Kanisa la Parokia ya Kaning'ombe
Askofu Mkuu wa Jimbo la Iringa Tarcisius Ngalalekumtwa
Baba Askofu akielekea altare Shemasi Victorino Kalinga Aliyepata daraja la Upadre
Baba Askofu akiwa Tayari kumtunuku daraja la upadre Shemasi
Victorino Kalinga
Hapa anapewa upadre
Hapa Tayari ametunukiwa daraja la Upadre
Mmiliki wa mtandao huu ndugu Lewis Mbonde katikati mwenye koti nyekundu akiwa kazini na Thobias Myovela wa Radio Maria kushoto na Gustav Chahe Kulia aliyesimama mmiliki wa Gustav Chahe blog
Na Gustav Chahe,Lewis Mbonde na
Thobias Myovela Iringa
RAIS wa
Baraza la Maaskofu Tanzani Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka watu
wasiwe wasanii kwa kutumia jina la Mwalimu Nyerere kuwa wanamuenzi huku
wakifanya mambo ya ajabu ya unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za watu.
Aliyasema
hayo katika maadhimisho ya Misa utoaji wa daraja la Upadre kwa Shemasi
Victorino Kalinga iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya Yubilei ya Miaka 75 ya
Parokia ya Kaning’ombe jimbo Katoliki la Iringa.
Askofu
Ngalalekumtwa ambaye pia ni askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa alisema,
kutokana na usanii wa watu wanaojifanya wanamuenzi hayati Baba wa Taifa Julius
Nyerere huku wakifanya mambo ya kihuni ipo siku uongo wao utawatokea puani.
“Ipo siku
mtasema mnamuenzi halafu mmkute ameketi juu ya kaburi sijui mtasema nini? Nyie
watu wadanganyifu mnaotumia jina la Mwalimu Nyerere, acheni usanii, uhuni na
uongo kuwadanganya watu wenye akili” alisema.
Alisema kuwa
si kila mtu amefirisika kifikra na kwamba watu wanajua kila kitu kinachoendele
kuwa ni uongo au ukweli.
Alisema
binadamu wa leo ametoka nje ya matakwa ya Mungu na kufanya mambo yasiyo stahili
kwa kutenda dhambi kwa kujifanya wema huku wakiwaumiza wenzao.
Aliwaasa
Wakristo kuwa wajumbe wa habari njema kwa ajili ya kulinda amani ambapo
wanatakiwa kumtafuta Mungu kwa ajili ya wokovu.
“Maaskofu na
Mapadre wameteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufungua mioyo ya watu ili waweze
kumtafuta Mungu na kuufifikia wokovu wa wa milele.
“Mungu
mwenye upendo, huruma na msamaha ni Yule tunayehitaji kuajikabidhi maisha yetu
kwa ajili ya furaha ya milele” alisema askofu Ngalalekumtwa.
Hata hivyo
alisema Padre anapasika kuwa na msimamo usio na lawama ili asije akachakachua
maagizo ya Mungu na kujitunza nafsi yake kwa ajili ya kuwa muangalizi mwema wa
kondoo alioachiwa na Mungu.
“Padre awe
na msimamo safi na awe na akili kichwani ili apate kubaini kufichua na kukemea
yale ambayo hayastahili yanyowafanya wana wa Mungu kuishi kwa hofu. Padre ni
mjumbe wa amani ambaye anatakiwa kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya kuishi kwa
upendo, mshikamano na kuwahurumia wengine” alisema.
Alisema kuwa
pamoja na purukushani zote zilizopo, bianadamu ana kiu ya Mungu ambayo padre
anatakiwa kuizima kiu hiyo.
Alisema kuwa
wakristo wanatakiwa kukusanyika pamoja na kutoa dua kwa Mungu ili kuliombea
Taifa linaloingiliwa na watu wasio na mapenzi mema wanaopenda kuwasambaratisha
watu wasio kuwa na hatia.
Miaka 75 ni
heshima tuliyopewa na Mungu kwa ajili ya kutangaza uweza wake kwa mataifa
ambayo bado hayajamfahamu.
“Miaka 75
iwe ishara ya kuendeleza na utamaduni wetu wa upendo aliotuachia Kristo Mwokozi
kwa ajili ya maisha yetu. Lindeni hayo ili Mungu Mwenyezi azidi kutulinda
katika ukamilifu wa upendo, mshikamano, huruma, hekima, busara na amani”
alisema.
Kanisa
lazima litoe lishe kwa watu wake ili miili yao isishambuliwe na magonjwa ya
dhambi. Kwa njia ya padre, binadamu watapata faraja ya Mungu kwetu tunaoishi
katika bonde la machozi.
Maadhimisho
ya upadre yalikwenda sambamba na maadhimisho ya Yubilei ya miaka 75 ya Parokia
ya Kaning’ombe ambapo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiroho na
serikali ndani na nje ya jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment