KUTOKANA
na familia ya Freeman Illuminati bloodline kuanzisha chama cha ‘Priory
de Sion’kilichokuwa na lengo la kuingiza mafundisho machafu ndani ya
imani ya kweli, dunia ililazimika kusubiri awamu nne za utawala wa
serikali moja kabla ya kuunganisha dini na serikali na kuwa kitu kimoja.
Kumbuka kwamba Mungu hutumia namba 1 hadi 12 ambapo namba 4 humaanisha
‘ukomavu na kuvunwa kwa mazao’ – rejea Marko 4: 26 kwa mbegu njema na
Yakobo 1:14,15.
Rais
Nimrodi wa serikali ya awamu ya kwanza ndiye aliyepanda mbegu ya
‘tamaa’ ya kuanzisha serikali na dini moja itakayoitawala dunia nzima.
‘Tamaa’ ya rais Nimrodi ilitengeneza ‘mimba’ na kupelekea awamu ya pili
ya serikali moja ya dunia chini ya Waamedi na Waajemi wakati huo Dario
akiwa ndiye rais na ikulu ya serikali hiyo ikiwa katika eneo la Iran ya
leo. Baada ya miongo kadhaa kupita, ‘Mimba’hiyo ilileta mtoto aliyepewa
jina la ‘dhambi’ wakati wa awamu ya tatu ya serikali moja ya dunia
iliyoitwa Uyunani chini ya rais Alexander mkuu aliyeweka ikulu yake huko
Ugiriki. Historia inatuambia kwamba rais Alexander mkuu alikuwa katili
na aliyefanikiwa kuua mamia kama sio maelfu ya watu duniani kote.
Hatimaye
mbegu ya ‘tamaa’ iliyopandwa na rais Nimrodi wa serikali ya awamu ya
kwanza ilipotengeneza‘mimba’ na kuzaa mtoto ‘dhambi’, mtoto huyo
alikomaa baada ya kufikisha umri wa utu uzima. Sasa hakuitwa ‘mtoto’
tena bali jina lake lilibadilika na kuitwa‘mauti’. Kumbuka kwamba kuna
hatua nne za kukua na kukomaa kwa mbegu hadi wakati wa kuvunwa. Hivyo
ndivyo ilivyokuwa wakati dunia yetu iliposhuhudia awamu nne za serikali
moja ya dunia ambapo katika awamu ya nne palitokea mavuno yaliyoleta
mazao ya muungano wa serikali na dini.
Ulikuwa
ni utawala wa serikali ya awamu ya nne (Roman empire) chini ya rais
Constantine aliyeweka ikulu yake huko Roma ndipo imani ya kweli
ilipokufa baada ya rais huyo kuanzisha dini iliyochanganya ukweli na
uongo kwa kutumia kanuni ya‘Thesis x Antithesis = Synthesis. Imani
ya kweli ilikuwa ni ‘Thesis’ wakati imani ya kipagani iliyoanzishwa na
Nimrodi ilikuwa ni ‘Antithesis’. Imani hizi mbili zilichanganywa na rais
Constantine na kuzaa kitu kinachoitwa ‘Synthesis’ yaani mchanganyiko wa
ukweli na uongo. Hiyo ilikuwa ni baada ya miaka mingi kupita tangu rais
Nimrodi alipotamani kuanzisha mfumo wa utawala uliunganisha serikali na
dini na kuwa kitu kimoja. Hiyo ilikuwa ni awamu ya nne ya utawala wa
serikali moja ya dunia. Naam! Dini iliyoanzishwa huko Roma wakati wa
awamu ya nne ya utawala wa serikali moja ya dunia chini ya rais
Constantine ilikuwa ni matokeo ya mbegu ya ‘tamaa’ ya rais Nimrodi ya
kuanzisha mfumo wa serikali iliyoungana na dini katika utawala wa dunia
nzima.
Jambo
hilo la kuunganisha serikali na dini pamoja na kuchanganya ukweli na
uongo lilipigwa vita vikali na ‘waprotestant’ ambao hawakuwa tayari
kuona ukweli wa neno la Mungu ukichanganywa na uongo. Hata hivyo
‘waprotestant’ hao hawakufanikiwa kutenganisha serikali na dini na ndipo
wakamua kujitenga na dini iliyokuwa imeungana na serikali ili wapate
kumuabudu Mungu katika roho na kweli.
Ilipofika
mwaka 1798 kulitokea badiliko katika serikali iliyoungana na dini baada
ya rais na kiongozi wa dini kukamatwa na kuuawa huko ufaransa. Baada ya
kifo cha rais na kiongozi wa dini wa serikali moja ya dunia, ilionekana
kana kwamba ndio mwisho wa mfumo wa utawala uliounganisha serikali na
dini. Lakini haukuwa mwisho kwa sababu liliundwa taifa moja katika mji
wa Roma likiwa linaendeleza mfumo wa kuunganisha serikali na dini. Taifa
hilo likapewa jina la Vatican. Ndioo! Vatican ni nchi inayotawalaiwa na
Papa akiwa ndiye rais na kiongozi wa dini pia. Sasa jina la serikali
hiyo likaitwa ‘Roman Catholic’ yaani ‘ulimwengu wa Kirumi’. Maana ya
neno ‘catholic’ ni ‘universal’ au iliyoenea dunia nzima. Serikali hii
imeenea dunia nzima kutokana na uwepo wa wawakilishi (mabalozi) wa taifa
hilo duniani kote. Ukilinganisha na mataifa mengine katika eneo la
mraba, inawezekana taifa hili ndilo dogo kuliko mataifa mengine duniani
kote lakini ni taifa lenye nguvu kubwa kuliko mataifa yote – usishangae!
Zimekuwepo
juhudi za kuhakikisha kwamba dunia nzima inarudi kwenye mfumo wa
utawala wa serikali na dini. Freemasons wamekuwa kwenye mipango ya muda
mrefu latika kuhakikisha kwamba serikali moja ya dunia itakayounganisha
dini na uchumi kwa pamoja inaundwa haraka iwezekanavyo. Serikali hiyo
itakuwa imejengwa kwenye msingi uliowekwa na rais wa kwanza katika awamu
ya kwanza ya utawala wa serikali moja ya dunia. Itakumbukwa kwamba rais
Nimrodi alianzisha dini iliyoabudu miungu (sayari) 36 ambapo jumla ya
miungu hao ilileta namba 666.
..... Safari ijayo tutaitazama namba 666 na uhusiano wake na Freemasons .... Endelea kuwa na NDGSHILATU BLOG mahala popote na wakati wowote .....
FREEMASONS NA HEKA HEKA ZA MWISHO WA DUNIA
Naam! Disemba
21, 2012 imepita; Sayari yetu haikugongwa na kupasuka na Hatukuona
mwisho wa dunia! Lakini ni nini kimetokea? Ilifanyika mikutano kadhaa
katika pande nne za dunia. Moja ya mikutano hiyo ni ule uliofanyika
Vatican siku 18 (6+6+6) kabla ya Disemba 21. Mkutano huo ulifanyika siku
ya Disemba 3, 2012 ukiwahusisha wakuu wa kanisa Katoliki katika kile
kinachojulikana kama ‘Pontifical Council for Justice and Peace’ ambapo
kiongozi mkuu wa kanisa hilo Papa Benedict xvi ndiye aliyehutubia
mkutano huo. Akihutubia makumi ya makadinali waliohudhuria kwenye
mkutano huo Papa Benedict xvi alitoa wito wa kuundwa kwa serikali ya
dunia (world government) itakayokuwa
na mfumo mpya wa dunia (New world Order) kwa ajili ya kutatua matatizo
ya kijamii na kiuchumi. Kiongozi huyo wa kanisa alikaririwa akisema
kwamba kuna umuhimu wa kuundwa kile alichokiita: “construction of a world community, with a corresponding authority,” Kisha akaongeza kusema:“The
proposed body (World Government) would not be a superpower,
concentrated in the hands of a few, which would dominate all peoples,
exploiting the weakest. Maneno hayo yanamaanisha kuundwa kwa chombo cha
dunia kitakachokuwa na mamlaka ya umma ambacho hakitakuwa chini ya watu
wachache watakaowanyonya wanyonge. Itakumbukwa kwamba mwaka 2010 Papa
Benedict xvi alitoa wito wa kuundwa kwa ‘Central World Bank’
itakayoshughulikia maswala ya fedha duniani kote.
Sasa msikilize muumini wa freemason na mfanyabiashara za kibenki bwana Paul Warburg akisema kwamba "We
will have a world government whether you like it or not. The only
question is whether that government will be achieved by conquest or
consent." (maneno
hayo aliyasema siku ya February 17, 1950, alipokuwa akilihutubia baraza
la Seneti nchini Marekani).Warburg alimaanisha kwamba serikali ya dunia
lazima ianzishwe, utake au usitake. Swali ni kama serikali hiyo
itaanzishwa kwa makubaliano au kwa vita.
Mwaka 1992, Dr. John Coleman aliandika kitabu kinachoitwa ‘Conspirators Hierarchy: The Story of the Committee of 300’.
Katika kitabu hicho Dr. Coleman anaainisha watu wanaohusika na mchakato
mzima wa kuundwa kwa serikali moja ya dunia au New World Order. Katika
ukurasa wa 161 Dr. Coleman anaelezea malengo ya kamati ya watu 300
(mwenyekiti wake akiwa ni mkuu wa kanisa duniani) na kusema:"A
One World Government and one-unit monetary system, under permanent
non-elected hereditary oligarchists who self-select from among their
numbers in the form of a feudal system as it was in the Middle Ages. In
this One World entity, population will be limited by restrictions on the
number of children per family, diseases, wars, famines, until 1 billion
people who are useful to the ruling class, in areas which will be
strictly and clearly defined, remain as the total world population.
There
will be no middle class, only rulers and the servants. All laws will be
uniform under a legal system of world courts practicing the same
unified code of laws, backed up by a One World Government police force
and a One World unified military to enforce laws in all former countries
where no national boundaries shall exist. The system will be on the
basis of a welfare state; those who are obedient and subservient to the
One World Government will be rewarded with the means to live; those who
are rebellious will simply be starved to death or be declared outlaws,
thus a target for anyone who wishes to kill them. Privately owned
firearms or weapons of any kind will be prohibited."
Kwa
ufupi maneno hayo yanamaanisha kwamba kutakuwepo na serikali moja na
mfumo mmoja wa kifedha ambapo kiongozi wa serikali hiyo atachaguliwa na
watu 300 wanaounda kamati kuu ya serikali hiyo. Idadi ya watu duniani
itapunguzwa kwa kuanzishwa sharia za kuwa na idadi maalumu ya watoto
katika familia ambapo mbinu itakayotumika kutekeleza lengo hilo ni
kusababisha magonjwa, vita, njaa hadi idadi ya watu ifikie bilioni moja
duniani kote. Kutaanzishwa mfumo mmoja wa kijeshi utakaosimamia sharia
katika nchi zote ambapo mipaka yote ya nchi zote itaondolewa. Wale
watakaokuwa watiifu katika serikali hiyo watawezeshwa kuishi; wale
watakaokuwa wapinzani na waasi wataanchwa wafe kwa njaa au kuhumiwa kama
wavunja sharia. Haki ya kumiliki silaha za aina yoyote itaondolewa’.
Itakumbukwa kwamba hivi karibuni watoto 20 na waalimu wao 6 waliuawa kwa
kupigwa risasi katika shule moja huko Marekani. Baada ya tukio hilo
serikali ya Marekani imeanza kupitia upya sheria za umiliki wa silaha
kwa watu binafsi.
Rais
Barack Obama aliyeshinda uchaguzi ulioshirikisha vyama 6 nchini
Marekani amekwisha saini mabadiliko kadhaa ya sheria. Rais Obama
amesaini sheria inayoitwa TARP (Troubled Asset Relief Program) ambapo
chini ya sheria hiyo mabenki yote (Wall street) pamoja na mabenki ya
kigeni yanakuwa katika dhamana kwa serikali. Sheria nyingine ni H.R 347
(House Resolution) au “Federal Restricted Buildings and Grounds Improvement Act of 2011,”.
Sheria hii inazuia maandamano ya kwenda kwenye majengo ya serikali
ikiwa ni pamoja na zuio la kuendeleza majengo na ardhi. Wanaharakati wa
haki za binadamu nchini Marekani (American Civil Liberties Union –ACLU))
wanaipinga vikali sheria hiyo kwamba inawagandamiza wanyonge. Sheria
nyingine ni‘National Defense Authorization Act’ – NDAA. Sheria hii
inampa nguvu na mamlaka rais wa Marekani kuamuru kukamatwa na kufungwa
gerezani kwa mtu yeyote bila hata ya kufikishwa mahakamani na
kufunguliwa mashitaka. Kama ulikuwa unafikiri kwamba rais Morsi Mohamed
wa Muslim Brotherhood Misri amejipatia madaraka makubwa kupita kiasi,
basi yupo pia rais wa Marekani chini ya NDAA!
Najua
wengi watanishangaa ninaposema kwamba uchaguzi wa rais Marekani
ulishirikisha vyama 6 na sio viwili. Ili usiniulize maswali juu ya hilo,
vyama hivyo ni: 1)Democratic –Baraka Obama; 2)Republican – Miti Romney;
3)Libertarian Party - Gary Johnson; 4) Green Party- Jill Stein; 5)
Constitution Party - Virgil Goode; na 6) Justice Party - Rocky
Anderson.Kwa nini vyama 6 – ni namba ya utawala wa freemason.Kwa nini
vyama vingine havikusikika? Ni kwa sababu Illuminati ndio walioshikilia
‘media’ na wao ndio waamuzi wa nani atangazwe na nani hapana.
Nini
maana ya wito wa kuundwa kwa ‘world community’ pamoja na ‘Central World
Bank’ kutoka kwa Papa Benedict xvi? Ni kutimizwa kwa unabii wa Ufunuo
13:17. Haitawezekana kuzuiwa kuuza na kununua kama hakuna chombo
kinachosimamia uchumi na fedha. Chombo hicho ni ‘Central World Bank’
(CWB). Lakini pia CWB haitakuwa na nguvu za kusimamia shughuli za
kifedha kama hakuna serikali nyuma yake. Serikali hiyo ni ‘World
Community Authority’ au ‘World Government’ yaani serikali ya dunia.
Wakati
Papa Benedict xvi akitoa wito wa kuleta ‘haki na amani’ duniani, chuo
kikuu cha Kiislamu (Sunn Al - Azhar University) kimetoa shukrani kwa
Vatican kutokana na juhudi za kanisa Katoliki kwa kukemea vitendo
vinavyoashiria uvunjifu wa amani duniani, kutetea imani za watu wote
pamoja na kuziwezesha dini zote kutumia alama na nembo kama utambulisho
wa dini husika.
Akihojiwa
na waandishi wa habari, Mahmoud Azab ambaye ni mshauri wa Sheikh
anayesimamia kitengo cha mahusiano ya kidini (interfaith Dialogue)
katika chuo kikuu cha Al-Azhar, aliwashukuru wote wanaotetea ukweli na
heshima ya dini. Mahmoud Azab alikuwa akijibu hotuba iliyotolewa hapo
kabla na msemaji wa Vatican Fr. Federico Lombardi. Kwa
nini Mahmoud atoe shukrani kwa Papa kutokana na matumizi ya alama/nembo
katika dini? Unaweza kuchunguza alama/nembo kwenye jengo la chuo kikuu
cha Al-Azhar na jengo alipokaa Papa Benedict xvi akihutubia baraza la
haki na amani Vatican. Unazikumbuka kanuni 3 wanazotumia freemasons
kufanya kazi zao? Tafakari!
Itakumbukwa
kwamba baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Benghazi na
kuuawa kwa aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya kutokana na hasira
za waumini wa kiislamu zilizotokana na kutolewa kwa sinema inayomkashifu
SAW Mohammad (Innocence of Muslims), Fr. Federico Lombardi alitoa matamko na kusema kwamba: “profound
respect for the beliefs, texts, outstanding figures and symbols of the
various religions is an essential precondition for the peaceful
coexistence of peoples”akiwa
anamaanisha kwamba ili pawepo na amani kwa watu, kunatakiwa pawepo na
kuheshimu imani, maandiko pamoja na alama/nembo mbalimbali zinazotumiwa
na dini kama utambulisho wao.
Akielezea
kwa nini pamekuwepo na mjadala kati ya Al-Azhar University na Vatican,
Abdel Muti al-Bayoumi, mjumbe wa ‘Islamic Research Academy’ katika chuo
kikuu cha Al-Azhar alisema kwamba mjadala huo hauhusiani na kauli ya
Papa Benedict xvi aliyoitoa kwa kuwatetea Wakristo wa dhehebu la
Christian Copts wa Misri ambao wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na
kushambuliwa kwa sababu ya imani yao. Alipoulizwa kutoa kauli juu ya
mjadala kati ya pande hizo mbili, Mahamoud Azab alisema, ““I
have nothing to say on the subject at this present time” akimaanisha
kwamba hawezi kusema juu ya mjadala huo kwa wakati huu. Hata hivyo Azab
alikemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya waumini kwa kuchoma
Biblia wakati wa maandamano yaliyofanyika kupinga sinema ya ‘Innocence
of Muslims’.Aliwataka waislamu wote kuheshimu Torah, Injili na maandiko
Matakatifu kwa sababu ndivyo alivyofanya mtume Mohammad SAW.
Kwa
nini pawepo na mfululizo wa mijadala kati ya Al-Azhar University na
Vatican; serikali ya Iran na Vatican na hata serikali ya Saud Arabia na
Vatican?
Wiki
jana nilielezea vyanzo vya baadhi ya makanisa. Sikuelezea historia ya
kanisa la Roman Katoliki na lini lilianza.Lakini pia sikuelezea historia
ya dini ya Kiislamu.
Kwa
uchache kanisa la Roman Catholic ni kanisa la Roma, kama
linavyojulikana, kanisa la Roma.Roma ni mji mashuhuri uliopo Italia. Mji
wa Roma una historia ndefu katika dunia na ni mji uliotabiriwa na Mungu
pia.
Dunia
yetu imewahi kushuhudia ikitawaliwa na serikali moja katika awamu nne.
Awamu ya kwanza ilikuwa ni serikali ya dunia iliyopewa jina la Babeli.
Rais au mfalme wakwanza katika serikali hiyo alikuwa ni Nimrodi
akifuatiwa na Nebukadneza pamoja na marais waliomfuata. Asili ya
serikali hii ni mnara wa Babeli uliojengwa na mfalme wa kwanza wa
Babeli, rais Nimrodi. Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya serikali ya
dunia awamu ya kwanza ni Iraqi.
Awamu
ya pili ya serikali ya dunia iliitwa Mede/Uajemi ambapo mmoja wa marais
wa serikali hii aliitwa Dario.Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya
serikali hii ni Iran ya leo. Awamu ya tatu ya serikali ya dunia iliitwa
serikali ya Uyunani au Greece government. Mmoja wa marais mashuhuri
katika serikali hii alikuwa ni Alexander mkuu (Alexander the Great).
Awamu ya nne ya serikali ya dunia iliitwa‘Roman Empire’ au himaya ya
Roma. Mmoja wa marais wa serikali hii alikuwa ni Constantine. Serikali
hii ndiyo iliyotawala kwa muda mrefu kuliko serikali zote
zilizoitangulia.
Wakati
serikali hizo zinatawala dunia, dini ya kweli ilikuwa haijatikiswa hadi
serikali ya Roma ilipoanza kutawala. Je, dini ya freemasons ilianza
lini? Ukiondoa dini aliyoianzisha Mungu katika bustani ya Edeni, dini ya
freemasons ndiyo dini iliyoanza siku nyingi kuliko dini nyingine.Dini
hii ilianzishwa pia kwenye bustani ya Eden mwanzilishi wake akiwa ni
Shetani. Alimtumia Kaini anayejulikana kwa freemasons wa leo kama ‘first
freemason’ yaani mjenzi huru wa kwanza.
Hatimaye
rais Constantine kwa nusu aliamua kuachana na ibada za kipagani na
kujiunga na Ukristo. Hii ilikuwa ni kutimizwa kwa andiko la 2
Wathesalonike 2:3,4 maana ulikuwa ni ukengeufu wa kanisa la mitume
sehemu ya kwanza uliopelekea kuanzishwa kwa dini iliyochanganya ukweli
na uongo. Kwa nini dini hii ilisubiri hadi awamu ya nne ya serikali ya
dunia? Pengine nizungumzie kidogo maana ya namba nne kama inavyotumiwa
na Mungu. Namba nne sio namba maalumu kwa freemasons lakini ni muhimu
sana kwa Mungu. Namba nne inamaanisha kukomaa kwa mavuno na kuvunwa.
Tazama hapa: “Akawaambia ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu
aliyemwaga mbegu juu ya nchi…..Maana nchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena(pili)suke, kisha(tatu),ngano pevu katika suke. Hata (nne)matunda yakiiva
mara aupeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika” Marko 4:26 –kwenye
mabano ni ufafanuzi wa mwandishi. Hizo ni hatua nne kufika kuvunwa kwa
mbegu njema. Vipi habari ya mbegu mbaya? “Lakini kila mmoja hujaribiwa(kwanza)kwatamaa yake mwenyewe. Halafuile tamaa ikisha kuchukua mimba(pili), huzaa dhambi (tatu),na ile dhambi ikiisha kukomaa, huzaa mauti(nne)”Yakobo
1:14,15. Unaweza pia kujua ni kwa nini waisraeli walitumia miaka 40
(4x10) kutoka Misri hadi Kanaani; kwa nini Yesu, Musa walifunga kwa siku
40 (4x10). Kumbuka kwamba namba 10 kwa Mungu inawakilisha ‘ukamilifu wa
Mungu’ na namba 7 inawakilisha ‘utimilifu wa Mungu’.Kuna tofauti kati
ya ‘ukamilifu’ – ‘perfection’ na ‘utimilifu’ – ‘fulness’.Kitu kinaweza
kuwa ‘timilifu’ lakini kisiwe ‘kamilifu’ lakini kitu hakiwezi kuwa
‘kamilifu’ bila ya kuwa ‘timilifu’.
Kwa mfano mapigo 7 ni utimilifu wa ghabu ya Mungu lakini ukamilifu wa
hukumu yake utafikiwa wakati Shetani, dhambi na wadhambi
watakapoangamizwa motoni. Mungu alitoa amri 10 kwa wanadamu ikimaanisha
kwamba amri hizo zinawakilisha tabia ya Mungu ambayo ni ‘kamilifu’.
Lakini pia tunasoma “….Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima na ‘ukamilifu’ wa uzuri” kisha anaanza kutaja ni kwa namna gani alikuwa ‘mkamilifu’
wa uzuri akisema “1)Akiki, 2)Yakuti manjano, 3)Almasi, 4)zabarajadi,
5)shohamu, 6)Yaspi, 7)yakuti samawi, 8)zumaridi, 9)baharamani na
10)dhahabu. Lusifa alikuwa‘mkamilifu wa uzuri’ kutokana na kuvikwa aina 10 za madini ya thamani kubwa. Mungu ni‘mkamilifu’ kutokana na kuwa na tabia inayoelezewa kwenye amri 10katika Kutoka 20:4-17. Je wewe ni mkamilifu wa tabia kama ya Mungu kwa kuzitunza amri 10? Tafakari!
FREEMASONS NA FAMILIA 13 ZA ILUMINATI
NI chama cha Prieure de Sion (Priory de Sion) kilichoanzishwa na familia ya 11 ya Illuminati inayoitwa Freeman Illuminati bloodlines ndicho kilichosababisha kuanzishwa kwa ‘Uprotestant’ au ‘Upinzani’ ndani ya dini. Wakainuka mashujaa wengi waliopinga mafundisho machafu yaliyoingizwa ndani ya imani ya kweli ili kutetea neno la Mungu litawale tofauti na mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Miongoni mwa mashujaa walioinuka kupingana na mafundisho ya chama cha Prieure de Sion alikuwa Martin Luther. Kumbuka kwamba wapinzani ‘Protestants’hawa walikuwa wanapinga mafundisho wakiwa ndani ya mifumo ya dini zao. Hata hivyo hawakufanikiwa kuleta matokeo mazuri ya upinzani wao na hivyo wakaamua kutoka na kujitenga na dini wakiwa na baadhi ya mafundisho machafu waliyoyarithi kutoka kwenye mifumo potofu ya kidini. Wakiwa wamejitenga, sasa waliamua kufanya ‘matengenezo’ kwa lengo la kuondoa mafundisho machafu na kubaki na mafundisho safi kama ilivyoagizwa na Mungu. Hivyo jina lao wakaitwa‘Reformers’ au ‘Wanamatengenezo’ badala ya ‘Protestants’ au ‘wapinzani’.‘Waprotestants’ wa awali walijua maana ya kanisa na ndio maana hawakuona shida kujitenga na mifumo iliyokuwa inadhaniwa kuwa ndiyo kanisa.Lakini je, nani aliyeanzisha ‘Uprotestant’na ‘matengenezo’? Ellen White anasema: “Christ was a protestant...The Reformersdate back to Christ and the apostles. They came out and separated themselves from a religion of forms and ceremonies. Lutherand his followers did not invent the reformed religion. They simply accepted it as presented by Christ and the apostles." E.G. White, Review and Herald, vol. 2, 48, col. 2.Hapo anamaanisha kwamba ‘Kristo (Yesu) alikuwa ni Mprotestant….wanamatengenezo waliiga kutoka kwa Kristo na mitume. Walijitenga na dini ya desturi na sherehe. Luther na wafuasi wake hawakuanzisha dini ya matengenezo. Waliikubali kama ilivyoonyeshwa na Kristo na mitume’ [rejea: R&H, Vol. 2, 48, col.2].
Ni kwa namna gani Kristo alijitenga? E. White anaendelea kusema: “Pharisees and Sadducees were alike silenced. Jesus summoned His disciples, and prepared to leave the temple,
not as one defeated and forced from the presence of his adversaries,
but as one whose work was accomplished. He retired a victor from the
contest”. {DA 620.2}
‘Mafarisayo
na masadukayo walinyamazishwa. Yesu aliwakusanya wanafunzi wake, na
akawaandaa kuliacha hekalu, sio kama aliyeshindwa na kulazimishwa
kuondoka kwa maadui zake, bali kama ambaye kazi yake ilikuwa
imekamilika. Alikuwa ni mshindi katika mashindano”. {DA 620.2}
Biblia
inasema kwamba Yesu alijitahidi kupingana na mafarisayo na masadukayo
akiwa ndani ya mfumo wa dini ya kiyahudi na sasa alikuwa amefikia mwisho
wa upinzani wake na akaamua kujitenga moja kwa moja na mfumo wa dini
hiyo ili awafundishe vizuri wanafunzi wake ambao walikuwa tayari
kukubali mafundisho safi. E.G. White anasema:"
Hitherto He had called the temple His Father's house; but now, as the
Son of God should pass out from those walls, God's presence would be
withdrawn forever from the temple built to His glory. Henceforth its
ceremonies would be meaningless, its services a mockery. {DA 620.4}Hatimaye
Yesu na wanafunzi wake walijitenga na hekalu lililokuwa mpendwa wao.
Lakini kwa sababu viongozi wa hekalu walikataa kufuata mafundisho ya
neno la Mungu peke yake, Mwana wa Mungu hakuona sababu ya kuendelea
kubaki ndani ya hekalu ingawa “Alikuwa akiliita hekalu kuwa ni nyumba ya
Baba yake; lakini sasa, kama Mwana wa Mungu ambavyo akipita kutoka
katika kuta hizo, uwepo wa Mungu ungeondolewa milele usionekane ndani ya
hekalu lililojengwa kwa utukufu Wake. Hivyo sherehe zilizofanyika ndani
ya hekalu hazikuwa na maana, huduma zake zikawa dhihaka”. {DA 620.4}.
Hivyo ndivyo alivyofanya Martin Luther na wafuasi wake.
Baada
ya kifo cha Martin Luther, wafuasi wake waliendelea katika kufanya
matengenezo. Hata hivyo kwa sababu freemasons hawakati tamaa,
matengenezo yalikoma na kuanza kurudi nyuma taratibu ambapo leo hii wale
wanaoitwa ‘Walutheri’ wameungana tena na mfumo ambao mwanzilishi wao,
Martin Luther, aliuiita ‘mfumo mchafu’.
Wakati
matengenezo yanaendelea, ulikuwa ni wakati wa kutimizwa kwa unabii wa
siku 1260 sawa na miaka 1260 kama ilivyotabiriwa na nabii Yohana. Wakati
huo kulianzishwa matengenezo mengi na kupelekea kuanzishwa kwa mifumo
mingine ya makanisa. Baadhi ya makanisa yaliyoanzishwa yalikuwa haya:
Anglican:
Lilianzishwa huko England na mfalme wa Uingereza ili kupinga kanisa la
Roma. Kiongozi mkuu wa kanisa hilo ni Malkia wa Uingereza. Hata hivyo
wachunguzi wa dini ya freemasons wanasema kwamba familia ya Malkia ni
familia mojawapo kati ya familia 13 za waumini wa Freemasons.
Presbyterian:
Mwanzilishi ni John Calvin mwaka 1509 – 1564 na John Knox 1505 – 1572.
Kanisa hili lilijitenga na Roma likiwa na motto “Chunguza maandiko”
maana liliona kwamba kanisa la Roma linakwenda kinyume na maandiko. Hata
hivyo wafuasi wa John Calvin na John Knox wameshindwa kufikia malengo
ya kuyachunguza maandiko na kufuata kile asemacho Mungu na badala yake
wamekubali kurudi walikotoka!
MENNONITE:
Lilizaliwa rasmi mwaka 1525 – 1530 na Conrad Grebel na wenzake akiwemo
Zwingli Ulrich aliyetofautiana na Martin Luther juu ya somo la pasaka.
Hawa walikataa ubatizo wa Roma wa kunyunyizia maji na jina jingine
wanaitwa “Meno Knights” majina ambayo yanafanana na vikundi vya
Freemason kama vile “The knights of Eulogia”(Skull and Bones), “The
knights of Malta”. Ingawa lengo la Zwingli Ulrich lilikuwa zuri, baada
ya kifo chake wafuasi wake walikubali kuingiliwa na freemasons na hivyo
kushindwa kufikia lengo lililokusudiwa.
LUTHERAN:
Mwanzilishi ni Martin Luther mwaka 1517. Alikuwa ni Mjerumani
aliyesomea ukasisi wa kanisa la Roma na mwaka 1511 akapata Phd katika
chuo kikuu cha Wattenberg. Alipingana na kanisa lake la Roma na kuandika
sababu 95 zinazopinga mafundisho ya Roma ndipo akajitenga na Roma na
hivyo wafuasi wake wakaendelea kutumia jina la Lutheran, yaani wafuasi
wa Luther. Wafuasi wa Luther hawakuendelea mbele na sasa wamerudi kwenye
makosa aliyokuwa akiyapinga Luther. Je, Lutheran wa leo wanafuata kweli
nyayo za Martin Luther? Au wametekwa kwa matumizi ya njama ya
“Following Gurus”yaani kufuata kila wasemacho viongozi? Tafakari!
Moravian:
Mwanzilishi ni John Huss aliyezaliwa mwaka 1366 na kuchomwa moto na
papa hadi kufa mwaka 1416 baada ya kulipinga kanisa la Roma. Wafuasi
wake hadi leo wanaitwa kanisa la Moravian. Kwa bahati mbaya wafuasi wa
John Huss hawakuendelea kufanya matengezo ili kusonga mbele zaidi ya
Huss na kibaya zaidi ni kwamba wanarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Leo Huss akifufuka atashangaa kuona jinsi wafuasi wake walivyoacha
kanuni alizozianzisha. Je, wamoravian wa leo wako tayari kuchomwa moto
kwa kutetea ukweli kama John Huss? Tafakari!
Baptist:
Ni kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa Martin Luther ambao walijitenga
na Lutheran mwaka 1600 huko Uholanzi na Uingereza baada ya kuona kwamba
wafuasi wenzao wameacha kanuni alizoziweka Martin Luther. Hata hivyo
kanisa la Baptist la leo haliendeleza jitihada za Luther na sasa badala
ya kusonga mbele linapiga ‘marktime’ likiwa limegeuka nyuma.
Salvation Army (Jeshi la Wokovu):
Mwanzilishi ni Booth mwaka 1878. Kanisa hili lilianzishwa na wafuasi wa
freemasons kwa lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Kumbuka kwamba
Shetani hutumia fursa inayotolewa na Mungu akiwa na lengo la kuwafanya
watu washindwe kujua kipi ni cha kweli na kipi sio. Katika kila
matengenezo ya kweli, pamekuwepo na matengenezo bandia.
Marmon church:
Mwanzilishi ni Joseph Smith (1805 – 1844). Kanisa hili linajulikana pia
kama The church of Jesus Christ of later day saints. Kanisa la Mormon
lilianzishwa na wafuasi wa freemason wakiwa na lengo la kuchafua
matengenezo ya kweli. Mitt Romney ni muumini wa kanisa la Mormon.
Methodist: Kiongozi Mwanzilishi ni John Wesley. Lilianzishwa na watu 17 wa familia moja
mwaka 1738 likiwa na lengo la kupinga mafundisho ya freemasons. Kanisa
hilo halijakamilisha lengo la matengenezo kutokana na ukweli kwamba
wafuasi wake hawana mwamko aliokuwa nao John Wesley.
Watch Tower:
Mwanzilishi ni Charles T. Russel 1852 – 1916 na mwenzake J. Lutheford
1869 – 1942. Baba yake Charles T. Russel alikuwa ni mchungaji wa
Prebyterian. Mnamo mwaka 1932 huko Marekani jina la kanisa hilo
lilibadilishwa na kuitwa Mashahidi wa Yehova. Markus Mpangala ameelezea
kwa kirefu chanzo cha dhehebu hili akiainisha kwamba waanzilishi
walikuwa ni Freemasons kutoka kwenye familia ya Illuminati inayoitwa
Russel illuminati bloodline ambayo nimeshaielezea kwenye makala
zilizopita.
Brethen Assemblies:
Mwanzilishi ni ndg. Dabi 1800 – 1882 ambaye alikuwa ni muumini wa
Anglican na akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake. Dabi
aliamua kujitenga na Anglican kutokana na kanisa hilo kutawaliwa na
familia ya freemasons.
Makanisa ya Kipentekoste au kilokole:
Ni makanisa yaliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni. Makanisa haya
yalianzishwa huko Kansas City Marekani mwaka 1901kwa lengo la kupata
nguvu ya kile kinachoaminiwa kuwa roho mtakatifu. Je, unajua uhusiano
uliopo kati ya muziki wa‘rap’ au ‘kufoka’ na uvuvio wa kunena kwa lugha
kutoka kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni nguvu za roho mtakatifu wakati
waumini wa kilokole wanapokuwa wakiomba? Kumbuka kwamba Muziki wa rap
ulianzia huko Kansas City Marekani, mahali ambako makanisa ya
kipentekoste yalianzishwa. Panapo majaaliwa, nitakuwa na makala ndefu
kuhusu asili, lengo na nguvu inayoonekana kwa viongozi wa makanisa ya
kilokole kama akina T.B Joshua wa SCOAN la huko Nigeria. Kwa wakati huu
nasema,‘Soma Biblia na Tafakari’!
Gospel terbenacle: Mwanzilishi ni Pastor A.B. Simpson mwaka 1881 akitokea Presybiterian.
Christian Churches: Mwanzilishi ni Thomas Chapel mwaka 1807 akitokea Presybiterian.
Seventh –Day Advetist Church:
Mwaka 1844 baada ya kutokurejea kwa Yesu duniani kama ilivyohubiriwa na
muhubiri mashuhuri aitwaye William Miller, watu wengi walivunjika moyo
isipokuwa watu 50 tu ndio walioendelea kujifunza Biblia miongoni mwao
akiwa ni Ellen G. White. Watu hao waliendelea kuchunguza makosa
yaliyofanywa na William Miller maana wao pia waliamini juu ya marejeo ya
Yesu tarehe 22/10/1844. Hatimaye mwaka 1863 kanisa hilo likapewa jina
la Seventh –Day Adventists Church huku likiwa na motto au kauli mbiu ya
“Amri za Mungu na imani ya Yesu na Ujumbe wa malaika watatu” na baadaye
kanisa hilo likawa chini ya rais
wa General Conference ya SDA makao makuu yake yakiwa huko Marekani.
Rais huyo ndiye kiongozi (kichwa) mkuu wa kanisa hilo duniani na
huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wakati viongozi wa kanisa
walipokutana ili kujadili mambo ya kanisa, palikuwa na
‘Mwenyekiti’(Chairman of General Conference) ambaye aliongoza kikao hadi
mwisho. Baada ya kikao kumalizika, mwenyekiti huyo alimaliza muda na
kazi yake. Hata hivyo kulitokea mabadiliko kutoka mwenyekiti wa baraza kuu hadi na rais wa kanisa ulimwenguni. Kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kumpata rais
wa kanisa hilo. Tofauti na makanisa mengine, kanisa hili linaabudu siku
ya Jumamosi wakati makanisa mengine yanaabudu siku ya jumapili. Sasa
hivi kuna makanisa mengi ya SDA ambayo yametoka ndani ya kanisa la
‘General conference of Seventh-Day Adventists’(GCSDA) kwa madai kwamba
kanisa hilo limeingiliwa na freemasons. Wengi wa waumini wa SDA
waliojitenga na GCSDA wanasema kwamba walikuwa wakipinga‘protest’
mafundisho machafu huku wakiendelea kuwa ndani ya GCSDA lakini
hawakuweza kuleta mabadiliko yoyote maana hali ilikuwa inazidi kuwa
mbaya. Hatimaye waumini hao waliamua kufuata nyayo za akina Luther za
kujitenga na sasa wanafanya ‘reformation’ au ‘matengenezo’ hatua kwa
hatua maana walitoka na mafundisho machafu ambayo waliyapokea kama kweli
wakiwa ndani ya GCSDA.Waumini hao wanadai kwamba walijitenga na GCSDA
kwa sababu
Je, madai hayo ni kweli? Tafakari!
Msingi
wa kanisa la SDA au ‘Wasabato’ kama inavyojulikana kwa wengi,kuabudu
siku ya jumamosi, ni kile kilichoandikwa na Mungu wakati wa uumbaji,
kwamba aliumba kwa siku 6 na siku ya 7 akastarehe, akaibariki na
akapumzika kisha akawaambia waisraeli: “Ikumbuke siku ya Sabatouitakase….” Kutoka 20:8.
Kutokana
na kazi ya chama cha Priory de Sion kwa kuingiza mafundisho machafu
ndani ya imani safi, kulitokea utitiri wa makanisa mengi ambayo yanadai
kupinga uchafu huo. Hata hivyo wengi wa waumini wa madhehebu hayo ama
hawajui asili ya dhehebu lao au hawajui asili ya kile wanachokiabudu.
Wengi wamefundishwa na waalimu wa dini na kuwaamini bila hata ya kutaka
kuhakikisha kwa akili zao kile wanachofundhishwa. Mungu ametoa nafasi ya
kufahamu ukweli kwa kila mmoja wetu bila ya kutegemea viongozi wa dini.
Umewahi kufikiri kwamba kama ungekuwa unaishi duniani wewe peke yako,
ungemtegemea nani? Tafakari!
UJUE UNDANI WA FREEMASON
HISTORIA KWA UFUPI
Freemason
ni shirika ambalo mambo yake ni siri kuu. Mimi nilifanya utafiki
kwenye mitandao, nikafatilia historia yao kama inavyoonyeshwa mara kwa
mara kwenye makala za historia katika televisheni za magharibi pamoja na
kuongea na watu waliofuatilia kwa karibu mambo yao.
Kwenye maelezo yao kwa nje Free masons wanajitangaza kama shirika zuri tu.
Naomba niorodheshe mambo machache niliyoambiwa kuhusiana na Freemasonry.
1.
Ni kweli Freemasonry kama ilivyo maana yake kwanza ilkuwa ni kundi la
mafundi waashi (masons) au wajenzi kuwa lugha nyingine. Walikuwa ni
wataalamu waliobobea kwenye masuala ya ujenzi wa mahekalu na mabenki ya
zama hizo zinazoitwa kwa kizungu (medieval times).
Niliambiwa
walikuwa ni watunzaji wa pesa za kanisa katoliki. Kwani walikuwa
wanajenga mahekalu(cathedrals) za wakatoliki na mabenki/ mahandaki ya
kuhifadhia pesa pamoja na kuzikia(catacombs).
Niliambiwa
wanaweza kujenga hayo maandaki kwa utaalamu mkubwa kiasi kwamba
ukiingia ndani ya hayo mahandaki bila ramani unaweza ukashindwa kutoka
hata unaweza kupotelea humo humo ndani usiweze kutoka tena. Hicho ndicho
kilichokuwa ni kiwango cha utaalamu wao.
2. Kwa kuwa walikuwa ni waashi ndiyo maana alama zao ni vifaa vya ujenzi, Pima maji n.k
3.
Inasemekana mji mkuu wa marekani (Washington DC) ulisanifiwa na
kujengwa na Freemasons. Na inasemekana ni mji makini ambao umejengwa
ukizingatia pembe tatu zenye nyuzi zinazowakilisha u freemason.
3.
Ikatokea kipindi ambapo hawa freemasons wakaasi kwa kuanza
kujishirikisha na mambo ya nguvu za giza. Wengine wanasema walianza
kuiba pesa za kanisa katoliki, lakini ukweli halisi haujulikani.
Kutokana na sababu hizi na zinginezo ambazo ni siri kati ya kanisa
katoliki na freemasons, Freemasons wakafukuzwa kutoka ukatoliki.
Ndio
maana hakuna maelewano kati ya freemasons na wakatoliki. Wakatoliki
wakaanzisha shirika jingine badala ya hao freemasons lijulikanalo kama
Jesuits.
Jesuit
Fathers ni mapadri wa katoliki wa daraja la juu sana wenye elimu ya juu
zaidi ambao hufanya kazi za siri za utawala na udhibiti ndani ya kanisa
katoliki.
4.Kuhusu
imani yao (freemasons) nikaelezwa kwa kifupi kuwa wanaamini Yesu na
Lucifer ni mtu na ndugu yake. wanaamini kuwa Lucifer ndiye mwema na
mzuri lakini wanaamini kuwa Yesu ndiye mwenye mabaya. alimfanyia hila
Lucifer aonekane mbaya.
4.Kinachoendelea
ndani yake kuhusiana na ibada zake ni siri kwani kuna daraja ambazo
muumini wa freemason anapanda kutokana na kubobea katika imani ikiwa ni
pamoja na kutunza siri zao. Ninajua kuwa daraja ya juu kabisa ni nyuzi
ya 33 (33rd degree)
5.
Kwa hiyo ijapokuwa wanatumia biblia wanapoongelea “Bwana” huwa
hawamaanishi Yesu bali huwa wanamaanisha Lucifer ambaye ndiye
wanayemwabudu.
6. Ni watu wenye nguvu mno na mambo yao ni makubwa mno na siri zao ni nzito mno. Ndiyo maana haziko wazi.
Wafuasi
wa kiwango cha chini wala hawajui shirika hili linahusika na nini
manake hata wao hawaambiwi kitu. Kwa wafuasi wa daraja ya chini
wanakwenda ku socialize tu. Yaani kwa wasio jua kitu kule kwenye lodge
zao ni kama ywca au wmca au club hivi. Kwenye nchi kama marekani watu
wasio jua siri wanachukulia kama sehemu za kusocialize tu.
7.
Freemasonry inawekwa pamoja na makundi mengine makubwa ya siri,
yanayoendesha ulimwengu mzima kwa nguvu za kiuchumi, siasa na mambo ya
utawala.
WALIOSHIRIKI KUPINGA FREEMASON NA UASI WA
LIONS CLUB NA ROTERY CLUB
Kanisa la Katholiki wakati moja waliwahusisha Rotarians (Lions Club) moja kwa moja na Freemasons. Mwaka wa 1928 Maaskofu wa kihispania walitangaza wazi kwamba Rotary Club si chama tu cha kawaida bali ni Muungano au chama kipya cha kuabudu mashetani wakiwa na katiba, tabia na kila kitu chao kufanana na zile za Freemasons wakawatahadharisha waumini wao wajichunge sana na Chama hicho, na baada ya muda mfupi wakuu wa Vatican walitoa amri kwamba maaskofu wa kanisa la katoliki hawaruhusiwi kujiunga na vyama hivyo (Rotary, Lions Club).
LIONS CLUB NA ROTERY CLUB
Kanisa la Katholiki wakati moja waliwahusisha Rotarians (Lions Club) moja kwa moja na Freemasons. Mwaka wa 1928 Maaskofu wa kihispania walitangaza wazi kwamba Rotary Club si chama tu cha kawaida bali ni Muungano au chama kipya cha kuabudu mashetani wakiwa na katiba, tabia na kila kitu chao kufanana na zile za Freemasons wakawatahadharisha waumini wao wajichunge sana na Chama hicho, na baada ya muda mfupi wakuu wa Vatican walitoa amri kwamba maaskofu wa kanisa la katoliki hawaruhusiwi kujiunga na vyama hivyo (Rotary, Lions Club).
Mohammed Sayed Tantawi
Katika
miaka ya 1970 kiongozi wa juu na Sheikh wa Chuo kikuu cha kiisilamu
huko Misri (Egypt) inasemekana alitoa fatwa kuwakataza waisilamu
wasijiunge na chama cha Rotary Club na wakati mambo haya yalikua
yakikatazwa na dhehebu la sunni Chama cha rotary pia kilisikika
kukatazwa na Ayatollah Khomeini.
Ayatollah Khomeini
katika
mwaka wa 1798 Mwandishi Mmoja wa Kiingereza aliejulikana kwa jina la
john Robbinson aliandika kitabu kijulikanacho kama Proofs of a
Conspiracy Against All the Religions and Governments of Europe, Carried
On in the Secret Meetings of Free Masons, Illuminati, and Reading
Societies (Uthibitisho wa njama dhidi ya Dini zote na Serikali zote za
Ulaya ilipangwa katika mikutano ya siri ya Freemasons, Illuminati, na
vyama vinginevyo vya Reading)
John Robbinson
Kitabu hicho kinaelezea Ari na hamasa za Freemason walivyokuwa wakipanga kisiri jinsi ya kupinduwa mipangilio mizuri ya Maisha (Serikali) na ndio waliosababisha mapinduzi nchini Marekani na Ufaransa.
Shuku za kuenea kwa Freemasons zilienea hadi kufikia miaka ya 1800 ambapo
Rais Wa 13 Millard Fillmore wa Marekani
alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la Marekani (Congress) kama mgombea aliyekuwa akipinga mambo ya Freemasons na akafikia kilele katika karne ya 20 (20th Century)
alichaguliwa kwa mara ya kwanza katika bunge la Marekani (Congress) kama mgombea aliyekuwa akipinga mambo ya Freemasons na akafikia kilele katika karne ya 20 (20th Century)
Sergiei Nilus Mwandishi Kitabu cha Protocol
Kitabu
cha The Protocols of the Elders of Zion sio kuhusu mayahudi kutawala
dunia lakini ni kuhusu njama za freemason wa kiyahudi kubadili mfumo wa
dunia.
Hitler Reinhard Heydrich
Hitler alizungumzia kuhusu njama za Mayahudi-Bolshevik-Freemason na kiongozi mwingine wa Ujerumani kwa jina la Reinhard Heydrich aliunda kikosi maalum (Special Section SS) kuangamiza ushawishi wa freemason nchini Ujerumani.
Hitler alizungumzia kuhusu njama za Mayahudi-Bolshevik-Freemason na kiongozi mwingine wa Ujerumani kwa jina la Reinhard Heydrich aliunda kikosi maalum (Special Section SS) kuangamiza ushawishi wa freemason nchini Ujerumani.
Moqtada al-Sadr Al Hawza
Nchini
Irak, Gazeti la Moqtada al-Sadr lijulikanalo kama Al Hawza lilichapisha
picha ya George H.W. Bush na Bill Clinton na akaelezea kwamba ishara ya
mikono yao ilikuwa ni alama ya waandamizi wa kizayoni na freemason, na
kama walivyo Wakatoliki Waisilamu pia waliwahusisha wanchama wa Rotary
moja kwa moja na Freemasons na kusema vyama vyote viwili ni laana.
Rais Bush Rais Clinton
Freemasons
wamehusika moja kwa moja katika jitihada za kutawala Mashariki ya kati
jitahada ambazo zilibuni uhasama kati ya Mashariki ya Kati na Jumuiya ya
Magharibi.
Freemason
walitoa fursa ya wafanyabiashara kuunda mtandao mmoja, hii ni katika
malengo ya wafanyabiashara wanachama wa Freemason wa Ulaya wafungue
ofisi za Freemason nje ya nchi na kuwaalika wanainchi wa Ulaya kujiunga
nao.
Kwa ujumla sio Wafanya biashara wa Wakiingereza au Mashariki ya kati ndio waliowengi tu kama anavyoeleza bwana Hamid Algar wa Berkeley ambaye ni Mwanachuoni maarufu duniani wa historia ya Kiisilamu:-
Hamid Algar
Freemason imeweza kuhudumika katika uisilamu tangu kijitambulisha kwa waisilamu katika karne ya 18 kama njia ya kukuza utawala wa fikra za wa Magharibi kisiasa na kimawazo; Mojawapo wa Ofisi za Freemason huko Istambul nchini Uturuki, ilikuwa na Balozi wa Uingereza kama mkuu
Freemason imeweza kuhudumika katika uisilamu tangu kijitambulisha kwa waisilamu katika karne ya 18 kama njia ya kukuza utawala wa fikra za wa Magharibi kisiasa na kimawazo; Mojawapo wa Ofisi za Freemason huko Istambul nchini Uturuki, ilikuwa na Balozi wa Uingereza kama mkuu
WANACHAMA WA FREEMASONS NCHINI TANZANIA
Sir Andy Chande akiwa na wenzake wakipanda Miti jijini Tanga kama moja ya shughuli zao za kijamii |
Tanzania
ina wanachama hai zaidi ya 600 wa kundi la watu wenye imani ya siri ya
Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa kada mbalimbali wakiwemo
maarufu, huku ikielezwa kwamba miongoni mwao hakuna viongozi wakuu wa
serikali.
Hayo
yalibainishwa na Kiongozi wa kundi la Freemasons katika eneo la Afrika
Mashariki, Jayantilal Keshavji Chande maarufu kama Sir Andy Chande.
Kiongozi
huyo Mtanzania mkazi wa Dar es Salaam mwenye asili ya Kiasia, alisema
licha ya Tanzania kuwa na wanachama hao, kwa sasa idadi ya wanachama
duniani inapungua tofauti na inavyoonekana sasa kuwa wanaongezeka
kutokana na kuibuka maneno mengi kuhusu kundi hilo.
Alisisitiza
kuwa si rahisi kumjua mwanachama wa kundi hilo, bali wenyewe ndio
wanaofahamiana, akisema ni siri na kwamba wenyewe wanakutana katika
vikao mbalimbali mara moja kwa mwezi au zaidi.
Alisema
nchini kuna wanachama zaidi ya 600 wakiwemo wafanyabiashara, watumishi
serikalini, walimu pamoja na wanataaluma mbalimbali wanaoheshimika sana
na kusisitiza kuwa kuna maneno mengi yanayosemwa kuhusu kundi hilo,
ambayo siyo ya kweli.
Alisema
idadi ya wanachama wake duniani inazidi kupungua kutoka milioni nane
hadi sasa wako milioni sita, tofauti na wengi wanaodhani kuwa idadi hiyo
inaongezeka.
Chande
alizungumza na mwandishi wa habari hizi katika Shule ya Sekondari ya
Shaaban Robert ambako yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule alipozungumzia
maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema
duniani kuna watu wazito wengi ambao ni wanachama wa kundi hilo kama
majaji wakubwa na hata Binamu wa Malkia Elizabeth wa Uingereza ni
kiongozi mkubwa wa kundi hilo.
Akizungumzia
masharti ya kujiunga na kundi hilo, Chande alisema ni lazima mwanachama
huyo awe anaamini katika Mungu bila kubagua iwapo ni Mkristo au
Muislamu.
Alisema
pia ni lazima anayetaka kujiunga awe na umri unaozidi miaka 21 na walio
chini ya umri huo hawaruhusiwi kujiunga na lazima familia ya anayetaka
kujiunga na wanandugu wafahamu kuwa umejiunga na kundi hilo.
“Unajua
katika imani hii kuna michango mbalimbali ambayo unatakiwa kutoa ambayo
ni zaidi ya dola milioni sita (karibu Sh bilioni 10), hivyo ni lazima
ndugu wafahamu ili kuepuka matatizo utakapotakiwa kutoa,” alisisitiza.
Alisema
si kweli kuwa wenye fedha wengi ni wanachama wa kundi hilo huku
akikanusha wanachama wanajiunga kwa ajili ya kupata fedha, bali ni dini
kama imani nyingine.
Alisisitiza
kuwa hakuna ukweli kwamba wanaopata mafanikio katika maisha wakiwa
ndani ya imani ya Freemasons kuwa wanatoa kafara watu wao wa karibu kwa
lengo la kupata utajiri.
Chande
pia alisema hairuhusiwi kutumia jina la kundi hilo kwa nia ya kujipatia
nafasi sehemu mbalimbali au kuongeza nafasi katika chuo au shule.
No comments:
Post a Comment