Wednesday, December 12, 2012

HUYU NDIO BIBI WA MIAKA 60 ALIYEUA JAMBAZI KWA RISASI BAGAMOYO.


.
Mara nyingi taarifa ya jambazi kuuwawa na mwanaume ni kitu cha kawaida lakini kwa jambazi kuuwawa kwa risasi iliyopigwa na mwanamke tena bibi mwenye umri wa miaka 61 anaekaribia 62 ni kitu kikubwa sana.
Jumapili december 9 2012 nilisafiri mpaka Bagamoyo kufanya mahojiano na bibi ambae ijumaa iliyopita alivunja rekodi ya stori za ujambazi kuingia kwenye habari kumi za AMPLIFAYA ya CLOUDS FM kutokana na kumuua jambazi mmoja kati ya nane waliomvamia nyumbani kwake, baada ya kumuua huyo mmoja wale wengine waliobaki wakakimbia.
Sikiliza AMPLIFAYA ya leo kuanzia saa moja kamili usiku CLOUDS FM ambapo utamsikia mwenyewe akiongea na pia endelea kuitembelea millardayo.com ambapo video yake na picha za eneo la tukio na jambazi alieuwawa nitaziweka hapa, kwa taarifa za haraka zaidi unaweza kujiunga na mimi kwenye twitter.com/millardayo facebook.com/millardayo
.

No comments: