Friday, December 7, 2012

270 wafariki katika kimbunga Ufilipino


 
Athari za kimbunga Bhopal nchini Ufilipino

Zaidi ya watu mia mbili sabini wamethibitishwa kufariki katika kimbunga kikali kinachoendelea kusababisha uharibifu kusini mwa Ufilipino.
Wengine wengi hawajulikani waliko. Nusu ya walioathiriwa walikuwa ni wakaazi katika maeneo ya milima walioathirika na maporomoka ya udongo baada ya kuyakimbia makaazi yao ili kwenda kwenye maeneo yalio salama.
Katibu mkuu wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo, Gwendolin Paang, ameiambia BBC kuwa idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la AP Miili zaidi ya 270 ya watu waliofariki katika kimbunga hicho ilipokelewa katika maeneo yalioathiriwa na kimbunga hicho kusini mwa ufilipino.
Kwa mujibu wa maafisa nchini humo huenda miili zaidi ikapatikana katika maeneo mengine ambayo kwa sasa waokoaji wanaendeleza shughuli za uokozi.
Katika mkoa wa Compostela zaidi ya watu 151 wakiwemo wanajeshi na wenyeji wameripotiwa kufariki katika mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga hichi cha bopha .
Zaidi ya watu 80 waliponea kimbunga hicho lakini wengi bado hawajulikani walipo na wengine zaidi ya elfu 45 wakikosa makao.
Idadi ya vifo hivi vimetokea licha ya rais wa ufilipino Benigno Aquino kutaka raia wa ufilipino kuhamia maeneo yaliyo salama. Nchi ya ufilipino hukumbwa na zaidi ya vimbunga 20 kila mwaka

No comments: