Monday, January 7, 2013

SENTENSI 5 ZA ROMA MKATOLIKI KUHUSU UHUSIANO WAKE NA KUNDI LA KINA JOH MAKINI.

Roma Mkatoliki.
Rapper Roma Mkatoliki ambae ni mzaliwa wa 96.0 Tanga ameitii kiu ya mashabiki wengi wa hip hop waliotaka kujua siku akifungua kinywa chake kuhusu kundi la WEUSI atasema nini.
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Roma amejibu maswali machache mazito kuhusu WEUSI ambao wengi waliamini kama ana beef nao.
Wakati akiizungumzia single yake mpya ya 2030 Roma alitumia hiyo nafasi pia kuweka wazi kwamba haba beef wala chuki na kundi la Weusi na kama vile haitoshi akatolea mfano status aliyoiandika kwenye page yake ya facebook siku kadhaa kabla ya kuwasifia WEUSI kwa show yao ya mwaka pale Maisha Club.
Joh Makini na Nikki wa II siku ya show december 23 2012.
Japo anasema baada ya kuiandika hiyo status kuna ambao walimuunga mkono na waliompinga, namkariri akisema “kuna waelewa na wasio waelewa… mara nyingi tumfatilishe yule muelewa, kitu kikiwa kizuri mimi ni mtu wa kukubali, ndio hivyo nilivyoumbwa haiwi kwa njia ya unafiki au kwa kutafuta kitu kingine chochote, ile show ya WEUSI ilikua kali mi Maisha Club nakwenda sana kwenye show nyingi lakini ilikua ni show nzuri jinsi ilivyopangiliwa, haikupata watu wengi sana kama nilivyotarajia lakini hata waliofika inatosha, kikubwa nilichokipenda ni show ambayo haikumuhusisha msanii mwingine yeyote… walifanya show nzuri kuanzia Lord Eyez, Nikki, Bonta, G alitisha sana Joe mwenyewe alifanya vizuri, haikuniboa hata kidogo”
“Jana yake usiku kabla ya show nilikua nao kina Lord na G nikapiga nao stori lakini once wanapofanya mistake kwenye game unagundua hapa wamekosea hilo pia sitalifumbia macho nitaweza kuliongea, kama unakuta 50 na Jay Z wanabeef lakini tunashangaa 50 anapoperform Jay Z anaamka kwenye kiti kabisa anapiga makofi anaonekana ana mzuka, mawazo ya watu tu kwamba labda watu wakiwa na utofauti basi siwezi kukubali mtu akifanya vizuri, mbali na hivyo vyote nilivyoviongea hakuna matatizo kati ya Roma na wale watu, najiona niko sawa sina matatizo na mtu yeyote mbali hata na wale pale” – Roma Mkatoliki
Hii ndio status ya Roma Mkatoliki dec 13 2012.

MAGAZETI YA LEO JAN 7 NDIO HAYA NA STORI KUBWA ZA MICHEZO NA HARDNEWS.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

PICHA 6 ZA STUDIO MPYA YA CLOUDS FM!!

Hii ilikua siku ya uzinduzi wa kamanda mpya anaetoa kibali kwenye spika za kila mwanafamilia wa CLOUDS FM Dar es salaam, anaitwa 88.5
Hii studio ina sehemu ya kisasa ya kupumzikia, sehemu ya vinywaji pamoja na mitambo ya kisasa kabisa.
.
.
.
B12 na Geah Habib wakimsikiliza Mkuu wa vipindi Clouds Fm my bro Sebastian Maganga.
Unaweza kuisikiliza CLOUDS FM kupitia 88.5 ukiwa Morogoro, Singida ni 89.8, Mwanza 88.1, Shinyanga 87.5, Arusha 87.9, Moshi 87.9, Tanga 96.0, Dodoma 104.4, Mbeya 87.8, Mtwara 88.4, Pwani 88.4, Mara 98.6, Lindi 89.7, Masasi 88.5, Manyara 104.4, Iringa 92.9, Tabora 88.0, Kigoma 89.3 pia online kupitia cloudsfm.co