Saturday, May 18, 2013

MATUKIO NA PICHA

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe Zakaria Anshar,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akimsindikiza mgeni wake Balozi wa Indonesia nchini Tanzania  Mhe Zakaria Anshar,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi baada ya mazungumzo yao. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu, Zanzibar

Kinywaji cha Chilly Willy yamwaga vifaa kwa Taswa FC, Taswa

 

IMG_0368Meneja Masoko wa kinywaji cha Chilly Willy kinacho sambazwa na kampuni ya TSN Group, Yohana Manoli  (Kushoto) akimkabidhi jezi mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary (wa kwanza kulia) katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye mgahawa wa Hadees. Kulia ni Meneja Uhusiano wa TSN Group, Meshack Nzowah.
……………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Kinywaji maarufu cha kuongeza nguvu, Chilly Willy Energy Drink kimetoa msaada wa jezi  na mipira kwa timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na timu ya Netiboli, Taswa Queens kwa ajili ya kutumika michezo yake mbali mbali.
Meneja Masoko wa Kampuni ya TSN Group kinachosambaza kinywaji cha Chilly Willy Yohana Manoli alikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyopfanyika kwenye mgahawa wa Hadees uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Manoli alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Taswa SC ni kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kuendeleza michezo nchini na hasa ukizingatia kuwa kinywaji cha Chilly Willy hakina kilevi na ni maalum kwa wanamichezo.

POLISI YAWATIA MBARONI KANGAMOKO ..... RIPOTI KAMILI HII HAPA




JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia baadhi ya wanenguaji wa kundi maarufu kwa kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo lina hatimiliki ya hii habari.

Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambamba na watu hao walikamatwa katika maeneo ya Hoteli ya Travertine, Ambiance Club, Kinondoni Makaburini, Coco Beach na Barabara ya Tunisia.

“Tumewakamata hao wanaofanya mchezo maarufu wa Kangamoko na Laki si Pesa na tayari wanafikishwa mahakamani muda wowote na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.


Kesi ya Mkurugenzi wa Richmond kuunguruma upya, ni baada ya DPP kuikatia rufaa


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imefuta hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Saalam, iliyomuachia huru mkurugenzi wa kampuni ya Richmond Ltd, Naeem Adam Gire, limeandika gazeti la Tanzania Daima la leo

Gire alikuwa akikabiliwa na makosa ya kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kutoa taarifa za uongo kwa maofisa wa umma.

Hukumu hiyo ilitolewa kutokana na rufaa Na.126/2001 iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi(PICHANI) dhidi ya uamuzi wa kesi ya kutoa taarifa za uongo kwa Shirika la Umeme la TANESCO Na. 15/2009 iliyokuwa ikimkabili Gire ambapo mwaka juzi Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alimuona hana kesi ya kujibu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Lawrance Kaduri ambaye katika hukumu yake hiyo alisema alisikiliza hoja za mawakili wa serikali waliokuwa wakimwakilisha muomba rufaa (DPP), Frederick Manyanda na Oswald Tibabyekomya na mjibu rufaa alikuwa akiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa.

“Baada ya kusikiliza hoja zote mbili na pia nimeangalia nakala ya hukumu ya Mahakama ya Kisutu iliyomuachia huru Gire kwa maelezo kuwa hana kesi ya kujibu.

KIPEPERUSHI CHA UCHOCHEZI WA MADAI YA GESI KINACOSAMBAZWA KWA KASI HIKI HAPA



 KIPEPERUSHI CHENYE UJUMBE


Mtihani mgumu kwa Rais Kikwete huu hapa

 

Dar es Salaam. Kuna kila dalili kwamba wabunge wa CCM wameanza kupanga majeshi kwa lengo la ‘kumalizana’ watakapokutana kwa siku mbili mfululizo na mwenyekiti wa chama hicho tawala, Rais Jakaya Kikwete.

Mkutano huo unaotajwa kuwa zao la jitihada za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana unatarajiwa kufanyika kesho na keshokutwa mjini Dodoma, huku kukiwapo taarifa kwamba wabunge wamegawanyika katika makundi kwa lengo la kupenyeza, kisha kutetea hoja walizonazo dhidi ya wenzao.
Miongoni mwa hoja zinazotajwa ni ile ya kushughulikiwa kwa wabunge ambao wamekuwa wakitajwa kwamba ni wapinzani ndani ya CCM, wakiwamo, Alphaxard Kangi Lugora (Mwibara), Deo Filikunjombe (Ludewa), Ally Keissy Mohamed (Nkasi Kaskazini) na Luhaga Mpina (Kisesa).
Wabunge hao wanatuhumiwa na wenzao kwamba wanawasaidia wapinzani kutokana na misimamo yao ya kuikosoa hadharani Serikali katika vikao na mikutano tofauti ya Bunge.
Itakumbukwa kuwa Aprili 25 mwaka huu baada ya kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji, wabunge wa CCM walikutana katika kikao cha dharura kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambako Lugola na Filikunjombe walishambuliwa kutokana na kile kilichodaiwa kwamba wamekuwa wakiidhalilisha Serikali ya CCM bungeni.

JUST IN: Askofu Mkuu Mstaafu Mtega azungumza na waandishi wa habari ... Alichokisema hiki hapa

 


 
 Baba Askofu Mstaafu Norbert Mtega, akijibu maswali ya waandishi wa habari mkoani Ruvuma.
Picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi hao.(Picha na Juma Nyumayo)
--------------------------------------------------------- 

Na Nathan Mtega,Songea
 
 SIKU moja baada ya Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbet kutangaza kustaafu nafasi hiyo kauli ambayo ilizua maswali na mijadala mingi miongoni mwa waumini wa kanisaa katoliki nchini na wananchi kwa ujumla ameamua kuzungumza na waandishi wa habari mjini Songea kufafanua zaidi kuhusiana na uamuzi wake huo.
 
Alisema kuwa ni wazi kuwa uamuzi huo aliouchukua umewashitua wengi lakini amelazimika kufikia uamuzi huo kufuatia kukumbwa na matatizo ya kiafya yaliyojitokeza kwake katika siku za hivi karibuni ambayo hakuwahi kuyapata kwa miaka mingi ya maisha yake pamoja na utume.

Wanafunzi 15 wa sekondari wakamatwa ..... Sababu ya kukamatwa hii hapa

 

 
Na Brandy Nelson, Mwananchi

 Wanafunzi 15, wa Shule ya Sekondari ya Jumuiya ya Wazazi ya Lupata wilayani Rungwe mkoani Mbeya , wanashikiliwa polisi kwa tuhuma za kuchoma moto bweni la wanafunzi wa kiume na kusababisha uharibifu wa mali mbalimbali.  
Aizungumzia tukio hilo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:00 usiku shuleni hapo  na kwamba  wanafunzi hao walifikia hatua hiyo ya kuchoma moto bweni hilo, wakipinga kusimamishwa masomo kwa wanafunzi wenzao watatu kwa utovu wa nidhamu. 
Aliwataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kwa utovu wa nidhamu kuwa ni Joseph Robert (18), anayesoma kidato cha nne na Mwita Chacha (17) na anayesoma kidato cha tatu, wote wakazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam na Mwingine ni Daniel David (18), anayesoma kidato cha tatu ambaye ni mkazi wa Ipinda wilayani Kyela.

MATUKIO KATIKA PICHA YA KIKAO CHA TATHIMINI YA ELIMU WILAYA YA MBINGA

 

 BAADHI YA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBINGA WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA HIYO SENYI NGAGA(HAYUPO PICHANI) WAKATI WA KIKAO CHA TATHIMINI YA ELIMU KATIKA WILAYA HIYO AMBAPO IMEFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA KUONGEZA KIWANGO CHA UFAURU KATIKA ELIMU YA MSINGI KUTOKA NAFSI YA TANO KIMKOA HADI YA TATU KATIKA MITIHANI YA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI KWA MWAKA 2012/2013
 BAADHI YA WATENDAJI WA MITAA,KATA NA WAKUU WA SHULE WILAYA YA MBINGA WALIOHUDHURIA KIKAO CHA TAHIMINI YA ELIMU
 BAADHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI HIYO YA MBINGA WAKIFUATILIA KWA MAKINI TAARIFA MBALIMBALI
 MKUU WA WILAYA YA MBINGA SENYI NGAGA AKIFUNGUA KIKAO CHA TATHIMINI YA ELIMU KATIKA WILAYA HIYO KILICHOFANYIKA MJINI HUMO

No comments: