Mpenzi
msomaji wa safu hii, juma lililopita tuliona na kujifunza baadhi ya dalili za
mpenzi asiye na penzi la dhatiu kwako, hii tunajikita kujua walau faida tisa za
kufanya ngono.
Ngono
au tendo la ndoa lina faida kubwa katika mwili wa binadamu ambazo ni zaidi ya
kustarehesha ama kustareheshwa hasa linapofanywa na watu wazima na tendo hilo ukizidisha unaweza
kupata madhara kiafya .
1.
Mzunguko
wa Damu.
Tendo
la ndoa huongeza kasi ya mzunguko wa damu mwilini kutokana na kuongezeka kwa
mapigo ya moyo ambayo huboresha mzunguko huo wa damu pale unapopumua wakati wa
kufanya tendo hilo.
2.
Mazoezi
ya mwili.
Watu
wengi hawafanyi mazoezi lakini kufanya ngono ni moja ya mazoezi ya mwili ambapo
unatakiwa kwa wiki moja asizidishe kufanya ngono mara tatu jambo ambalo
litakusaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini pia ukifanya hivyo kwa kipindi
cha mwaka mmoja ni sawa na kukimbia maili 75 na tendo hilo huongeza karibia
vizalisha nguvu 150 kwa nusu saa ambayo ni sawa na kukimbia dakika 15 uwanjani.
3.
Maumivu
Unapofanya
mapenzi homoni iitwayo oxytosin huzalishwa mwilini ambayo hupelekea kuzalishwa kwa
homoni iitwayo endorphin ambazo huwezesha kupunguza maumivu mwilini ikiwemo
uvimbe, maumivu ya shingo na kichwa ambapo ukiona vitu hivyo vinakusumbua fanya
mapenzi.
4.
Mafuta
yenye kileo
Huweka
uwiano wa mafuta yenye kileo (Cholesterol) nzuri na mbaya na hupunguza kwa
uwiano sawa kiasi cha mafuta mwilini.
5.
Huondoa
Maji yenye madhara
Tendo
la ndoa la mpangilio huondoa uzalishaji wa majimaji yanayozalishwa kwenye
prostate ambayo huwa na madhara kwa binadamu.
6.
Usingizi
mnono
Hakuna
ubishi kwa yeyote aliyewahi kufanya ngono kuwa aliwahi kupata usingizi mnono
isivyo kawaida hasa baada ya shughuli ambayo hata mnyama Simba angeingia mahala
hapo pa faragha hakuna hata mmoja ambaye angeweza kuacha tendo hilo na kumkimbia Simba.
Kufanya
mapenzi na kuupumzisha mwili kabla ya kuanza tena tendo hilo hasa kwa wanaume ni jambo muhimu ambapo
utaupa mwili auheni ya kutuliza akili na kurekebisha mzunguko wa damu mwilini ambapo baadaye ukitaka kulala
utalala swadakta…….
7.
Kudumisha
ujana
Homoni
iitwayo DHEA huzalishwa mwilini ambayo husaidia msisimko kuongezeka ambapo
mwanadamu anayefanya mapenzi huongezewa ufahamu, kuimarisha mifupa, mishipa ya
moyo na hata kuzuia wapinzani wa kazi za mishipa ya fahamu na hupunguza baridi
na mafua na watu wanaofanya mapenzi huelezwa kuwa mara kadhaa huonekana vijana
hata kama umri utakuwa umekimbia.
8.
Homoni
za kiume na za kike kuongezeka
Uzalishaji
wa homoni za kike na kume huongezeka mara dufu ambapo kwa mwanaume humsaidia
kuimarika kwa homoni ya kiume ambayo husaidia kuimarisha mifupa na miduli na
kwa mwanamke tendo al ndoa humwongezea honi ambayo inatunza tissue za sehemu ya
uke na humsaidia kupokea mapenzi na kuwajibika awapo mahala husika na mwenzi
wake.
Mpenzi
msomaji wangu bila shaka umeanza kupagawa baada ya kuona walau faida chache za
kufanya mapenzi, sasa wiki lijalo tutaangalia dalili za mwanamke anapotaka
ngono.
No comments:
Post a Comment