Timu za Taifa za Malawi na Kenya zimetoka sare kwa kufungana mabao 2-2 mjini Blantyre katika mechi ya kufuzu kombe la dunia.
Malawi
ndio walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1 lakini katika dakika ya mwisho
Chimango Kayira alijifunga na kupunguza uwezekano wa Malawi kusonga
hatua inayofuata.
The
Flames ndio waliowa kuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 46,
bao lililofungwa na Robion Ngalande, lakini dakika sita baadaye Mohamed
Jamal akaisawazishia Harambee Stars.
Katika
dakika ya 81, Robert Ng'ambi alifunga bao la pili kwa Malawi, kabla ya
Kayira kujifunga na mechi kumalizikia mabao mawili kwa mawili.Matokeo
hayo yana maana kwamba mabingwa wa Afrika Nigeria ndio watakaofuzu
hatua inayofuata kutoka kundi F, ikiwa wataishinda Namibia mjini
Windhoek, mechi inayochezwa baadaye usiku huu.
Hadi kufika leo kumebakia mwaka mmoja, kabla ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kuanza nchini Brazil.
Mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi
na babake wanachunguzwa nchini Hispania kwa kuilaghai serikali ya nchi
hiyo zaidi ya pauni milioni tatu nukta nne.
Mchezaji huyo kutoka Argentina na
babake, Jorge wanatuhumiwa kuibia serikali ya nchi hiyo, kwa kujaza fomu
zisizokuwa za ukweli za marejesho ya kodi kati ya mwaka wa 2007 na
2009.Hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hajasema lolote kuhusiana na madai hayo.
Messi hulipwa Euro milioni kumi na sita kila mwaka na ndiye mchezaji anayelipwa kiasi cha juu zaidi duniani.Lakini
mwendesha mashtaka Raquel Amado, aliwasilisha nyaraka za mahakama
nyumbani kwake kwa mchezaji huyo katika mtaa wa kifahari wa Gava mjini
Barcelona.
Jaji mjini humo ni sharti waidhinisha malalamishi dhidi ya mshukiwa yeyote kabla hajafunguliwa mashtaka.Messi
na babake wanashukiwa kutumia kampuni katika mataifa ya ngambo, mjini
Belize na Uruguay kuuza haki za kutumia picha ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo na babake wanatuhumiwa
kutumia kampuni hizo zilizoko nje ya Hispania, ambako anaishi na kucheza
soka ya kulipwa, kukwepa kulipa kodi inayokisiwa kuwa pauni milioni
tatu na nusu.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akifafanua jambo wakati wa
uzinduzi wa Kili Music Tour 2013 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kala
Jeramiah na Nasssib Abdul 'Diamond'.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul 'Diamond' akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu ziara ya wasanii kwenye mikoa 8, ambapo jumla
ya wasanii 24 watashiriki.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Kala Jeramiah akizungumzia ziara ya wasanii.
Chazi Baba akitoa vionjo vya moja ya nyimbo zake.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akiteta jambo na, Diamond na Chaz
Baba wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kili Music Tour
2013.
Profesa
J akiwashukuru wale wote waliompigia kura pamoja na kuwasihi wasanii
tutokata tamaa na kujipanga vizuri katika tuzo za mwakani ili waje
kung'ara.
Timu
ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati yao na
wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Jamhuri
hapa Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB imekabidhi jezi
kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata na shoka ambao
umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili.
Mheshimiwa
Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge
na NMB kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate.
Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki
saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mheshimiwa
Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka kwa nahodha wa
timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote zinatarajiwa
kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.
Javier Mascherano ameomba radhi kwa
kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwendesha gari ya kutolea
majeruhi kiwanjani katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya
Ecuador.
Kiungo
huyo wa Barcelona, ambaye aliwahi kuchezea Liverpool na West Ham,
alitolewa baada ya kumpiga dereva wa gari ya kuondolea wachezaji
majeruhi kiwanjani katika dakika ya 87.
Mascherano,
ambaye alikuwa nahodha wa timu hiyo kwa usiku huo, baadae alisema kuwa:
'Hakuna mtu anayependa fujo nchini kwetu nilifanya makosa naona aibu
kwa kufanya vile .
mwendesha
gari alikuwa anakwenda kwa kasi kubwa sana ilikuwa bado kidogo
nidondoke.Nilimkanya (Dereva) lakini alidharau, lakini nilichofanya
hakikuwa kitendo cha kiungwana.‘Ninaelewa umuhimu wa mimi kuomba radhi na nimefedheheshwa na kwa masikitiko nimeomba radhi.’
Kwenye mtandao wa Twitter,: 'Nakiri nimefanya kitendo kibaya, hakielezeki.Baada ya kuumia , mwendesha gari alikuja kunichukua kama sheria inavyotaka japokuwa
kiungo huyo, alianzisha fujo kama alivyokuwa akionekana kwenye Tv .na
picha za runinga zilionyesha , Mascherano akiwa anapiga makelele kwa
wahudumu wa huduma ya kwanza .
Mkuu wa Kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara wa
Kampuni ya Rockstar 4000 Bi. Christine Mosha “Seven” akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo ambapo amesema
amefurahishwa sana kufanya kazi na Orijino Komedi ambao ni watu wenye
vipaji vya hali ya juu na kuingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting
Agency ambapo kwa pamoja wamedhamiria kukuza na kubadilisha dhama ya
vipaji na sanaa kutoka ilipo na kuwa ya kimataifa. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa Nexus Agency Bw. Bobby Bharwani na kulia ni Muandaaji wa
vipindi vya Orijino Komedi Sekioni David.
Mkurugenzi Mkuu wa Nexus Consulting Agency Bw. Bobby
Bharwani (kushoto) akieleza kuwa kwa upande wa kampuni yao kushirikiana
na Orijino Komedi ni kitu muhimu kwa Nexus kwani siku zote imekuwa
ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao
kutokana na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa
kundi hilo.
Picha ya pamoja kati viongozi wa makampuni ya ‘Nexus
Consulting Agency’ na ‘Rockstar 4000′ na wasanii wa kundi la Orijino
Komedi mara baada ya kutolewa kwa taarifa ya kundi hilo kuingia mkataba
na makampuni hayo.
Kundi la kipaji cha Televisioni
“Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa vipindi vyake kupitia
televisionilimeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa
kushirikiana na Rockstar 4000, ambao utakuwa ni mkataba wa kwanza kwa
wasanii wa luninga kupitia kampuni ya Nexus.
Nexus imenunua haki zote za
usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo linajulikana sana
nchini kupitia vichekesho vyake vinavyoonyeshwa na vituo vya television
na matamasha mbalimbali, ambapo mkataba huo utakuwa ni kwa ajili ya
kusimamia kipindi hicho cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji saba
ambao ni Joti, Macreagan, Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Vengu na Seki
David ambacho kimekuwa hewani kwa mfululizo wa miaka sita.
Kwa kushirikiana na Rockstar 4000,
Nexus imesema itahakikisha inaendeleza vipaji vya wasanii wa kundi hilo
ili vipaji vyao viweze kufikia kiwango cha juu cha ufanisi ndani ya
Afrika na Kimataifa kwa ujumla.
Kiingilio cha chini katika mechi ya
mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast
(The Elephants) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.
Viti
vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000
viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni
sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897
ni sh. 10,000.
Viingilio vya daraja la juu ni kama
ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000
ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748
kiingilio chake ni sh. 30,000.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo
itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili kabla ya
mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari
Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa
Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala
na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Katika
vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia
yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Tunapenda kuwakumbusha
watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo
yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya
kushuhudia mechi hiyo.
Utaratibu
katika mechi hiyo utakuwa kama ilivyokuwa katika mchezo wa Simba na
Yanga, ambapo hayataruhusiwa kuingia uwanjani isipokuwa kwa yale
yatakayokuwa na sticker maalumu kutoka TFF.