MITANDAO ya kijamii imekuwa ni njia
nyepesi ya kuwasiliana na kujifunza mambo mbalimbali ya kimaendeleo
yanayofanyika ndani na nje ya nchi.
Mitandao hii imefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kuteka akili za watu wa rika zote wadogo kwa wakubwa, kila mtu
akitumia mitandao kulingana na dhumuni, mahitaji na akili zake
zinavyomtuma.
Ilivyo sasa ni kwamba mitandao hii
imekuwa huru kwa kiasi kikubwa hali inayochochea mmomonyoka wa maadili
kwa jamii hasa watoto wadogo wanaoingia kwenye mitanadao hiyo wakiwa
hawana usimamizi wa kuwaongoza kuangalia kipi na wasiangalie lipi.
Sipingani na matumizi ya mitandao
hiyo kwani ndiyo maendeleo tunayoyatafuta ila umefika wakati wa
kuangalia na kuzingatia mambo yanayopaswa kufanyika kwa lengo la
kuepusha usumbufu ama kutokuelewana kwa jamii ya watanzania.
Wapo wanao tumia mitandao hii kwa
kujifunza na kujipatia maarifa, pia wapo baadhi ya watumiaji na tovuti
zenye lengo la kupotosha jamii na kusababisha lawama na usumbufu kwa
watu binafsi ama taasisi za umma.
Naeleza wazi kuwa hizi jitihada zetu
za kugeuza dunia kuwa kijiji kwa Tanzania zimeanza kuonesha madhara
ikiwemo wizi kwa njia ya mitandao, mmomonyoko wa maadili kwa jamii pia
kudhalilishana jambo ambalo ni kinyume na utamaduni wetu ma lengo la
kuwepo mitandao hiyo.
Mambo haya hayajaishia hapo kwani
kila kukicha mambo yanaendelea kuongezeka kwenye mitandao, imefikia
hatua ya kuwadanganya wananchi kuchukua machapisho kwenye tovuti
nyingine na kuondoa au kuongeza baadhi ya maneno hali inayosababisha
lawama baina ya pande mbili.
Ukweli wa mambo ni kuwa hivi karibuni
Watanzania wametakiwa kujihadhahari na mitandao ya kijamii inayo andaa
matangazo yanayohusiana na mchakato wa ajira katika utumishi wa umma
kwani matangazo hayo si ya kweli.
Pamoja na Serikali kupitia Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (Tcra) kutanga kuwachukulia hatua za kisheria
wamiliki wa mitandao wanaotoa habari za kughushi bado wamiliki hao
wamekuwa na uthubutu wa kuchukua matangazo katika tovuti za Serikali na
kuyahariri kisha kuyabandika kwenye kurasa zao bila woga.
Watu wanafanya hilo kwa makusudi
lengo ni kupotosha umma huku wakijua wazi kuwa taarifa hizo
wanazochapisha au kuziandika katika mitandao hiyo ya kijamii si sahihi
na hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira.
Wanao tumia mitandao kupotosha waadhibiwe
Tangu July 4, 2013, na | Imesomwa mara 4 | Haina maoni
Prof-Makame-Mbarawa[1]
Na Joyce Ngowi

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira,
Xavier Daudi ndiye aliyesikika akilalamika kuhusu mitandao hiyo na
kuitaja baadhi ikiwemo ule wa www.eastafricajobscareer.com ambao umetoa
matangazo yanayoonesha mwisho wa kupokea maombi ni Julai 14 na Ogasti 10
mwaka huu.
Hadi sasa ni alimia 10 tu ya
Watanzania ndio tunaotumia mitandao hiyo tupo wachache lakini
tunaudanganyifu mwingi hivi tukifika asilimia 44 kama wenzetu wa Kenya
tutakuwa upande gani? Pia tunapaswa kujiuliza na kutafuta majibu ya
msingi kwa nini tunadanganya.
Tabia hii iachwe mara moja inaweza
kuleta mafarakano katika jamii kwani dunia ya sasa kazi imekuwa ni
bidhaa adimu kwa dunia nzima hivyo mtu anaposikia nafasi za kazi hasa
katika sekta za umma akili na mawazo ya mhusika yanahamia juu ya
mchakato wa upatikanaji wa ajira yenyewe, hivyo mtu anatumia muda mwingi
kuhangaikia jambo lisilo la kweli. Hali hiyo haipendezi.
Pamoja na kuwataka wananchi wote
kufahamu kuwa Sekretarieti hiyo ndiyo chombo pekee kilichoundwa kwa
mujibu wa sheria kushughulikia mchakato wa masuala ya ajira katika
utumishi wa umma itakuwa ni kazi nyingine hasa wasiofuatilia mambo na
kujiridhisha ikiwa tangazo ni la kweli au si halali.
Ikiwa watu hawa wanakuwa na jeuri
hata ya kuingilia shughuli za Serikali itakuwaje kwa wananchi na wale
wasio na ufahamu wa mitandao wala njia za kujilinda.
Nionavyo ni kwamba usumbufu
unaotoakana na matangazo ni kuwasababishia wananchi kero zisizo na
msingi ambao wengi wao wanatafsiri kuwa Tume ya Ajira inatangaza nafasi
za kazi na nafasi hizo zilisha kuwa na watu hivyo fursa hiyo imetumika
kuhalalisha waliopewa nafasi hiyo.
Jambo hili linaweza kuleta msigano
pande zote kwani kila mmoja atajiona yupo sahihi kwa nafasi yake hivyo
wananchi wataiona Tume hiyo haiwatendei haki au kuelewa kuwa nafasi hizo
zinapatikana kwa njia zisizo halali ilhali usaili unafanyika kwa
kuzingatia vigezo vya muombaji na mahitaji ya nafasi zilizopo.
Wamiliki wa mitandao mnawajibu wa kusimamia mitandao yenu ili kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu kupitia kwenye tovuti zenu.
No comments:
Post a Comment