UZEMBE WA MAMA LISHE WASAABABISHA HASARA MKOANI SINGIDA.
KAMANDA
wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akizungumza na waandishi
wa habari(hawapo pichani) ofisini kwake kuhusiana na tukio la moto.
*********
Na Nathaniel Limu.
Vibanda
vinne vya biashara vinavyozunguka soko kuu la Manyoni mjini mkoa wa
Singida, vimeteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na mamalishe
kusahau kuzima moto wakati akifunga biashara yake.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela amesema mtu wa kwanza
kuuona moto huo ulioanzia kwenye kibanda cha mama lishe, ni mlinzi wa
soko hilo aliyejulikana kwa jina la Jotamu Daud.
Kamanda
huyo amesema moto huo baada ya kupamba zaidi, ulihamia kwenye vibanda
vingine vya maduka ya nguo na kuteketeza vibanda hivyo na mali yote
iliyokuwa ndani.
Kamanda
Kamwele ametoa wito kwa mamalishe na babalishe kuhakikisha wanazima
majiko yao ya moto mara tu wanapomaliza kufanya biashara zao ili
kuzuia uwezekano wa kuwaka wakati wao hawapo.
Waumini wengi wa kanisa katoliki jimbo kuu la Songea washitushwa na kujiuzulu kwa Askofu Mtega
Waumini wa kiwa njia panda wakingoja kauli ya Uhakika kuhusu Mhashamu Norbet Mtega ni kweli Amestahafu ?
Mhashamu Askofu Norbeth Wendelin Mtega.
.....................................................
Na Nathan Mtega,Songea.
BAADHI ya waumini wa kanisa katoliki jimbo kuu la Songea waishio katika
maeneo mbali mbali mjini Songea
mkoani Ruvuma wameonesha kushitushwa na taarifa zilizo patikana za kujiuzulu
kwa kiongozi mkuu wa jimbo kuu la Songea
, Mhashamu Askofu Norbeth Wendelin Mtega.
Taarifa za kujiuzulu kwa kiongozi huyo zilipatikana jana majira ya saa 7 mchana ambazo zilieleza kuwa
Askofu Mtega alikuwa ametembelea abasia ya wabeneditini iliyopo Hanga wilayani Namtumbo mkoani humo .
DK. MWAKYEMBE MAJI YAMFIKA SHINGONI, ABARIKI KUBINAFSISHWA KWA TRENI YA KUSAFIRISHIA ABIRIA DAR
BAADA ya Serikali kubuni na kufanikiwa
kuanzisha na kuendesha usafiri wa treni jijini Dar es Salaam, sasa
inajipanga kubinafsisha usafiri huo unaosaidia kupunguza msongamano.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, alisema hayo bungeni jana,
wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa
fedha 2013/2014.
Alisema Serikali inakamilisha mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma hiyo jijini humo.
Kwa mujibu wa Dk Mwakyembe, Kampuni
Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), ndiyo itakayokamilisha
mchakato wa kumpata mwekezaji na mwendeshaji wa huduma hiyo,
atakayetumia miundombinu ya reli iliyopo na vichwa vya treni na mabehewa
maalumu ya usafiri katika miji.
Dk Mwakyembe alisema mwitikio wa
wananchi kutumia huduma ya treni ya abiria, umekuwa mkubwa
ikilinganishwa na uwezo wa kutoa huduma yenyewe, hususan nyakati za
mahitaji makubwa ya usafiri.
Wingi wa abiria Kwa sasa kwa mujibu wa
Dk Mwakyembe, treni hiyo ya jijini Dar es Salaam, inabeba watu 14,000
kwa kila siku, sawa na zaidi ya daladala 467 zenye uwezo wa kubeba
abiria 30 kila siku.
Breaking newzzz: Dr. Ferdinand Masau wa Tanzania Heart Institue afariki dunia
Taarifa
zilizotufikia zinasema muasisi wa hospitali ya moyo ya Tanzania Heart
Institue Dr. Ferdinand Masau amefariki dunia usiku wa kuamkia leo hata
hivyo bado tunaendelea kufuatilia taarifa zaidi juu ya msiba huo mkubwa
kwa taifa kutokana na umuhimu wa Marehemu Dr. Ferdinand Masau, Tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata.
Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu Dr. Ferdinand Masau AMIN
KATIBU MKUU MALIASILI NA UTALII ATEMBELEA MAKAO MAKUU TANAPA
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akisaini kitabu
cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA. Aliyesimama ni
Mkurugenzi wa Utumishi na utawala wa TANAPA Bi. Witness Shoo na kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na
wafanyakazi wa Makao Makuu ya Hifadhi za Taifa (hawapo pichani) Arusha
alipowatembelea na kuzungumza nao juu ya changamoto ya kukabiliana na
vitendo vya ujangili nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan
Kijazi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi akizungumza na
wafanyakazi wa Makao Makuu ya Hifadhi za Taifa Arusha alipowatembelea na
kuzungumza nao juu ya changamoto ya kukabiliana na vitendo vya ujangili
nchini.
Tukio la bomu la Arusha latua UN
Tukio
la kutupwa bomu katika Kanisa Katoliki la Joseph Mfanyakazi, Arusha
limetua katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) baada ya
kuwasilishwa na Balozi wa Vatican UN, Askofu Mkuu Frances Chullikatt.
Askofu
Chullikatt anakuwa kiongozi wa kwanza wa Vatican kutoa tamko kuhusiana
na shambulizi hilo ambalo mmoja wa viongozi wake alikuwapo.
BREAKING NEWSSSS: ..... MLINZI WA BAA ACHINJWA NA MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO
Mlinzi
wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya
Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni mkoani hapa Bw
Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.Habari
zilizoptaikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi hao baada ya
kuvamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo
na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali
mbali.
Akihojiwa
mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai
kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadae
walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo
na kuiba vitu mbali mbali.Alipoulizwa
kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala
Bw Mushi alisema" inawezekana lakini
hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti
tukio hilo linatokea"alisema Bw Mushi ambaye anadai bado hajafahami
dhamani ya vitu vilivyoibikiwa na majambazi hayo.
MAMBO YANAZIDI KUNOGA .... DULLY SYKES KUPAMBA USIKU WA REDDS MISS MOSHI 2013 AVENTURE
Dully Sykes |
MSANII wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Fleva, Dully Sykes "mista Misifa" anatarajia kupanda jukwaani kutumbuiza katika usiku wa Ulimbwende, usiku wa Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika May 18, katika ukumbi wa Aventure, Mjini Moshi.
Akizungumza mratibu wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa kampuni ya New Vision plan inayohusika na kazi za kuandaa mashindano ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya warembo19 watachuana kumsaka malkia wa Moshi wakisindikizwa na Prince Dully Sykes.
Moses alisema tayari maandalizi yameshaanza na mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote wameshaingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.
JASHO LA BINADAMU HUMVUTIA MBU WA MALARIA-UTAFITI
Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Utafiti
wa kisayansi umebaini kuwa mbu jike wanaoambukiza vijimelea vya ugonjwa
wa Malaria huvutiwa zaidi na harufu ya mwili wa binadamu kuliko wadudu
wengine.
Watafiti
waliochapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la Plos One,
wanaamini kuwa Mbu wanaobeba viini vinavyosababisha Malaria, huwa na
uwezo mkubwa wa kunusa.
Daktari
James Logan, kutoka chuo cha mafunzo ya fya mjini London, anasema kuwa
moja ya mambo ambayo humshangaza ni ambavyo viini vinakuwa na akili
nyingi.
Anasema kuwa viini vinaonekana kuwa na akili nyingi kiasi cha kuwa mbele kwa fikira kuliko hata wanasayansi.
Katika kufanya utafiti wao, wanasayanyi waliwaambukiza Mmbu na viini hatari vya Plasmodium falciparum.
Waliwaweka
Mmbu hao katika mkebe pamoja na soksi ilyoikuwa inavunda na ambayo
ilikuwa imevaliwa kwa masaa ishirini. Mmbu hao walijazana kwenye soksi
hiyo,Wanasayansi hao walifanya utafiti huo na Mmbu ambao walikuwa hawana
viini hivyo.
Waligundua kuwa Mmbu waliokuwa na viini waliweza kuvutiwa zaidi na soski zilizokuwa na uvundo.
Wanasayansi
wanaamini kuwa Mmbu waliokuwa na viini wanakuwa na uwezo mkubwa zaidi
wa kunusa kwa sababu viini ndivyo vinawawezesha kunusa zaidi.
Kwa
Mbu, binadamu anakuwa rahisi kushambulia kwa sababu ya harufu ya mwili
wake na kisha viini hivyo ninavamia damu yake kuhakikisha kuwa
vinaendelea kuzaana.
