Wednesday, December 26, 2012

HII NDIO AJALI MBAYA YA BASI NA LORI USO KWA USO LEO MBEYA.

Unaambiwa zaidi ya abiria 40 wamenusurika kifo hapa, hili basi lilikua linatoka Mbeya kwenda Dar es salaam na limegongana na lori uso kwa uso sehemu inaitwa PIPE LINE INYALA, mwenye makosa anatajwa kuwa dereva wa lori alielipita gari jingine kwenye kilima na kukutana na basi uso kwa uso.
Dereva wa lori kakimbia baada ya ajali.
.
Huyu mtoto kasimulia na kusema alikua nyuma ya dereva kabisa na kilichomsaidia ni kufunga mkanda, mama aliyekua kakaa nae jirani ameumia sana kwa sababu hakufunga mkanda.
.
.
.
Baadhi ya majeruhi. (Picha zote zimepigwa na mbeyayetu.blogspot.com)

No comments: