Friday, May 3, 2013

PICHA ZA POLISI ALIEPIGWA RISASI NJE YA UKUMBI ALIPOKUA ANAAPISHWA WAZIRI WA KWANZA MWEUSI NCHINI ITALIA

.
.
Ripota wa nguvu Michael Minja kutoka nchini Italia, anaripoti kwamba baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kwa Waziri mwenye asili ya Kiafrika kwenye historia ya Italia ambae ni CECILE KYENGE KASHETU kutokea Congo DRC, alijitokeza mwanaume mmoja na kuwapiga risasi polisi wawili waliokuwemo nje ya Ukumbi walikokua wanaapishwa Mawaziri wapya Ikulu.

Mtu mmoja alijotokeza na kuwashambulia Polisi kwa kuwapiga Risasi wakati wakiwa wanaendeleza ulinzi katika eneo hilo ambapo Polisi mmoja alijeruhiwa vibaya kwa risasi shingoni lakini hakupoteza maisha.
Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi ambapo habari zisizo rasmi zimeeleza kwamba kuna uwezekano alikua na matatizo ya akili au uamuzi huo unahusika na ubaguzi wa rangi baada ya kuteuliwa kwa Waziri mpya wa mambo ya nje ambae ni Mweusi.
.
.
.
.
.
Huyu ndio Waziri wa kwanza mweusi kwenye historia ya Italia, aliolewa na Muitaliano miaka mingi iliyopita na kuhamia pamoja na kuchukua uraia wa Italia mwaka 1983.

No comments: