Ulinzi umeimarishwa kila kona
Hali ya usalama ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni tete. Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi. Usafiri wa Pikipiki unapatikana katika baadhi ya maeneo machache ya mji, huku maneo makuu ya biashara yakiwa wazi bila ya pilikapilika za watu kama ilivyo kawaida.
Polisi
wakiwa kwenye magari wameonekana katika maeneo mbalimbali ya mji, na
wengine kuweka makambi madogo katika maeneo yanayoaminika kuwa na
msongamano wa watu katika siku za kawaida.
Mwandishi
huyu ameshuhudia magari ya polisi yakiwa na askari katika maeneo ya
Bima, Soko kuu ambako pia kulikuwa na gari la kumwaga maji ya kuwasha,
Magomeni, Skoya na Majengo.
Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi.
MWANDISHI CHARLES MULINDA AJITOA JUKWAA LA WAHARIRI .... SABABU ZA KUFANYA HIVYO HIZI HAPA
Charles Mullinda
Mhariri Mtanzania Jumatano
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la WahaririYAH: KUJITOA KWENYE
JUKWAANapenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la
Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.Nimeamua
kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru
wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini
hayapaswi kufumbiwa macho.
Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi
ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano
yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.Aidha,
siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri
wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande
mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya
wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.
ZITTO KABWE AONGELEA KUHUSU KUBINAFSISHWA KWA RELI DSM
Zitto Kabwe
Ubinafsishaji
wa usafiri wa reli Dar Es salaam - uk. 24 wa hotuba ya Waziri Mwakyembe
" .... Wizara kupitia RAHCO itakamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji
na mwendeshaji wa huduma ya usafiri wa treni ya abiria katika jiji la
Dar Es Salaam atakayetumia miundombinu ya reli iliyopo....."
Ubinafsishaji wa usafiri wa reli Dar Es salaam - uk. 24 wa hotuba ya Waziri Mwakyembe " .... Wizara kupitia RAHCO itakamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma ya usafiri wa treni ya abiria katika jiji la Dar Es Salaam atakayetumia miundombinu ya reli iliyopo....."
Kwa nini serikali haikuanza Kwa kuwa na Shirika la Reli Dar Es Salaam
kabla ya kwenda kwenye ubinafsishaji? .Tumeshafanya tathmini ya
ubinafsishaji wa awali wa usafiri wa reli nchini? Tumejifunza nini?
TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU (TFF)
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu
(2012/2013) inafikia tamati kesho (Mei 18 mwaka huu) kwa timu zote 14
kupambana katika viwanja saba tofauti.
Mechi
zote zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Ni jukumu la kamishna wa
mechi husika kuhakikisha mchezo unaanza katika muda uliopangwa,
vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi
Kuu ya Vodacom toleo la 2012.
Yanga
ambayo tayari imeshatwaa ubingwa itakuwa mgeni wa Simba katika mechi
namba 180 itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo mwamuzi
atakuwa Martin Saanya kutoka Morogoro na Kamishna ni Emmanuel Kavenga wa
Mbeya.
Mgambo
Shooting vs African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Mwamuzi ni Amon
Paul wa Mara wakati Kamishna ni Ally Mkomwa kutoka Pwani), JKT Ruvu vs
Mtibwa Sugar (Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mwamuzi ni Israel
Mujuni wa Dar es Salaam wakati Kamishna ni Salum Kikwamba kutoka
Kilimanjaro).
Tanzania
Prisons vs Kagera Sugar (Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Mwamuzi ni Ibrahim
Kidiwa wa Tanga wakati Kamishna ni John Kiteve kutoka Iringa), Oljoro
JKT vs Azam (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha. Mwamuzi ni
Athuman Lazi wa Morogoro wakati Kamishna ni Juma Mgunda kutoka Tanga).
Uwanja
wa Jamhuri, mjini Morogoro utatumika kwa mechi kati ya Polisi Morogoro
na Coastal Union ya Tanga ambapo Mwamuzi atakuwa Said Ndege wa Dar es
Salaam wakati Kamishna ni Hakim Byemba kutoka Dodoma. Toto Africans
itacheza na Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
ambapo mwamuzi ni Geoffrey Tumaini kutoka Dar es Salaam na Kamishna ni
Josephat Magazi wa Singida.
MECHI ZA MARUDIANO RCL WIKIENDI HII
Tamko la Wizara kuhusu habari ya Nipashe “Aibu kwa profesa Maghembe ....
JAMHURI YA MUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAJI
TAARIFA KWA UMMA
Katika
gazeti la Nipashe la Jumapili tarehe 12 Mei 2013 mwandishi Mshaka Mgeta
aliandika makala yenye kichwa cha habari “Aibu kwa Profesa Maghembe
na dharau kwa wataalamu wa Wizara” na kuwa, Wizara ya Maji imejiwekea
rekodi chafu kwa bajeti yake kurejeshwa kabla ya kupitishwa na Bunge na
wataalamuwa wa Wizara ya Maji wamekuwa miongoni mwa wasiosikilizwa na
kupuuzwa suala hilo si la kweli.
Mnano tarehe 24 na 25 Aprili, 2013, Waziri wa Maji Mhe. Prof. Jumanne Abdallah Maghembe (MB) aliwasilisha Bungeni Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2013/2014.
Bajeti hiyo iliwasilishwa na mjadala uliendelea kwa muda wa Siku mbili. Mjadala mkubwa ulikuwa Bungeni baada ya
Mnano tarehe 24 na 25 Aprili, 2013, Waziri wa Maji Mhe. Prof. Jumanne Abdallah Maghembe (MB) aliwasilisha Bungeni Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2013/2014.
Bajeti hiyo iliwasilishwa na mjadala uliendelea kwa muda wa Siku mbili. Mjadala mkubwa ulikuwa Bungeni baada ya
kuwasilisha maoni ya Kamati ya kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji kuwa Bajeti ya Wizara ya Maji haitoshi.
Mjadala ulihairishwa na Mhe. Spika chini ya Kanuni ya Bunge 67(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kama Ibara ya 89(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 2 Toleo la 2002. Wakati huo, Bunge halikuulizwa kama linakubali au kukataa Bajeti ya Wizara ya Maji.
Mjadala ulihairishwa na Mhe. Spika chini ya Kanuni ya Bunge 67(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge kama Ibara ya 89(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sura ya 2 Toleo la 2002. Wakati huo, Bunge halikuulizwa kama linakubali au kukataa Bajeti ya Wizara ya Maji.
MAMA PINDA: TUMUOMBE MUNGU YASITOKEE MABOMU MENGINE
Mama
Tunu Pinda akiwa anaonyweshwa na Paroko Peddy Castellino mahali Bomu
lilipo angukia na kusababisha maafa na majeruhi katika kanisa Katoliki
Parokia ya Olasiti mkoani Arusha katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na
Katiba Angela Kairuki kulia kwa Mama Pinda ni Mkuu wa Wilaya Arusha Jonh
Mongela picha na Chris Mfinanga
Mama
Tunu Pinda akiwa na viongozi wa parokia ya Olasiti wakiwaombea Marehemu
walio fariki kutokana na Bomu lililo tupwa katika kanisa Katoliki
parokkia ya Olasiti Mkoani Arusha marehemu hao wamezikwa katika eneo la
Kanisa mahali Bomu lilipo tupiwa Picha na Chris Mfinanga
Mama
Tunu Pinda akiwa anampa pole Bibi Consesa Mbaga (43) ambaye nimiongoni
wa majeruhi walio lazwa katika Hospitali ya Maunt Meru kutkana na
majeraha ya bomu iliotokea katika Kanisa la Katoliki Parokia ya Olastiti
na kusababisha vifo na majeruhi picha na Chris Mfinanga
Dk Shein akutana na balozi wa Indonesia leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania <ke Zakaria Anshar,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais leo asubuhi
No comments:
Post a Comment