Saturday, August 31, 2013

HII NAYO KALI BALOTELLI AAMUA KUFUGA NGURUWE TOFAUTI NA MASTAA WENGINE WANAOFUGA MBWA




WAKATI watu wengine wanafuga mbwa au paka kama wanyama rafiki, mchezaji mtukutu Mario Balotelli ameamua kufuga nguruwe.

Katika ununuzi wake wa ajabu hivi karibuni, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia, alishangaza watu kwa mara nyingine tena kwa staili yake ya masiha baada ya kununua mtoto wa nguruwe.

Akitupia picha kwenye mtandao wa Twitter, Balotelli akawaambia wafuasi wake milioni moja katika mtandao huo: “Hatimaye nguruwe wangu mdogo amewasili, ana umri wa miezi miwili, ni wa kike lakini nimemuita SUPER!”.

Alikuwa akikumbukia jina lake la utani Super Mario alilopewa wakati akiwa Manchester City.

Ilionekana kuleta mchanganyiko kidogo watu wakiwa hawajui iwapo rakiki yake huyo mpya ni mwanamke au mwanaume.

Nyota huyo wa miaka 22 akaandika: “Hakika nimeshindwa kubaini hivyo nadhani ni mwanamke ahahahaha lakini pia pengine ni mwanaume Ahahah.”

Inaaminika nguruwe huyo atajizolea umaarufu mkubwa ndani ya jiji la Milan.

No comments: