Muungano wa Ulaya umetoa ripoti
kuonyesha kuwa zaidi ya robo ya wapenzi wa jinsia moja waliohojiwa
wameshambuliwa ama kutishwa katika miaka mitano iliyopita.
Ripoti hiyo iliandaliwa na wataalamu wa muungano huo kuboresha sera zinazoelekea kutenga watu kutokana na hulka zao za mapenzi.Na shuleni wanafunzi wawili kati ya watatu waliohojiwa walisema kuwa walificha kuwa wao ni wapenzi wa jinsia moja.
Kinachotia wasiwasi ni kuwa zaidi ya nusu yao hawako radhi kuripoti visa vya kushambuliwa kwa polisi kwa sababu wanaamini kuwa hakuna kitakachofanyika.
Wanasiasa na watunga sera mia tatu wanakutana Hague Uholanzi kujadili njia mpya za kuwalinda watu na kuhakikisha kuwa hawashambuliwi hata wakipendelea mapenzi ya jinsia moja.
No comments:
Post a Comment