Friday, May 17, 2013

Mtihani mgumu kwa Rais Kikwete huu hapa

 

Dar es Salaam. Kuna kila dalili kwamba wabunge wa CCM wameanza kupanga majeshi kwa lengo la ‘kumalizana’ watakapokutana kwa siku mbili mfululizo na mwenyekiti wa chama hicho tawala, Rais Jakaya Kikwete.

Mkutano huo unaotajwa kuwa zao la jitihada za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana unatarajiwa kufanyika kesho na keshokutwa mjini Dodoma, huku kukiwapo taarifa kwamba wabunge wamegawanyika katika makundi kwa lengo la kupenyeza, kisha kutetea hoja walizonazo dhidi ya wenzao.
Miongoni mwa hoja zinazotajwa ni ile ya kushughulikiwa kwa wabunge ambao wamekuwa wakitajwa kwamba ni wapinzani ndani ya CCM, wakiwamo, Alphaxard Kangi Lugora (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa), Ally Keissy Mohamed (Nkasi Kaskazini) na Luhaga Mpina (Kisesa).
Wabunge hao wanatuhumiwa na wenzao kwamba wanawasaidia wapinzani kutokana na misimamo yao ya kuikosoa hadharani Serikali katika vikao na mikutano tofauti ya Bunge.
Itakumbukwa kuwa Aprili 25 mwaka huu baada ya kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji, wabunge wa CCM walikutana katika kikao cha dharura kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambako Lugola na Filikunjombe walishambuliwa kutokana na kile kilichodaiwa kwamba wamekuwa wakiidhalilisha Serikali ya CCM bungeni.

JUST IN: Askofu Mkuu Mstaafu Mtega azungumza na waandishi wa habari ... Alichokisema hiki hapa

 


 
 Baba Askofu Mstaafu Norbert Mtega, akijibu maswali ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma.
Picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi hao.(Picha na Juma Nyumayo)
--------------------------------------------------------- 

Na Nathan Mtega,Songea
 
 SIKU moja baada ya Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbet kutangaza kustaafu nafasi hiyo kauli ambayo ilizua maswali na mijadala mingi miongoni mwa waumini wa kanisaa katoliki nchini na wananchi kwa ujumla ameamua kuzungumza na waandishi wa habari mjini Songea kufafanua zaidi kuhusiana na uamuzi wake huo.
 
Alisema kuwa ni wazi kuwa uamuzi huo aliouchukua umewashitua wengi lakini amelazimika kufikia uamuzi huo kufuatia kukumbwa na matatizo ya kiafya yaliyojitokeza kwake katika siku za hivi karibuni ambayo hakuwahi kuyapata kwa miaka mingi ya maisha yake pamoja na utume.

Wanafunzi 15 wa sekondari wakamatwa ..... Sababu ya kukamatwa hii hapa

 

 
Na Brandy Nelson, Mwananchi

 Wanafunzi 15, wa Shule ya Sekondari ya Jumuiya ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe mkoani Mbeya , wanashikiliwa polisi kwa tuhuma za kuchoma moto bweni la wanafunzi wa kiume na kusababisha uharibifu wa mali mbalimbali.  
Aizungumzia tukio hilo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku shuleni hapo  na kwamba  wanafunzi hao walifikia hatua hiyo ya kuchoma moto bweni hilo, wakipinga kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wenzao watatu kwa utovu wa nidhamu. 
Aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu kuwa ni Joseph Robert (18), anayesoma kidato cha nne na Mwita Chacha (17) na anayesoma kidato cha tatu, wote wakazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam na Mwingine ni Daniel David (18), anayesoma kidato cha tatu ambaye ni mkazi wa Ipinda wilayani Kyela.

MATUKIO KATIKA PICHA YA KIKAO CHA TATHIMINI YA ELIMU WILAYA YA MBINGA

 

 BAADHI YA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA HIYO SENYI NGAGA(HAYUPO PICHANI) WAKATI WA KIKAO CHA TATHIMINI YA ELIMU KATIKA WILAYA HIYO AMBAPO IMEFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAURU KATIKA ELIMU YA MSINGI KUTOKA NAFSI YA TANO KIMKOA HADI YA TATU KATIKA MITIHANI YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI KWA MWAKA 2012/2013
 BAADHI YA WATENDAJI WA MITAA,KATA NA WAKUU WA SHULE WILAYA YA MBINGA WALIOHUDHURIA KIKAO CHA TAHIMINI YA ELIMU
 BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO YA MBINGA WAKIFUATILIA KWA MAKINI TAARIFA MBALIMBALI
 MKUU WA WILAYA YA MBINGA SENYI NGAGA AKIFUNGUA KIKAO CHA TATHIMINI YA ELIMU KATIKA WILAYA HIYO KILICHOFANYIKA MJINI HUMO

UZEMBE WA MAMA LISHE WASAABABISHA HASARA MKOANI SINGIDA.

 

KAMANDA wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) ofisini kwake kuhusiana na tukio la moto.
*********
Na Nathaniel Limu.
Vibanda vinne vya biashara vinavyozunguka soko kuu la Manyoni mjini mkoa wa Singida, vimeteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na mamalishe kusahau kuzima moto wakati akifunga biashara yake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela amesema mtu wa kwanza kuuona moto huo ulioanzia kwenye kibanda cha mama lishe, ni mlinzi wa soko hilo aliyejulikana kwa jina la Jotamu Daud.
Kamanda huyo amesema moto huo baada ya kupamba zaidi, ulihamia kwenye vibanda vingine vya maduka ya nguo na kuteketeza vibanda hivyo na mali yote iliyokuwa ndani.
Kamanda Kamwele ametoa wito kwa mamalishe na babalishe kuhakikisha wanazima majiko yao ya  moto  mara tu wanapomaliza kufanya biashara zao ili kuzuia uwezekano wa kuwaka wakati wao hawapo.

Waumini wengi wa kanisa katoliki jimbo kuu la Songea washitushwa na kujiuzulu kwa Askofu Mtega



 Waumini wa kiwa njia panda wakingoja kauli ya Uhakika kuhusu Mhashamu Norbet Mtega ni kweli Amestahafu ? 
 Mhashamu Askofu Norbeth Wendelin Mtega.
.....................................................
Na Nathan Mtega,Songea.

BAADHI ya waumini wa kanisa katoliki jimbo kuu la Songea  waishio katika  maeneo mbali mbali  mjini Songea mkoani Ruvuma wameonesha kushitushwa na taarifa zilizo patikana za kujiuzulu kwa kiongozi  mkuu wa jimbo kuu la Songea , Mhashamu Askofu Norbeth Wendelin Mtega.

Taarifa za kujiuzulu kwa kiongozi huyo zilipatikana jana  majira ya saa 7 mchana ambazo zilieleza kuwa Askofu Mtega alikuwa ametembelea abasia ya wabeneditini iliyopo  Hanga wilayani Namtumbo mkoani humo .

DK. MWAKYEMBE MAJI YAMFIKA SHINGONI, ABARIKI KUBINAFSISHWA KWA TRENI YA KUSAFIRISHIA ABIRIA DAR



BAADA ya Serikali kubuni na kufanikiwa kuanzisha na kuendesha usafiri wa treni jijini Dar es Salaam, sasa inajipanga kubinafsisha usafiri huo unaosaidia kupunguza msongamano. Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alisema hayo bungeni jana, wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
Alisema Serikali inakamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma hiyo jijini humo.
Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), ndiyo itakayokamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma hiyo, atakayetumia miundombinu ya reli iliyopo na vichwa vya treni na mabehewa maalumu ya usafiri katika miji.
Dk Mwakyembe alisema mwitikio wa wananchi kutumia huduma ya treni ya abiria, umekuwa mkubwa ikilinganishwa na uwezo wa kutoa huduma yenyewe, hususan nyakati za mahitaji makubwa ya usafiri.
Wingi wa abiria Kwa sasa kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, treni hiyo ya jijini Dar es Salaam, inabeba watu 14,000 kwa kila siku, sawa na zaidi ya daladala 467 zenye uwezo wa kubeba abiria 30 kila siku.

Breaking newzzz: Dr. Ferdinand Masau wa Tanzania Heart Institue afariki dunia

 



Dr-Ferdinand-Masau
Taarifa zilizotufikia zinasema muasisi wa hospitali ya moyo ya Tanzania Heart Institue Dr. Ferdinand Masau amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hata hivyo bado tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi juu ya msiba huo mkubwa kwa taifa kutokana na umuhimu wa Marehemu Dr. Ferdinand Masau, Tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata.
 
Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu Dr. Ferdinand Masau AMIN

KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA MAKAO MAKUU TANAPA

 


1
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi  akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA. Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Utumishi na utawala wa TANAPA Bi. Witness Shoo na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi. 2
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Hifadhi za Taifa (hawapo pichani) Arusha alipowatembelea na kuzungumza nao juu ya changamoto ya kukabiliana na vitendo vya ujangili nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi. 3 
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya Hifadhi za Taifa Arusha alipowatembelea na kuzungumza nao juu ya changamoto ya kukabiliana na vitendo vya ujangili nchini.

Tukio la bomu la Arusha latua UN



Tukio la kutupwa bomu katika Kanisa Katoliki la Joseph Mfanyakazi, Arusha limetua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) baada ya kuwasilishwa na Balozi wa Vatican UN, Askofu Mkuu Frances Chullikatt.
Askofu Chullikatt anakuwa kiongozi wa kwanza wa Vatican kutoa tamko kuhusiana na shambulizi hilo ambalo mmoja wa viongozi wake alikuwapo.
Bomu hilo lilirushwa katika kanisa hilo wakati likizinduliwa na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Francisco Padilla Mei 5, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watatu nakujeruhi zaidi ya 50.

BREAKING NEWSSSS: ..... MLINZI WA BAA ACHINJWA NA MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO


Mlinzi wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni mkoani hapa Bw Mika Athumani  amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.Habari zilizoptaikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi  hao baada ya kuvamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane  na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali mbali.
  Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili..


     Sehemu aliyochinjiwa mlinzi huyo aliyefahamika kwa jina Mika Athumani.
Akihojiwa mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema" inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"alisema Bw Mushi ambaye anadai bado hajafahami dhamani ya vitu vilivyoibikiwa na majambazi hayo.

MAMBO YANAZIDI KUNOGA .... DULLY SYKES KUPAMBA USIKU WA REDDS MISS MOSHI 2013 AVENTURE






Dully Sykes
Na Mwandishi Wetu, Moshi

MSANII wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Dully Sykes "mista Misifa" anatarajia kupanda
jukwaani kutumbuiza katika usiku wa Ulimbwende, usiku wa Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika May 18, katika ukumbi wa Aventure, Mjini Moshi.

Akizungumza mratibu wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa kampuni ya New Vision plan inayohusika na kazi za kuandaa mashindano ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya warembo19 watachuana kumsaka malkia wa Moshi wakisindikizwa na Prince Dully Sykes.

Moses alisema tayari maandalizi yameshaanza na mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote wameshaingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.

JASHO LA BINADAMU HUMVUTIA MBU WA MALARIA-UTAFITI

maisha_Mbu
1Lazima ulala kwa namna hiyo ili kuepuka kupata ugonjwa huu hatari zaidi duniani
Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Utafiti wa kisayansi umebaini kuwa mbu jike wanaoambukiza vijimelea vya ugonjwa wa  Malaria huvutiwa zaidi na harufu ya mwili wa binadamu kuliko wadudu wengine.
Watafiti waliochapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la Plos One, wanaamini kuwa Mbu wanaobeba viini vinavyosababisha Malaria, huwa na uwezo mkubwa wa kunusa.
Daktari James Logan, kutoka chuo cha mafunzo ya fya mjini London, anasema kuwa moja ya mambo ambayo humshangaza ni ambavyo viini vinakuwa na akili nyingi.
Anasema kuwa viini vinaonekana kuwa na akili nyingi kiasi cha kuwa mbele kwa fikira kuliko hata wanasayansi.
Katika kufanya utafiti wao, wanasayanyi waliwaambukiza Mmbu na viini hatari vya Plasmodium falciparum.
Waliwaweka Mmbu hao katika mkebe pamoja na soksi ilyoikuwa inavunda na ambayo ilikuwa imevaliwa kwa masaa ishirini. Mmbu hao walijazana kwenye soksi hiyo,Wanasayansi hao walifanya utafiti huo na Mmbu ambao walikuwa hawana viini hivyo.
Waligundua kuwa Mmbu waliokuwa na viini waliweza kuvutiwa zaidi na soski zilizokuwa na uvundo.
Wanasayansi wanaamini kuwa Mmbu waliokuwa na viini wanakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kunusa kwa sababu viini ndivyo vinawawezesha kunusa zaidi.
Kwa Mbu, binadamu anakuwa rahisi kushambulia kwa sababu ya harufu ya mwili wake na kisha viini hivyo ninavamia damu yake kuhakikisha kuwa vinaendelea kuzaana.
Watafiti hao sasa watafanya utafiti wa miaka mitatu kutaka kujua ni vipi viini vina uwezo wa kufanya hivyo.
Daktari Logan , anasema kuwa ikiwa wataweza kujua viini vinavyosababisha Malaria, itawasaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Kulingana na takwimu za hivi karibuni, shirika la afya duniani linasema kuwa mnamo mwaka 2012, takriban watu milioni 219 waliugua Malaria huku wengine 660,000 wakiripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo.
Afrika ndilo bara lenye visa vingi vya watu kuugua Malaria na asilimia tisini ya vifo vinavyotokana na Malaria hutokea barani humo.

JAJI MKUU WA TANZANIA AELEZA MIKAKATI YA KUBORESHA MAHAKAMA KUU NCHINI



Jaji  mku wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande
............................................... 
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
JAJI mkuu wa Tanzania Mohamed Chande  amesema kuwa mahakama  kuu Tanzania inaendelea na mkakati endelevu wa miaka 2 utakao husisha unoreshajki wa miundombinu ya mahakama za ngazi zote nchini kutoa elimu ya kujiendeleza kwa watumishi wake na pia kuzitolea uamuzi kesi zote zilizochukua mda mrefu.
Jaji mkuu  Mohamed Chande  aliyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya siku ya kwanza ya kukagua maendeleo ya utendaji haki kwa mahakam ya mikoa ya Rukwa na Katavi.
Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed alisema kuwa utekelezaji wa mkakati huo ni moja ya miundombinu za kuondoa usumbufu wanaoupata wananchi wakati wa uendeshaji wa kesi zao na pia kuondoa lawama za muda mrefu za uwajibikaji mdogo na vitendo vya rushwa.
Akiongea na watumishi wa mahakama hizo za hakimu mkazi wilaya na mkoa na baadae watumishi wa mahakama kuu kanda ya sumbawanga alidai kuwa zaidi ya shilingi bilioni 10 zinategemewa ku[itishwa katika mwaka huu wa fedha wa utekelezaji mkakati.
Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Manase Goroba alisema kumekuwepo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hasa ya wapiga chapa ikiwamo ya uchakavu wa majengo mengi ambayo yanahitaji ukarabati mkubwa katika mahakama


Alisema kuwa kumekuwepo na mahakama mpya ambazo ni zilijengwa kwa nguvu za wananchi na bado majengo hayo hajakamilika hivyo kunahitaji fedha kwa ajili ya umaliziaji wa majengo hayo.
Mustafa sijani ni hakimu wa mwanzo wa wilaya walimweleza jaji mkuu kuwa adha zinazowakabili watumishi wa mahakama katika utendaji wa kazi ni pamoja na uhaba wa watumishi vitendea kazi

MANUMBA AREJEA KAZINI RASMI

 


Hatimaye hali ya afya ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini, Robert Manumba(Pichani juu), imeimarika na amerejea kazini, limeandika Mwananchi Akizungumza kwa njia ya simu, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alikiri kuwa Manumba amereje kazi ingawa hakuwa tayari kutaja tarehe aliyoingia kazini.“ Eh! Unauliza nini, mbona ameanza kazi siku nyingi, siwezi kukumbuka tarehe sipo ofisini naelekea kwenye kikao cha kazi,” alisema Senso.Habari za kuaminika kutoka kwa baadhi ya maofisa wa kitengo cha upelelezi, zilisema kiongozi huyo ameshaanza kazi baada ya afya yake kutengemaa.Manumba mwenyewe, kifupi alisema “Kwa sasa sijambo, ninakwenda kwenye mkutano.” Mkurugenzi huyo alirejea nchini April 22, mwaka huu akitokea Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Millpark.
Amekuwa katika hospitali hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, kuanzia Januari 26, mwaka huu akisumbuliwa na malaria.

MKUU WA GENGE LA MATAPELI WANAOJIFANYA MAAFISA WA TAKUKURU ANASWA JIJINI MWANZA, ALIKUWA AKITUMIA HIRIZI KUFANIKISHA WIZI

 



Mtuhumiwa Simon Jumbe anayetajwa kujifanya afisa wa Takukuru.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kumnasa mtu mmoja ambaye anasadikika kuwa mkuu wa genge la watu wanaojifanya Maafisa wa Ofisi ya TAKUKURU Mkoani hapa.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Ayubu Akida alisema kwamba kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Simon Jumbe (32) lakini amekuwa akitumia majina mengie kwa kujiita Mapunda na SP ni kutokana na mtego uliowekwa na maafisa wake.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.
“Tuliweka mtego huo kutokana na kuwepo taarifa za siri kutoka kwa raia wema ambapo walitueleza kwamba kuna wimbi la baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwadanganya watu kuwa wao ni maafisa na watumishi wa TAKUKURU baada ya kuweka mtego Mei 13 mwaka huu tumefanikiwa kumnasa huyu maeneo ya Kata ya Mkuyuni Wilayani Nyamagana” alisema Akida.

NAOMBA NIYAWASILISHE MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 17.05.2013



DSC 0230 cd07d

KOCHA WA TAIFA STARS KIM POULSEN ATAJA 26 WA STARS KUIVAA MOROCCO


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.
Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.
Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.
Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).

UJENZI WA KITUO CHA SIKOSELI WAPIGWA JEKI

 

 Mwenyekiti wa  Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (kulia) akisalimiana na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.   Wengine ni baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.
 Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Mhe. Abdallah Mwinyi (kuli) akisalimiana na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.   Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Grace Rubambey.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya ugonjwa wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey  (kulia) akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia walikuwa wakimkaribisha mwendesha baiskeli Alan Knight (wa tatu kushoto), ambaye hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

No comments: