Friday, May 17, 2013

Polisi mstaafu amcharanga mapanga mwanae wa miaka 4 [TAHADHARI: Picha za kukwaza]

Tukio hilo limetokea leo jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness Elius (28) huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.
Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango. 
Madaktari na wauguzi wakimhudumia mtoto huyo
Madaktari na wauguzi wakimhudumia mtoto huyo


polisi-amcharanga-mapanga-mwanae-miaka-4-picha-2

Mtuhumiwa akiwa hoi hospitalini baada ya kupokea kichapo kutoka kwa majirani wenye hasira
Mtuhumiwa akiwa hoi hospitalini baada ya kupokea kichapo kutoka kwa majirani wenye hasira


polisi-amcharanga-mapanga-mwanae-miaka-4-picha-0
Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Advertisement

No comments: