the  Prime Minister of Japan Mr Shinzo Abe in Tokyo this morning.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI ADDIS ABABA, ETHIOPIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani Mh Liberata Mulamula walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Mohamed Morsi walipokutana wakati wa mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibe walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibe na ujumbe wake walipokutana pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel Sidibe pamoja na Mratibu wa Masuala ya Ukimwi wa Marekani Balozi Eric Goosby walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Waziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulishaWaziri Mkuu wa Jamaica Bi. Portia Simpson Miller kwa Mhe Gideon Moi, Seneta wa Kaunti ya Baringo nchini kenya na ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha KANU cha nchi hiyo walipokutana pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika Mkutano wa kawaida wa 21 wa Umoja wa Afrika katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa taaisi ya kimataifa inayoshughulikia mapambano dhidi ya Ukimwei, Kifua Kikuu na Malaria ya The Global Fund Dkt Mark Dybil na afisa wa taasisi hiyo Bi Shu-shu Tekle-Haimanot walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) professor Ntumba Luaba na ujumbe wake walipokutana na kufanya mazungumzo pembeni ya mkutano na sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MARAIS WASTAAFU, AHUDHURIA KIKAO CHA AMANI DRC CONGO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizingumza na Marais Wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim kuhusiana na sherehe za miaka 50 ya AU alipokutana nao jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo Mei 26, 2013. Viongozi hao wastaafu ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioaliokwa kwenye sherehe hizo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa Kanda wa Usimamizi wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika DRC na nchi za Maziwa Makuu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika leo Mei 26, 2016.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wanahabari baada ya kuhudhuria Mkutano wa Kanda wa Usimamizi wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika DRC na nchi za Maziwa Makuu katika makao makuu ya Umoja wa Afrika leo Mei 26, 2016.PICHA NA IKULU.

TASWIRA MBALIMBALI ZA RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA KWENYE MAKAO MAKUU YA UMOJA HUO JIJINI ADDIS ABABA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika chumba cha mikutano baada ya kuhudhuria kikao cha 29 cha wakuu wa nchi za NEPAD pembeni ya mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
Marais wastaafu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia. Kutoka kushoto ni Dkt Kenneth Kaunda (Zambia), Sam Nujoma (Namibia) na Mzee Festus Mogae (Botswana).
Mama Salma Kikwete na wake wa marais wengine wakiwa katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika na wageni mashuhuri walioalikwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika na wageni mashuhuri walioalikwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
Wapiga picha toka nchi mbalimbali wakiwa kazini wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
Wajumbe, wageni waalikwa, wanahabari na wadau mbalimbali wakijichanganya nje ya ukumbi wa mkutano wakati wa mapumziko.
Mandhari za nje na ndani ya jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mhe Ban Ki Moon akiwa meza kuu pamoja na Rais wa AU Mama Nkosazana Dlamini Zuma na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn na viongozi wengine wa umoja huo.
Sehemu ya ukumbi wa mikutano kwa ndani.
Viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA AU JIJINI ADDIS ABABA LEO

Muono wa jicho la samaki katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.
Viongoi mbali mbali wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) wakiwakumbuka waliotangulia mbele ya haki.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013. 
Marais Wastaafu wakiwa katika Mkutano wa Sherehe za miaka 50 ya AU katika makao makuu ya umoja huo jijini Addis Ababa leo Mei 25, 2013.PICHA NA IKULU.

RAIS KIKWETE AWASILI ADDIS ABABA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 50 ZA UMOJA WA NCHI ZA AFRIKA (AU)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni miongomi mwa marais wa bara la Afrika watakaohudhuria Sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazo fanyika rasmi leo Jumamosi Mei 25, 2013 katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa, Ethiopia. 
 
 Shamrashamra zimetawala kila pembe ya jiji la Addis, wakati viongozi wa nchi za Afrika wakiwasili mmoja baada ya mwingine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole. 
 
 Muungano wa Afrika wakati huo ukijulikana kama OAU, ulizaliwa Mnamo Mei 25, 1963 jijini Addis Ababa, ukianza na nchi za 32 na baadaye nchi 21 zikajiunga miaka ilivyozidi kwenda, huku Afrika ya kusini ikijiunga kuwa mwanachama wa 53 mwaka 1994. 
 
Mwaka 2001 OAU iligeuzwa kuwa AU katika mkutano uliofanyika Lusaka, Zambia.Jumamosi hii kutakuwa na sherehe za kilele kuadhimisha miaka hiyo 50 ya AU na kuhudhuriwa na marais karibia wote wa Afrika.
 
 Kauli mbiu ya sherehe za hapo kesho ni mjadala mkuu kuhusu ushirikiano wa nchi za Afrika na kuimarishwa kwa muungano huo.Mwenyekiti wa tume ya muungano huo, Dr Nkosazana Dlamini Zuma, anaseme kuwa hii itakuwa fursa kwa AU kujadili kuhusu uwezo wa bara hili na ambacho kinaweza kufikiwa katika miaka 50 ijayo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa alipowasili Ijumaa usiku  tayari kujiunga na viongozi wenzie wa nchi za Afrika katika sherehe za miaka 50  tangu kuanzishwa kwa Umoja  wa  nchi za Afrika (AU) zinazofanyika leo katika makao makuu ya umoja huo
Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiwasili Addis Ababa
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya maandalizi ya sherehe hizo toka kwa balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Profesa Joram Biswaro mara baada ya kuwasili Addis Ababa

President Kikwete meets with Finland Delegation

H.E. President Jakaya Mrisho Kikwete (right), President of the United Republic of Tanzania Thursday (May 23, 2013) met with Hon. Dr. Alexander Stubb, Minister for European Affairs and Foreign Trade at the State House in Dar es Salaam.  
President Kikwete (center) in a group photo with Hon. Dr. Alexander Stubb (left) and Hon. Heidi Hautala (right), Minister for International Development, prior to the beginning of their discussion that highlighted the current mobile connection industry that has become a big demand for farmers in the country, including the alternative ways of using land such as forestry farming. 
H.E. President Kikwete in discussion with Hon. Dr. Alexander Stubb (2nd right), Minister for European Affairs and Foreign Trade, Hon. Heidi Hautala (2nd left), Minister for International Development and H.E. Sinikka Antilla (left), Ambassador of Finland in the United Republic of Tanzania.  Minister Stubb is in the country with a business delegation from Finland to discuss and explore areas of partnership in development such as higher education, innovative agricultural programs and infrastructure building.  
Hon. Bernard K. Membe (MP) (left), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation and Ambassador Dora Msechu, Director of the Department of Europe and Americas listening to President Kikwete discussion with delegation from Finland. 
 
Finland delegation that consisted of top businessmen in talks with President Kikwete (not in the photo) at the State House in Dar es Salaam.  The businessmen discussed with President Kikwete the need to mobilize farmers through KILIMO KWANZA program by facilitating them with communication technological devices that are affordable and useful in transmitting useful agricultural information among them.  The businessmen had recently signed a joint-venture deal with Vodacom aim at providing affordable mobile phones as a way of enhancing communication among farmers in rural areas.
 
Hon. Bernard K. Membe (MP) (left), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation and Ambassador Dora Msechu (2nd left), Director of the Department of Europe and Americas in the Ministry, listening to President Kikwete discussion with his guests at the State House.  President Kikwete further discussed telecommunication sector and the need to have more investors that can help build more infrastructures in rural areas to help economy grow in the country.   Others in the photo are Mr. Lumbila Fyataga (3rd left), Deputy Private Secretary to the President, Ms. Upendo Mwasha (right – back roll), Foreign Service Officer in the Ministry and Mr. Thobias Makoba, Assistant Private Secretary to Minister Membe.  
H.E. President Kikwete (2nd left – front roll), in a group photo with Hon. Dr. Alexander Stubb (left – front roll), Minister for European Affairs and Foreign Trade, Hon. Heidi Hautala (2nd right – front roll), Minister for International Development and other top businessmen from Finland.
 
All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MAONYESHO YA MFUMO WA MATOKEO MAKUBWA ‘SASA’ AWAMU YA KWANZA

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwasili kwenye Ukumbi wa Jumba la Makumbusho ya Taifa, leo Mei 24, 2013 kwa ajili ya Kufungua rasmi Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa ‘Sasa’ Awamu ya kwanza.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mchambuzi Sera Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mipango, Lorah Madete, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mtafiti Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Shetto, wakati walipokuwa wakitembelea Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa Awamu ya Kwanza, baada ya kuyafungua rasmi leo katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati wa Ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa ‘Sasa’ Awamu ya Kwanza leo Mei 24, 2013.
Wanamuziki wa Bendi ya Mjomba, wakiimba kutoa burudani katika Maonesho ya Mfumo wa Matokeo Makubwa ‘Sasa’ Awamu ya Kwanza, yaliyofunguliwa na Rais Jakaya Kikwete, leo Mei 24, 2013. Picha na OMR
 
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, AKIFUNGUA WARSHA YA WAZI (OPEN DAY) KUHUSU MFUMO MPYA WA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KITAIFA YA KIPAUMBELE, VIWANJA VYA MAKUMBUSHO YA TAIFA, DAR ES SALAAM, MEI 24, 2013

Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mhe. Seif Shariff Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Waheshimiwa Mawaziri na Manaibu Waziri;
Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi;
Makatibu Wakuu;
Dkt. Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango;
Washirika na Wadau wa Maendeleo;
Viongozi wa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma;
Viongozi wa Kidini na Sekta Binafsi;
Wataalamu Elekezi kutoka PEMANDU na Mckinsey;
Washiriki wa Maabara;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana:
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wote katika Warsha ya Wazi kuhusu mfumo mpya unaoanzishwa na Serikali wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kitaifa ya kipaumbele.  Warsha hii inatoa nafasi ya pekee kwa wananchi kushiriki na kutoa mawazo yao jinsi ya kuboresha mfumo huo unaopendekezwa.  Ni Warsha ya kuelimishana, kubadilishana mawazo na kufahamishana mipango na mambo ambayo Serikali inatarajia kuyafanya katika siku za karibuni. 
Namshukuru Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Philip Mpango, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, viongozi na watumishi wote wa Tume ya Mipango kwa kuandaa Warsha hii mahsusi.  Kwa namna ya pekee nawashukuru pia wataalamu wa PEMANDU na McKinsey kwa kushirikiana vizuri na wataalam wetu katika kila hatua ya safari hii ambayo Serikali yetu imeianza.
Ndugu Wananchi;
Kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo sio jambo geni hapa nchini.  Ni jambo ambalo tumelifanya tangu tupate Uhuru na tunaendelea nalo.  Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ilianza na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo mwaka 1961 – 1964.  Mpango huo uliainisha maadui watatu wa maendeleo ambao ni umaskini, ujinga na maradhi.  Mikakati mbalimbali na mipango madhubuti ya maendeleo ilibuniwa ili kupambana na maadui hao.  Baada ya hapo ukaja Mpango wa Maendeleo wa Miaka 15 wa mwaka 1964 – 1980, uliokuwa umegawanywa katika vipindi vitatu vya utekelezaji vya miaka mitano mitano.
Baadhi yenu mtakumbuka kuwa utekelezaji wa vipindi viwili vya mwanzo ulikuwa wa kuridhisha.  Hata hivyo, utekelezaji wa kipindi cha mwisho cha Mpango ule, yaani kati ya mwaka 1975 – 1980, ulikuwa duni mno.  Utekelezaji wake ulivurugwa sana na changamoto za wakati ule kama vile kupanda sana bei ya mafuta, kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (1977) na Vita ya Kagera.  Mambo haya yalisababisha fedha zetu nyingi kutumika kuagiza mafuta, kujenga taasisi zetu wenyewe na kutetea mipaka ya nchi yetu.  Rasilimali kidogo tuliyonayo ikaenda huko badala ya kugharamia miradi ya maendeleo.   
Ndugu Wananchi;
Pamoja na changamoto zilizojitokeza, Serikali iliamua kuanzisha mpango mwingine wa maendeleo wa muda mrefu wa mwaka 1981 – 2000.  Kwa bahati mbaya mpango huo nao haukutekelezwa kufuatia kuendelea kudorora kwa uchumi.  Kati ya mwaka 1981 na miaka ya 90 mwanzoni, Serikali ilianza kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi.  Tukawa na National Economic Survival Programme (NESP) mwaka 1981 – 82 na Structural Adjustment Programme (SAP) mwaka 1982 – 1985.  Mipango hiyo haikutekelezwa vizuri kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa rasilimali za kutosha.  Kati ya mwaka 1986 – 89, Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ikaanza kutekeleza programu ya kwanza ya kufufua uchumi (ERP – I).  Ya pili ikafuatia kati ya mwaka 1989 – 1992.
Mwaka 1994 Serikali ikaanza kuandaa mpango wa maendeleo wa muda mrefu utaowezesha kuzikabili changamoto mpya kufuatia mageuzi ya kiuchumi na kijamii yaliyokuwa yanaendelea nchini na duniani kwa ujumla.  Kazi hiyo ilikamilika mwaka 1999 na kuzinduliwa kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.  Malengo ya Dira hiyo ni kuleta maendeleo ya haraka nchini na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.  Maana yake ni kwamba wananchi wawe na chakula cha kutosha, huduma ya elimu na afya iliyo bora iwafikie watu wengi zaidi, vifo vya watoto na akina mama vipungue, wastani wa kuishi uongezeke, maji safi na salama yapatikane kwa wote, uhalifu upungue na umaskini uliokithiri usiwepo kabisa na pato la wastani la Watanzania liwe zaidi ya dola za Kimarekani 3,000.  Vile vile pawe na maendeleo ya viwanda, matumizi ya teknolojia na sayansi yaongezeke, miundombinu ipanuke na uchumi ukue kwa asilimia 8 au zaidi. 


Ndugu Wananchi;
Juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali za awamu zote ikiwemo na hii ninayoiongoza mimi zimeleta mafanikio ya kutia moyo.  Kwa mfano, uchumi wa nchi umekua kwa wastani wa asilimia 7 kwa miaka kumi iliyopita, mfumuko wa bei upo chini ya asilimia 10, mapato ya ndani yameongezeka, mauzo ya nje yameongezeka na hifadhi ya fedha za kigeni imeongezeka pia.  Hata hivyo, idadi ya Watanzania walio maskini bado ni kubwa hususan umaskini wa kipato.  Vile vile bado hatujafanikiwa kufikia malengo katika maeneo mengi tuliyojiwekea.  Hata tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2025 tuliyofanya mwaka 2000 imethibitisha hivyo.  Hatuendi kwa kasi inayotakiwa na utekelezaji wake siyo wa kuridhisha.  Matokeo yake tupo nyuma ya hatua tuliyotakiwa kuwa.  Kwa mfano, kwa upande wa safari ya kuelekea pato la wastani la watu kuwa dola 3,000 mwaka 2025, tulitakuwa tuwe tumefikia dola 995 mwaka 2010.   Lakini ilikuwa tumefikia dola 545 tu.  Kwa ukuaji wa uchumi, tulitakiwa tuwe asilimia 8, lakini tulikuwaasilimia 7
Zipo changamoto nyingi za ndani na nje, zilizofanya tusifikie malengo hayo:  Kubwa ni misukosuko ya uchumi wa dunia, uhaba wa rasilimali fedha na ufuatiliaji mdogo katika utekelezaji wa miradi iliyoainishwa kuleta maendeleo. Aidha, mipango na mikakati ya maendeleo ilikuwa na vipaumbele vingi kwa wakati mmoja wakati rasilimali za utekelezaji wake ni kidogo.  Hali hii haikutuwezesha kujielekeza ipasavyo kwenye maeneo yenye kuleta matokeo makubwa na kwa haraka.
Ndugu Wananchi;
Baada ya kutafakari yote haya, tukafikiria namna ya kuweza kufikia malengo yetu ya Dira ndani ya muda uliobakia. Hivyo, tukaamua kuja na Mpango ya Maendeleo wa Muda Mrefu wa Miaka 15 ambao utatekelezwa katika awamu tatu za miaka mitano mitano. Katika Mpango wa Kwanza Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16), maeneo yaliyopewa kipaumbele ni Miundombinu, Kilimo, Viwanda, Huduma za jamii na Uendelezaji Rasilimali Watu na Utalii, Biashara na Huduma za Fedha.  Changamoto kubwa ikabaki kuimarisha mfumo wetu wa kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ili kuleta matokeo ya haraka.  Kuendelea kufanya vilevile tulivyokuwa tukifanya kusingeweza kuleta mabadiliko tuliyokuwa tunayataka katika utekelezaji wa mipango yetu.  Ilibidi tubadilike, ikiwezekana tukimbie pale ambapo wengine wanatembea. 
Ndugu Wananchi;
Tukiwa katika hali hiyo ya kutafakari cha kufanya, mwezi Mei, 2011 ikawa bahati mimi kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa “Langkawi  International Dialogue” uliofanyika mjini Kuala Lumpur, Malaysia.  Katika mkutano huo, Serikali ya Malaysia iliwasilisha mada jinsi inavyoendesha na kusimamia utendaji wake ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na huduma kwa jamii.  Mimi na viongozi wenzangu tuliohudhuria mkutano huo tulivutiwa sana na mfumo wa utendaji wa Malaysia na tukadhamiria kujifunza zaidi kutoka kwao.  Tukaomba watusaidie.  Bahati nzuri Serikali ya Malaysia ikakubali ombi letu na kuandaa warsha maalum mwezi Novemba, 2011.  Ujumbe wa Tanzania kwenye warsha hiyo ya aina yake uliongozwa na Dkt. Philip Mpango.  Waliporudi, tukaamua kuwa na sisi tuanze kutumia utaratibu wa Malaysia wa “Matokeo Makubwa Sasa” ama kwa Kiingereza “Big Results Now”.
Ndugu Wananchi;
Utekelezaji wa mfumo wa “Big Results Now” hapa nchini ulianza kwa kuainisha maeneo sita yenye uwezo wa kutupatia matokeo makubwa kwa haraka. Maeneo hayo ni nishati, elimu, maji, miundombinu, kilimo na utafutaji fedha.  Kazi ya kuchagua maeneo sita ya kwanza nayo haikuwa rahisi.  Tulibishana sana katika kuchagua vipaumbele vichache lakini vyenye kuleta matokeo makubwa.  Hatimaye tukafanikiwa.  Vipaumbele hivi vinabeba msingi wa kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa Tanzania kwa ujumla na kuchochea ustawi wa maisha bora kwa wananchi. 
Hatua ya pili ikawa ni kufanya uchambuzi wa kina kupitia awamu ya kwanza ya maabara (lab) kama alivyoeleza Katibu Mkuu Kiongozi. Kazi hiyo ilitekelezwa kwa wiki sita mfululizo na wataalam wetu zaidi ya 300 kutoka nyanja na sekta mbalimbali na kukamilika tarehe 05 Aprili, 2013. Nawapongeza sana kwa kazi hiyo kubwa na moyo wao wa kujitolea. Tumeandaa ratiba ya utekelezaji kwa kila mradi na programu ikionyesha kazi zilizopangwa kufanywa, mtekelezaji-husika na muda na kukamilisha kazi.  
Katika mfumo huu, Mawaziri na Watendaji katika Wizara na Idara watapimwa kwa vigezo vilivyo wazi na ninyi wananchi mtapata fursa ya kuvijua vigezo hivi pamoja na matokeo ya upimaji.  Hapatakuwa na siri. Hii itarahisisha usimamizi wa utendaji kwa maana Waziri au Katibu Mkuu atajifunga yeye mwenyewe kimaandishi na ataweka saini yake kwenye vigezo ambavyo atapimwa navyo na wananchi mtashuhudia matokeo ya upimaji huo.
Ndugu Wananchi;
Ili kuweza kuratibu vyema shughuli za ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mfumo huu mpya, nimeunda chombo maalum kitakachokuwa chini ya Ofisi yangu ambacho kitajulikana kama President’s Delivery Bureau (PDB). Kazi zake za msingi zitakuwa ni pamoja na: kupanga na kuendesha shughuli za uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs); kuandaa mikataba ya kupima utendaji kazi wa Mawaziri kwenye miradi na programu za maendeleo katika wizara zao; kwa kushirikiana na Tume ya Mipango kuishauri Serikali kuhusu maeneo machache ya kipaumbele yenye kuleta matokeo ya haraka (National Key Results Areas); kusaidia sekta binafsi kuwekeza kwenye maeneo hayo; na kufanya tathmini huru ya utendaji kwa viongozi wote hususan Mawaziri katika utekelezaji wa maeneo muhimu ya kitaifa.
Ndugu Wananchi;
Tumefanya kazi kubwa sana ya kuandaa na kuainisha maeneo ya kimkakati na kuyaandalia programu za kina kwa ajili ya utekelezaji. Lakini tumeona ni vyema kuwashirikisha wadau na wananchi katika jambo hili kubwa.  Ndio maana tupo hapa kuhakikisha kuwa wananchi kwa ujumla wenu mnapata fursa ya kuchangia katika miradi na programu hizo kwa maendeleo ya taifa letu na watu wake.
Ndugu Zangu;
Sitapenda kuongea sana hivyo basi nataka niwape nafasi wananchi na wadau wengine mliofika hapa kupita katika eneo la kila maabara na kupata maelezo ya kina kutoka kwa wataalam.  Muwe huru kuuliza maswali, kujenga hoja, kutoa maoni na kukosoa na kuboresha katika kila maabara. Baada ya kupata maoni yenu ndipo tutaboresha na kwenda kuyafanyia kazi maoni na ushauri wenu.  
Ndugu Wananchi;
Baada ya kusema hayo, napenda kutamka kuwa Warsha ya Wazi imefunguliwa rasmi.  Ninawatakia majadiliano mazuri na uchangiaji mzuri.
Asanteni kwa kunisikiliza

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO

MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) leo katika ukumbi wa White House mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein na wengine kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu imemteua mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chambani, Pemba Mattr Said .(Picha na Bashir Nkoromo).

Rais Kikwete akutana na Mwenyekiti wa Direct AID Charity Organisation ya Kuwait

8E9U4408Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Dkt.Abdul RahmanAl Muhailan ambaye ni mwenyekiti wa asasi ya Direct AID Charity Organisation leo8E9U4423Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Dkt.Abdul RahmanAl Muhailan ambaye ni mwenyekiti wa asasi ya Direct AID Charity Organisation leo.8E9U4436Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Dkt.Abdul RahmanAl Muhailan ambaye ni mwenyekiti wa asasi ya Direct AID Charity Organisation mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam leo.picha na Freddy Maro,Ikulu.

Rais Kikwete afungua mkutano wa Maendeleo ya Kilimo Barani Afrika

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa kuzungumzia Mustakabali wa maendeleo ya Wakulima Barani Afrika uliofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo.mkutano huo umeandaliwa na asasi ya(The southern African Confederation of Agriculktural Unions(SACAU).Wapili kushoto ni Kaimu Rais wa SACAU Bwana Ishmael Sunga na Watatu kushoto ni Waziri wa Kilimo Christopher Chiza.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Mkutano utakaojadili Mustakabali wa Maendeleo ya Wakulima Barani Afrika uliofanyika katika hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam ambao umendaliwa na asasi ya SACAU(The Southern African Confederation of Agricultural Unions).(picha na Freddy Maro).

RAIS KIKWETE AZINDUA KITUO CHA TAASISI YA KIMATAIFA YA KILIMO CHA KITROPIKI (IITA) DAR ES SALAAM

Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chifu Olesegun Obasanjo akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa wakionja mikate iliyotengenezwa kwa unga wa muhogo wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mazungumzo na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo baada ya uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa
wakisikiliza maelezo ya kitaalamu juu ya utafiti wa maradhi ya migomba toka kwa Profesa Rony Swennen wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakiangalia mashine ya kuvunia mihogo
Wadau wakionja vyakula mbalimbali vinavyotengenezwa kwa unga wa muhogo
Wadau wakiwa katika sherehe hizo
Mmoja wa watafiti akielezea kazi yake kituoni hapo
Watafiti wakielezea kazi zao
Wadau wa ITTA ambao ni wapenzi wa Globu ya Jamii
Wadau shereheni
Wageni waalikwa
 
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakifungua kituo hicho
Rais Dkt. Jakaya Kikwete achunguza kitu kwa kutumia kifaa cha kisayansi katika taasisi hiyo.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Benjamin Mkapa pamona na Balozi wa Marekani nchini Tanzania wakiagalia sehemu ya vifaa vya kisayansi katika taasisi hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo wakifungua kituo hicho
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo pamoja na Rais Mstaafu,Mh. Benjamin Mkapa wakizindua rasmi jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.
Picha ya pamoja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Rais mstaafu wa Nigeria na Balozi wa heshima wa IITA Chief Olesegun Obasanjo baada ya uzinduzi wa jengo la sayansi katika kituo cha Taasisi ya Kimataiafa ya Kilimo cha Tropiki (IITA) Mikocheni jijini Dar es salaam leo Mei 13, 2013.

RAIS KIKWETE AREJEA TOKA AFRIKA KUSINI LEO

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymon Moshi mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 11, 2013 akitokea Cape Town, Afrika ya Kusini, alikohudhuria mkutano wa nchi SADC.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali (kulia) mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 11, 2013 akitokea Cape Town, Afrika ya Kusini, alikohudhuria mkutano wa nchi SADC.PICHA NA IKULU

Rais Kikwete ahudhuria kikao cha SADC jijini CAPE TOWN

Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(Watatu kushoto) akiongoza kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya SADC kilichofanyika jijini Cape Town Afrika ya Kusini leo.Wengine katika picha ni wajumbe wa kamati hiyo akiwemo mwenyeji Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini(kulia),Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Namibia Bibi Netumbo Nandi-Ndaitwa(kushoto) na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dkt.Tomaz Salomao.
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Dkt.Tomaz Salomao mjini Cape Town Afrika ya Kusini leo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakitoka katika ukumbi wa hoteli ya Westin jijini Cape Town Afrika ya Kusini mara baada ya kumalizika kwa kikao maalum cha Kamati ya Ulinzi na Usalma ya SADc kilichofanyika leo.Rais Kikwete alikuwa nchini Afrika ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mkurugenzi Mtendaji na mratibu wa asasi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bwana Mark Suzman jijini Cape Town Afrika ya Kusini.Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Adam Malima.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagana na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Misaada la Marekani USAID Dkt. Rajiv Shah muda mfupi baada ya kufanya naye mazungumzo katika ukumbi wa Cape Town Convention Centre jana.Picha na Freddy Maro.

Rais Kikwete awasili nchini Afrika Kusini kuhudhilia kikao cha viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Cape Town, Afrika ya Kusini kuhudhuria kikao cha viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika leo tarehe 10 Mei, 2013.
 
Viongozi wa SADC wanakutana chini ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo Tanzania ndiye mwenyekiti. 
 
Kikao cha leo kinatarajia kuzungumzia maendeleo na hali ya usalama katika ukanda huu hususan hali ya usalama Mashariki mwa Kongo, DRC, Madagascar na Zimbabwe.
 
Nchi za Afrika ya Kusini, Malawi na Tanzania zitapeleka vikosi Mashariki mwa DRC kulinda na kuleta utulivu na usalama. 
 
Kuhusu Madagascar, nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi Julai, 2013 wakati nchini Zimbabwe nako uchaguzi unatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu. 
 
Mbali na mkutano huo Rais anahudhuria mikutano kadhaa inayoendelea mjini Capetown ukiwemo ule wa Kiuchumi ambao viongozi wa kisiasa, kiserikali na wakubwa wa mashirika binafsi wanahudhuria na kuzungumzia fursa za kibiashara na kiuchumi barani Afrika. 
 
Rais anatarajia kurejea Dar es Salaam kesho tarehe 11 Mei, 2013
 
“Mwisho”
 
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Cape Town – Afrika ya Kusini
10 Mei, 2013

Rais Kikwete awatkaa wanajeshi wanaokwenda DRC,kuilinda heshima ya Tanzania

 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
 
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtakia kila la heri kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
PICHA NA IKULU.
 
Wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wametakiwa kudumisha utamaduni wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani kwa kuifanya kazi hiyo kwa heshima, nidhamu na utii ili kulinda heshima yao wenyewe na ile ya Tanzania.
 
Askari hao wamekumbushwa utamaduni huo wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikuwa akiwaaga wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa katika DRC katika hafla iliyofanyika leo, Jumatano, Mei 8, 2012, kwenye Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu la Tanzania yaliyoko Msangani, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.
 
Akizungumza na askari hao, Rais Kikwete amewaambia kuwa hana wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kutelekeza majukumu yao yanayowapeleka DRC isipokuwa tu kwamba waifanye kazi hiyo vizuri na kulingana na utamaduni wa majeshi ya kulinda amani ya Tanzania katika sehemu mbali mbali duniani.
 
“Tunakwenda kutelekeza majukumu ya Umoja wa Mataifa, sina shaka kuwa majukumu yenu mnayaelewa vizuri. Kazi yetu ni kulinda amani na wala hatuendi kupigana na yoyote. Kazi ya kijeshi mnaijua vizuri vile vile na kwa hili pia sina wasiwasi hata kidogo,” amesema Amiri Jeshi Mkuu na kuongeza:
 
“Kubwa ambalo lazima tulikumbuke ni kwamba nchi yetu kila ilikopeleka majeshi ya kulinda amani imejenga utamaduni wa pekee. Imejenga utamaduni wa askari wetu kuifanya kazi ya kulinda amani kwa heshima, kwa nidhamu na kwa utii wa kiwango cha juu. Hii ni heshima kwetu binafsi na heshima kwa taifa letu. Nawashukuruni na nawatakie kila la heri”
 
Kama ishara ya kuagana na askari hao, Rais na Amiri Jeshi Mkuu amemkabidhi Bendera ya Taifa Luteni Kanali Orestess Cassian Komba, Kamanda wa Kikosi cha Tanzania katika DRC ambacho kitajulikana kwa jina la TANZBATT 1-DRC, akimwambia “Bendera na Ikapepee”.
 
Katika jukumu la kulinda amani Mashariki mwa DRC, Kikosi cha Tanzania chenye askari 1281, kitajiunga na vikosi vya Malawi na Afrika Kusini ambavyo vyote vitakuwa chini ya Kamanda wa Brigedi hiyo, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa wa Tanzania pia. Kundi la kwanza la askari hao Tanzania linaondoka nchini kesho.
 
Majeshi hayo ya Tanzania yatalinda amani katika DRC chini ya Azimio Nambari 2098 (2013) la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2013

RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa pole kwa watawa wa kanisa hilo wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.
Wananchi wakimuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kumtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa kijana James Gabriel (16) aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Joachim Assey (aliyekaa kushoto kwake) wakati akihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.
Mama Salma Kikwete akipungia wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha Mei 7, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti Jumapili iliyopita.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013. PICHA NA IKULU.

Mama Kikwete akiomba kituo cha watoto wenye utindio wa ubongo kushirikiana na Tanzania kutoa mafunzo kwa watoto hao

Na Anna Nkinda – Kuwait Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa Ubongo kilichopo nchini Kuwait kushirikina na Tanzania ili waweze kufanya kazi kwa pamoja ya kuwasaidia na kutoa mafunzo kwa watoto wenye matatizo kama hayo waliopo nchini.
Mama Kikwete alilitoa ombi hilo jana alipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kuona jinsi wanavyotoa mafunzo kwa watoto hao ambayo yameweza kuwabadilisha akili zao na kuwa sawa na za watu wengine.
Alisema kuwa watoto wenye mtindio wa ubongo hata nchini wapo na wanapata mafunzo katika vituo vichache zilivyopo lakini kama watashirikiana kwa pamoja wataweza kubadilishana ujuzi ambao utawasaidia kutoa mafunzo mazuri zaidi kwa watoto hao.
 
“Ninawapongeza kwa kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kutoa mafunzo kwa watoto hawa kwani ni jambo jema kuwasaidia watu wenye matatizo.
 
“Watoto hawa wakipewa mafunzo akili yao itakuwa sawa na watu wengine, wakiwa wakubwa na kufikia umri wa kujitegemea wataweza kufanya kazi mbalimbali za maendeleo ambazo zitawaingizia kipato na kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Samira Al-Saad alisema kuwa kama watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo watapelekwa shule mapema zinazotoa mafunzo kwa ajili yao watapona na kuwa na akili sawa na watu wengine.
Dk. Samira alisema kuwa wazazi wengi hawajui kwamba matatizo ya mtindio wa ubongo yanatibika kama mtoto akipewa elimu ya darasani na kufanyishwa mazoezi ambayo yatamsaidia kufanya shughuli zake mwenyewe bila ya kutegemea msaada wa jamaa zao.
“Kituo hiki kilifunguliwa mwaka 1994 na hadi sasa kina wanafunzi 120 ambao wanapata mafunzo ya nadharia na vitendo na kinajiendesha kwa kupata msaada kutoa Serikalini, watu na mashirika binafsi ya ndani na nje ya nchi”, alisema Dk. Samira.
Aliendelea kusema kuwa umri wa watoto wa kuanza masomo ni miaka sita hadi 15 na kama mwanafunzi atakuwa amevuka miaka 15 atajifunza zaidi mafunzo ya vitendo ambayo yatamuwezesha kujitegemea hapo baadaye.
Dk. Samira alisema, “Wanafunzi wetu wameweza kupata ajira sehemu mbalimbali hii ni baada ya kupata mafunzo ambayo yamewafanya kuwa na akili sawa na watu wengine ambao hawana matatizo haya, kuna baadhi yao tumewaajiri hapa na hivi sasa wanawafundisha wanafunzi wenzao.
Mama Kikwete pia alitembelea Kituo cha Al-Kharafi ambacho kinatoa huduma ya mazoezi kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubungo na kuona jinsi watoto hao wanavyofanya mazoezi yao.
 
Kituo hicho kinapokea watoto wenye umri wa kuanzia miaka minne hadi 12 ambao wanafanya mazoezi kwa kucheza michezo mbalimbali ambayo inawabadilisha akili zao na kuwa katika hali ya kawaida .
 
Akiwa katika kituo hicho alijionea kazi mbalimbali zinazofanywa na watoto hao ambazo ni uchoraji, ushonaji, upishi pia aliona michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyimbo na maonyesho ya mavazi.Mama Kikwete aliambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Kuwait kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YA NCHINI KUWAIT

New Picture (9)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.

Rais Kikwete jana alitoa taarifa rasmi ya kulaani kitendo hicho cha kigaidi. Taarifa kamili ni kama ifuatayo:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha. Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa. Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.
Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili. Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma. Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.
Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.

TAMKO LA RAIS KIKWETE JUU YA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha. Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa. Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.
Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili.
Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma. Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.
Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.
 
Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
5 Mei, 2013

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI NCHINI KUWAIT LEO

k1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.
k2Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakipokea mashada ya mauwa alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.k3k4k5
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah wakiingia sehemu ya mapokezi na kukagua gwaride rasmi mara tu alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.k6k7
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mtawala wa Dola ya Kuwait Amiri Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-sabah katika mazungumzo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuwait City leo Mei 5, 2013 tayari kuanza ziara rasmi ya siku mbili katika nchi hiyo.PICHA NA IKULU

Rais Kikwete aongoza mazishi ya Marehemu Balozi Alfred Tandau

IMG_8950
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Waziri wa Zamani wa Kazi ,Marehemu Balozi Alfred Tandau wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Alfred Tandau ambaye alishika nyadhifa mbalimbali serikalini alifariki tarehe 30 Mwezi Aprili wiki iliyopita.
IMG_8988Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Mau katika kaburi la Marehemu Balozi Afred Tandau wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam leo jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa(picha na Ikulu)

RAIS KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS RAJOELINA WA MADAGASCAR

ra1

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mhe Andry Rajoelina wakati wa mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam Mei 3, 2013.

ra2
Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili mjini Dar Es Salaam jioni ya leo , Ijumaa Mei 3, 2013 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Amepokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar Es Salaam na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo baadaye leo Ikulu, Dar Es salaam.

Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa Asasi yaa Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Anakutana na Rais Rajoelina kwa mara ya tatu sasa, mara ya kwanza ikiwa ni mwezi Desemba mwaka jana, na baadaye mwezi Januari mwaka huu.

Rais Kikwete alipokutana mara ya mwisho na Rais huyo wa serikali ya mpito ya Madagascar alifanikiwa kumshawishi akubaliane na mapendekezo ya nchi za SADC kuwa asigombee kwenye uchaguzi mkuu utaofanyika mwaka huu kama njia ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Rais Kikwete awali ya hapo aliweza pia kumshawishi Rais wa zamani wa Madagascar Mhe Marc Ravalomanana asigombee katika uchaguzi mkuu huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WASHIKADAU WA SMART PARTNESHIP IKULU JIJINI DAR

sp2Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mkutano wa Smart Partnership Mei 3, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam. sp3Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washikadau toka katika mashirika binafsi na ya umma walioalikwa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya mkutano wa Smart Partnership Mei 3, 2013 Ikulu jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU.

Rais Kikwete apongeza wanabahari kwa kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Habari Duniani

Jakaya+Kikwete+Doug+Pitt+Named+Goodwill+Ambassador+VYq30mnJnaol
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewapongeza wanahabari ,wadau wa habari na Tasnia nzima ya habari nchini kwa kuadhimisha Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani (World Press Freedom Day) leo, Ijumaa, Mei 3, akiwahakikishia kuwa Serikali yake itaendelea kukuza, kulea, kulinda na kutetea Uhuru wa Habari ulioshamiri kwa kiwango cha juu kabisa nchini kwa sasa.
Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Serikali yake na yeye binafsi, kama mdau wa habari, wataendeleza kuelekeza nguvu kubwa katika kupanua Uhuru wa Habari kwa sababu uhuru huo ni kigezo muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Tanzania na katika kujenga na kupanua demokrasia nchini.
Katika salamu zake kwa wanahabari, wadau wa habari na Tasnia nzima ya habari nchini ambayo inasherehekea Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Dunia kitaifa mjini Arusha leo katika shughuli zilizoandaliwa na Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA), Tawi la Tanzania, Rais Kikwete amesema:
“Kama muumini na mdau wa Uhuru wa Habari ambao ni sehemu ya Uhuru Mpana Zaidi wa Kutoa Maoni (Freedom of Expression), napenda kuwapongezeni wanahabari wote nchini na wadau wenzenu duniani katika kusherehekea siku hii ya kuadhimisha Miaka 20 ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambayo kitaifa hapa kwetu inaadhimishwa na shughuli zilizoandaliwa na MISA-Tan mjini Arusha.”
Ameongeza Mheshimiwa Rais: “Sisi katika Tanzania tunayo kila sababu ya kusheherekea Siku hii ya leo ya Uhuru wa Habari nchini kwa sababu sote ni wadau wa habari ni mashahidi wa mafanikio makubwa na mengi katika nyanja ya habari katika miaka 20 iliyopita katika nchi yetu. Kwa sababu hiyo, naungana nanyi katika kusheherekea na kuadhimisha mafanikio haya makubwa.”
Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ambayo chimbuko lake ni Mkutano wa Waandishi wa Habari wa Afrika waliokutana na kutoa Tamko la Windhoek (Namibia) – the Windhoek Declaration on Promoting an Independent and Pluralistic African Press pamoja na kuanzisha Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika – Media institute of Southern Africa (MISA), Mei 3, mwaka 1991, ilichaguliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Uhuru Duniani mwaka 1993.
Amesisitiza Rais Kikwete: “Napenda kutumia Siku hii ya leo kuwapongezeni tena kwa kazi yenu nzuri ambayo imeendelea kuchangia maendeleo ya nchi yetu kupitia njia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha wananchi. Vile vile, napenda kutumia nafasi ya Siku ya leo kuwaelezeeni utayari wa Serikali yetu kuendelea kuithamini kazi hii nzuri. Ni matumaini yangu kuwa mtaendelea kuifanya kazi yenu kwa kuongozwa na misingi mikuu ya weledi wa taaluma ya uandishi wa habari.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Aidha, kama ambavyo tumekuwa tukifanya, napenda kuwahakikishieni kuwa mimi binafsi na Serikali ninayoingoza nitaendelea kushirikiana nanyi katika kupanua, kulea, kulinda na kutetea Uhuru wa Habari nchini ikiwa ni haki ya waandishi kufanya kazi yao kwa mazingira mwafaka ya kisiasa, kiuchumi, kisheria na kijamii. Vile vile, napenda kuwahakikisheni tutaendelea kushirikiana nanyi katika kulinda uhuru wa wapata habari nchini ambao ni muhimu kama ulivyo uhuru wa vyombo vya habari.”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE ALEXANDRE LEVEQUE LEO

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania Mhe Alexandre Leveque aliyemtembelea ofisini kwake Ikulu
jijini Dar es salaam leo asubuhi. Balozi Leveque aliongozana na Mkurugenzi Mwandamizi na Mkuu wa Ushirikiano wa Canadian International Development Agency (CIDA), Bi Patricia McCullagh. Wa pili kushoto ni
Balozi Dorah Msechu, Mkurugenzi katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa anayeshughulikia kurugenzi ya Nchi za Ulaya na Amerika, akifuatiwa na
ofisa dawati Bi Upendo Mwasha.
Picha na Ikulu

RAIS KIKWETE AFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU MZEE ALFRED TANDAU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa ameongozana na mke wake Mama Salma Kikwete, wakipokelwewa nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, na Mama Salma Kikwete, wakitambulishwa kwa watoto wa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau nyumbani kwa marehemu Magomeni jijini Dar es salaam walipofika kufariji wafiwa
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo.
Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezi nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma KLikwete wakiwafariji wafiwa nyumbani kwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwet akiwa na watoto wa marehemu Alfred Tandau. Kulia kwake ni Bw. Henry Tandau na kushoto kwake ni Bw Julius Tandau. Hapo nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Waziri wa zamani, Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mweka Hazina wa Taifa wa CCM wa zamani, Marehemu Alfred Tandau, aliyefariki dunia juzi jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya tumbo.PICHA NA IKULU

NEW PRESIDENT OF CHINA XI JINPING RECEIVES ROUSING WELCOME IN DAR ES SALAAM

 China’s new President Xi Jinping arrived in Tanzania today ahead of   a three-nation Africa tour also taking in South Africa and the Republic of the Congo. 
President Xi  flew into  Dar es Salaam with his wife from Moscow. After holding official talks scores of ministers and CEO of Chinese companies signed a totalo of 16  accords before the new President of China gave  a keynote speech on relations with Africa during a state banquet later on.


He is scheduled to head to Durban, South Africa, tomorrow  for a summit of leaders of the world’s major emerging economies, known as the BRICS, on Tuesday and Wednesday, and could endorse plans to create a joint foreign exchange reserves pool and an infrastructure.
 Banners with smiling faces of the two presidents
 Welcome to Tanzania a girl greets the President of China and his wife after she and the boy gave the visiting dignitaries bouquet of flowers
 President Jakaya Kikwete welcomes President Xi Jinping and his wife to Dar es salaam
 A warm welcome for President Xi Jinping at the Serena Inn in Dar es salaam
 President Xi Jinping’s motorcade arrives at the Eastern Gate of the State House 
 Guest and host work the crowd of hundreds of Dar es salaam residents
 The two Presidents wave to the huge crowd below
 Official talks

RAIS KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM, LEO

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013.
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Msanii Mrisho Mpoto akiburudisha wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim
wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali
za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi 16, 2013.
Seehemu ya wageni waalikwa na wanafunzi na wafanyakazi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, na viongozi wa hospitali ya Hubert Kairuki wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliozaliwa
katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita leo Machi 16, 2013.PICHA NA IKULU.

No comments: