Tuesday, August 27, 2013

HUYU NDIYE MSELA ALIYEMFUNIKA LIL WAYNE KWA TATOO, JAMAA ACHORA TATOO HADI KWENYE MENO:


Matthew Whelan

'Human branding' ambayo inajulikana pia kama 'scarification',ndo kitu kinachoongoza sasa hivi kwenye sanaa ya kujichora mwilini na mbritish mwenye tatoo nyingi kuliko wote hakutaka kuachwa nyuma na style hiyo mpya. Matthew Whelan,33, kutoka Birmingham hajajifunika mwili wake kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni  tu na sanaa ya ngozi bali hadi jicho lake moja jeupe kalitatoo na kuwa jeusi. Hicho kifaa kilichotumika kumtatoo kinatumia nguvu ya umeme kuunguza kwenye nyama  na ndo kifaa hicho hicho kinatumika na madaktari wa meno au surgeons kuunguza seli za kansa. Angalia picha chini:



Matthew Whelan


Matthew Whelan


Matthew Whelan
Lest Westwood, mchora tatoo aliyemchora alisema "Huwa inanukisha studio yote mwili wake unapoungua na kuna hatari pia ambazo zinaambatana na kujitatoo hivi, mwili unaweza ukapata shock".
 
Mr Whelan alikua na miaka 9 tu alipoanza kutamani sana tatoo. Tangia hapo alitumia masaa 300 kwenye kiti cha  wachora tatoo na alitumia zaidi ya euro 20,000 kujipamba mwili wake. Designs zake zilitoka kwenye maumbo ya nyoka,ng'e(scorpions) na mavampire hadi jina la TV program anayoipenda sana ‘The Jeremy Kyle Show’ alijitatoo nayo kwenye kisogo chake.
Hapo hapo, Whelan ambaye amebadilisha jina lake kisheria na kujiita 'His Royal Majesty Body Art,King of Ink Land' alisema anapenda kujifikiria kuwa yeye ni kipande cha sanaa kinachopumua na kuishi....


Matthew Whelan
Add caption
Matthew Whelan

No comments: