;Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said,amemwagiwa
tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu
yake ya kifua na jicho kuumia pia.
Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema
chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la
tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili
kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya
nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na
kwamba hakuweza kumtambua.
Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
No comments:
Post a Comment