IMG_7080
Mkuu wa Kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara wa Kampuni ya Rockstar 4000 Bi. Christine Mosha “Seven” akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo ambapo amesema amefurahishwa sana kufanya kazi na Orijino Komedi ambao ni watu wenye vipaji vya hali ya juu na kuingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency ambapo kwa pamoja wamedhamiria kukuza na kubadilisha dhama ya vipaji na sanaa kutoka ilipo na kuwa ya kimataifa. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Nexus Agency Bw. Bobby Bharwani na kulia ni Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi Sekioni David.
IMG_7083
Mkurugenzi Mkuu wa Nexus Consulting Agency Bw. Bobby Bharwani (kushoto) akieleza kuwa kwa upande wa kampuni yao kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao kutokana na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa kundi hilo.
IMG_7051
Picha ya pamoja kati viongozi wa makampuni ya ‘Nexus Consulting Agency’ na ‘Rockstar 4000′ na wasanii wa kundi la Orijino Komedi mara baada ya kutolewa kwa taarifa ya kundi hilo kuingia mkataba na makampuni hayo.
Kundi la kipaji cha Televisioni “Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa vipindi vyake kupitia televisionilimeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa kushirikiana na Rockstar 4000, ambao utakuwa ni mkataba wa kwanza kwa wasanii wa luninga kupitia kampuni ya Nexus.
Nexus imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo linajulikana sana nchini kupitia vichekesho vyake vinavyoonyeshwa na vituo vya television na matamasha mbalimbali, ambapo mkataba huo utakuwa ni kwa ajili ya kusimamia kipindi hicho cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji saba ambao ni Joti, Macreagan, Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Vengu na Seki David ambacho kimekuwa hewani kwa mfululizo wa miaka sita.
Kwa kushirikiana na Rockstar 4000, Nexus imesema itahakikisha inaendeleza vipaji vya wasanii wa kundi hilo ili vipaji vyao viweze kufikia kiwango cha juu cha ufanisi ndani ya Afrika na Kimataifa kwa ujumla.