Watafiti hao sasa watafanya utafiti wa miaka mitatu kutaka kujua ni vipi viini vina uwezo wa kufanya hivyo.
Daktari Logan , anasema kuwa ikiwa wataweza kujua viini vinavyosababisha Malaria, itawasaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria.
Kulingana
na takwimu za hivi karibuni, shirika la afya duniani linasema kuwa
mnamo mwaka 2012, takriban watu milioni 219 waliugua Malaria huku
wengine 660,000 wakiripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo.
Afrika
ndilo bara lenye visa vingi vya watu kuugua Malaria na asilimia tisini
ya vifo vinavyotokana na Malaria hutokea barani humo.
JAJI MKUU WA TANZANIA AELEZA MIKAKATI YA KUBORESHA MAHAKAMA KUU NCHINI
Jaji mku wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande
...............................................
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
Sumbawanga
JAJI mkuu wa
Tanzania Mohamed Chande amesema kuwa mahakama kuu Tanzania inaendelea
na mkakati endelevu wa miaka 2 utakao husisha unoreshajki wa
miundombinu ya mahakama za ngazi zote nchini kutoa elimu ya kujiendeleza
kwa watumishi wake na pia kuzitolea uamuzi kesi zote zilizochukua mda
mrefu.
Jaji mkuu Mohamed Chande aliyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya siku ya kwanza ya kukagua maendeleo ya utendaji haki kwa mahakam ya mikoa ya Rukwa na Katavi.
Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed alisema kuwa utekelezaji wa mkakati huo ni moja ya miundombinu za kuondoa usumbufu wanaoupata wananchi wakati wa uendeshaji wa kesi zao na pia kuondoa lawama za muda mrefu za uwajibikaji mdogo na vitendo vya rushwa.
Akiongea na watumishi wa mahakama hizo za hakimu mkazi wilaya na mkoa na baadae watumishi wa mahakama kuu kanda ya sumbawanga alidai kuwa zaidi ya shilingi bilioni 10 zinategemewa ku[itishwa katika mwaka huu wa fedha wa utekelezaji mkakati.
Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Manase Goroba alisema kumekuwepo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hasa ya wapiga chapa ikiwamo ya uchakavu wa majengo mengi ambayo yanahitaji ukarabati mkubwa katika mahakama
Alisema kuwa kumekuwepo na mahakama mpya ambazo ni zilijengwa kwa nguvu za wananchi na bado majengo hayo hajakamilika hivyo kunahitaji fedha kwa ajili ya umaliziaji wa majengo hayo.
Mustafa sijani ni hakimu wa mwanzo wa wilaya walimweleza jaji mkuu kuwa adha zinazowakabili watumishi wa mahakama katika utendaji wa kazi ni pamoja na uhaba wa watumishi vitendea kazi
Jaji mkuu Mohamed Chande aliyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya siku ya kwanza ya kukagua maendeleo ya utendaji haki kwa mahakam ya mikoa ya Rukwa na Katavi.
Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed alisema kuwa utekelezaji wa mkakati huo ni moja ya miundombinu za kuondoa usumbufu wanaoupata wananchi wakati wa uendeshaji wa kesi zao na pia kuondoa lawama za muda mrefu za uwajibikaji mdogo na vitendo vya rushwa.
Akiongea na watumishi wa mahakama hizo za hakimu mkazi wilaya na mkoa na baadae watumishi wa mahakama kuu kanda ya sumbawanga alidai kuwa zaidi ya shilingi bilioni 10 zinategemewa ku[itishwa katika mwaka huu wa fedha wa utekelezaji mkakati.
Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Manase Goroba alisema kumekuwepo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hasa ya wapiga chapa ikiwamo ya uchakavu wa majengo mengi ambayo yanahitaji ukarabati mkubwa katika mahakama
Alisema kuwa kumekuwepo na mahakama mpya ambazo ni zilijengwa kwa nguvu za wananchi na bado majengo hayo hajakamilika hivyo kunahitaji fedha kwa ajili ya umaliziaji wa majengo hayo.
Mustafa sijani ni hakimu wa mwanzo wa wilaya walimweleza jaji mkuu kuwa adha zinazowakabili watumishi wa mahakama katika utendaji wa kazi ni pamoja na uhaba wa watumishi vitendea kazi
MANUMBA AREJEA KAZINI RASMI
Hatimaye
hali ya afya ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini,
Robert Manumba(Pichani juu), imeimarika na amerejea kazini, limeandika
Mwananchi Akizungumza
kwa njia ya simu, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alikiri
kuwa Manumba amereje kazi ingawa hakuwa tayari kutaja tarehe aliyoingia
kazini.“
Eh! Unauliza nini, mbona ameanza kazi siku nyingi, siwezi kukumbuka
tarehe sipo ofisini naelekea kwenye kikao cha kazi,” alisema Senso.Habari
za kuaminika kutoka kwa baadhi ya maofisa wa kitengo cha upelelezi,
zilisema kiongozi huyo ameshaanza kazi baada ya afya yake kutengemaa.Manumba
mwenyewe, kifupi alisema “Kwa sasa sijambo, ninakwenda kwenye mkutano.”
Mkurugenzi huyo alirejea nchini April 22, mwaka huu akitokea Afrika
Kusini alikokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Millpark.
Amekuwa katika hospitali hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, kuanzia Januari 26, mwaka huu akisumbuliwa na malaria.
MKUU WA GENGE LA MATAPELI WANAOJIFANYA MAAFISA WA TAKUKURU ANASWA JIJINI MWANZA, ALIKUWA AKITUMIA HIRIZI KUFANIKISHA WIZI
Mtuhumiwa Simon Jumbe anayetajwa kujifanya afisa wa Takukuru. |
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kumnasa mtu mmoja ambaye anasadikika kuwa mkuu wa
genge la watu wanaojifanya Maafisa wa Ofisi ya TAKUKURU Mkoani
hapa.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Ayubu Akida alisema kwamba kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Simon Jumbe (32) lakini amekuwa akitumia majina mengie kwa kujiita Mapunda na SP ni kutokana na mtego uliowekwa na maafisa wake.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Ayubu Akida alisema kwamba kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Simon Jumbe (32) lakini amekuwa akitumia majina mengie kwa kujiita Mapunda na SP ni kutokana na mtego uliowekwa na maafisa wake.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza Ayoub Akida, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo. |
“Tuliweka
mtego huo kutokana na kuwepo taarifa za siri kutoka kwa raia wema ambapo
walitueleza kwamba kuna wimbi la baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwadanganya
watu kuwa wao ni maafisa na watumishi wa TAKUKURU baada ya kuweka mtego Mei 13
mwaka huu tumefanikiwa kumnasa huyu maeneo ya Kata ya Mkuyuni Wilayani
Nyamagana” alisema Akida.
KOCHA WA TAIFA STARS KIM POULSEN ATAJA 26 WA STARS KUIVAA MOROCCO
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi
cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini
Marrakech, Morocco.
Katika
kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao
wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao
kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda
mabao 3-1.
Wapya
aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu,
saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally
Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya
na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud
Cholo na Issa Rashid.
Kikosi
kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia
kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama
ifuatavyo;
Makipa
ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa
(Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto
Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari
Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
UJENZI WA KITUO CHA SIKOSELI WAPIGWA JEKI
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (kulia) akisalimiana
na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika hafla ya
kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu ya
wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki
mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini
Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya
Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Wengine ni
baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.
Mjumbe
wa Bodi ya Taasisi ya Sikoseli Tanzania, Mhe. Abdallah Mwinyi (kuli)
akisalimiana na mwendesha baiskeli wa masafa marefu, Alan Knight katika
hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia elimu, afya na matibabu
ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa kituo cha ugonjwa huo
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alan hivi karibuni alishiriki
mbio za baiskeli za KM 17,718 kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini
Afrika Kusini kwa ajili hiyo. Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya
Sikoseli Tanzania ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Grace Rubambey.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya ugonjwa wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (kulia)
akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha ya ajili ya kusaidia
elimu, afya na matibabu ya wagonjwa wa sikoseli nchini na pia ujenzi wa
kituo cha ugonjwa huo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia
walikuwa wakimkaribisha mwendesha baiskeli Alan Knight (wa tatu
kushoto), ambaye hivi karibuni alishiriki mbio za baiskeli za KM 17,718
kutoka Cairo Misri hadi Cape Town nchini Afrika Kusini kwa ajili hiyo.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Sikoseli Tanzania ilifanyika
jijini Dar es Salaam juzi.
TANZANIA YAJIONDOA MICHUANO YA COSAFA
Tanzania
(Taifa Stars) imejitoa kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa
Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) itakayofanyika nchini Zambia kuanzia
Julai 2-26 mwaka huu.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah
amesema Stars ambayo iliingizwa katika michuano hiyo kama timu mwalikwa
imejitoa kutokana na mwingiliano wa ratiba kati ya michuano hiyo na
mechi za Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Amesema
awali Tanzania ilithibitisha kushiriki michuano kwa matarajio kwamba
Uganda ingekubali ombi la TFF la kubadilisha ratiba ya mechi za CHAN,
lakini Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA) likagoma kwa vile
kipindi ambacho kilipendekezwa lenyewe litakuwa na uchaguzi wa viongozi
wao.
Taifa
Stars itacheza na Uganda (The Cranes) katika mechi za CHAN ambapo mechi
ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Julai 12-14 mwaka huu
wakati ya marudiano itafanyika jijini Kampala kati ya Julai 26-28 mwaka
huu.
Akizungumzia
michuano ya COSAFA, Kocha Kim amesema angependa kushiriki michuano hiyo
kwani ingekuwa kipimo kizuri kwa kikosi chake, lakini kwa sasa malengo
makubwa ya Stars kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia na michuano ya
Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambayo fainali zake zitafanyika
mwaka 2015.
MSONDO, CHE MUNDUGWAO, MAJUTO KUSINDIKIZA FAINALI ZA TAIFA ZA MISS UTALII TANZANIA MKWAKWANI TANGA MEI 19, 2013.
Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2013 wakiwa katika Picha ya Pamoja.
Baada
ya shamlashamla na mapokezi makubwa ya Miss Utalii Tanzania walipo
ingia Mkoani Tanga na kupokelewa na umati mkubwa wa watu, warembo hao
wapo kambini tayari kwa maandalizi ya Fainali hizo.
Fainali
za Taifa Miss Utalii Tanzania zitafanyika Tarehe 19.05.2013 Mkoani
Tanga ambapo warembo zaidi ya 30 watapanda Jukwaani kuwania Taji la
Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013 ndani ya Mkwakwani.
RC WA LINDI APOKEA KWA FURAHA TUZO ZA SAFARI LAGER MKOANI KWAKE
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya
Lindi Mji ni Dk. Hamid Nassoro wakiwa ameshikilia tuzo ya Ubingwa wa
Jumla ya Tuzo za Bia Bora Afrika ambayo Bia ya Safari Leger
inayozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Wengine katika picha ni
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Mwakilishi wa TBL
mikoa ya Lindi na Mtwara, Bariki Massawe.
Wakazi
wa Mji wa Lindi wakiwa na furaha na tuzo za Bia ya Safari Lager wakati
wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo
ilizoshinda Bia ya Safari Lager ambapo jana walikuwa Mkoani Lindi.
Wakazi
wa Mji wa Lindi wakiwa na furaha na tuzo za Bia ya Safari Lager wakati
wa ziara maalum ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuonesha Tuzo
ilizoshinda Bia ya Safari Lager ambapo jana walikuwa Mkoani Lindi. Picha
na Mpiga Picha Wetu.
Thursday, May 16, 2013
POLISI MSTAAFU AMCHARANGA MAPANGA MWANAE WA MIAKA 4 ..... RIPOTI KAMILI NA PICHA ZAIDI HIZI HAPA
MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA
KWANZA.
LOWASSA AZINDUA KITABU CHA MTIKISIKO WA UCHUMI
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (kushoto), akizindua kitabu kipya
kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho
'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam LEO.
Katikati ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni iliyochapisha kitabu hicho ya Matokeo Publishers
&Printers, Rosemary Sokile
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (katikati), akizindua kitabu kipya
kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho
'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam leo. Kulia
ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mchapishaji, Dk. Charles
Sokile.
TIKETI SIMBA, YANGA KUANZA KUUZWA KESHO, NANI KUCHEKA, NANI KUNUNA JUMAMOSI????
Mashabiki wa Yanga, Kuendelea kurekodi matukio ya furaha Jumamosi??
Mashabiki wa Simba.....Je Kuendelea na furaha hii Jumamosi???
Mashabiki wa Yanga, Je Simba kupakatwa Jumamosi??????
************************************
*Nani kuficha mabango ya utani Jumamosi?
Tiketi
kwa ajili ya pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Yanga
litakalochezwa keshokutwa (Jumamosi) kwenye Uwanja wa Taifa zitaanza
kuuzwa kesho (Ijumaa) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment