Saturday, January 5, 2013

USISHANGAE, HII NDIO CLUB YA WAVUTA BANGI ILIYOFUNGULIWA MAREKANI.

Hii stori kutoka CNN ikufikie kwamba huko Colorado Marekani imefunguliwa club ya wavuta bangi ambayo imeruhusiwa, ni wanachama tu wanaoruhusiwa kwa kulipa dola 30 ambazo ni zaidi ya elfu 40 za kitanzania, umri wa kuruhusiwa ni kuanzia miaka 21.
Katika Club hii inayoitwa Club 64 hauwezi kununua bangi ndani ya club lakini unaweza kwenda na ya kwako na ukashare na marafiki na mkavuta kwa pamoja, ni uhuru wa wavuta bangi ambao mmiliki wa Club anasema unampa nguvu ya kutimiza malengo yake mengine kama haya aliyonayo na wala hana cha kuogopa.

No comments: