WIKI iliyopita tuliona baadhi
ya dalili ambazo zinaweza kukupa mwelekeo wa kujua kama
mpenzi huyo ameumbwa kwa ajili yako, ama la, lakini wiki hii tunaangazia na
kuzijua walau dalili Nne za Mpenzi ambaye hana mapenzi ya dhati nawe.
Ifahamike
kuwa hakuna asiyehitaji mapenzi ya kweli ingawa kuna wapenzi wanaothamini penzi
wmenzi wake anapokuwa na pesa au kazi Fulani na baada ya hapo hujitoa katika
mahusiano hayo hali ambayo huleta kwikwi katika mtima wa moyo wa anayefahamu
kupenda.
1. Muongo
Hakuna
asiyefahamu athari za mtu muongo katika jamii, vivyo hivyo ndivyo ilivyo katika
mapenzi uongo ni sumu mbaya na nidalili moja wapo ya kuonyesha kuwa mpenzi wako
hana penzi la dhati nawe na huyo aweza kukuletea athari za kufikiri hapo baadae
endapo hautakuwa makini nae.
Hivi
karibuni nilikuwa mjini Mbeya nikipata chakula katika moja ya mgahawa uliopo
mkabala na Posta, katika mgahawa huo nilikutana na vijana wawili na msichana
mmoja wakiwa wanakula chakula ambapo kati ya kijana mmoja alionekana kuwa ni
mpenzi mpya wa yule binti ambaye alisikika akisema kiwa ‘’ukija kwangu atakalia
sofa ambazo hujawahi kuziona maishani’’ hali iliyonishtua na kuelewa mara moja
kati ya tabia alizonazo kijana yule ambaye anaonekana ni mcha Mungu.
Hivi
utajisikiaje Mpenzi wako akigundua kuwa ulikuwa ukimdanganya na hatimaye yeye
akajua ukweli wa suala ulilokuwa ukimpiga fiksi? Lakini ushauri wangu si
kumacha bali jaribu kumshauri kwa hekima na akiendelea na tabia hiyo ujue kuwa
hana mapenzi ya kweli kwako.
2. Kupenda pesa
Ukiona
mpenzi wako wa kike ama kiume anapenda sana
kupata pesa kutoka kwako tambua ni moja ya dalili ambazo zinajieleza kuwa hana
mpango nawe bali analazimika kuwa nawe kutokana na pesa ama kipato chako.
Mpenzi wa namna hiyo ili kujihakikishia dalili hii siku moja akikuomba pesa
hata kama ameziona mwambie kuwa huna, hapo
yupo tayari kuvunja hata mahusiano kwasababu kitu muhimu kwake hajapata na wala
wewe si muhimu tena kwake.
Nieleweke
kuwa sisemi pesa ni mbaya katika mapenzi, la hasha bali pesa na mapenzi ni sawa
na trafiki na kondakta katika mambo Fulani yale………ya kuchafua mifuko kwenye
nguo nyeupe……………na ni muhimu wapenzi mkapenda kupeana maarifa ya kufanya kazi
halali ili kujipatia vipato kwa ajili ya kuepukana na hili.
3. Hajali kutokuwa jirani na wewe.
Mpenzi
anaye kupenda muda mwingi hutamani kuwa nawe karibu na inapotokea hamjaonana
hata masaa sita au matatu hujisikia shida ambapo kwa wengine hufikia kupiga
simu na ukimuuliza anasemaje atakuuliza maswali yaliyoshonana kama
ushanga mara upo wapi? Umekula? Na upo na nani? Na maswali mengi ya namna hiyo
ili mradi moyo wake utulie.
Endapo
Mpenzi wako mkiwa mbali naye kwa muda wa masaa mengi na yeye akaonyesha kuwa
hakukosa chochote kutokuwa nawe karibu ama kuwasiliana nawe basi ujue kuwa
mpenzi huyo ni kimeo yaani hana mapenzi ya dhati kwako.
4. Anapenda kukuudhi
Dalili
ya Nne ya mpenzi asiyekuwa na mapenzi ya dhati nawe ni yule anayependa kukuudhi
mara kwa mara kana kwamba anatafuta sababu ya kuachana nawe lakini anashindwa
kutamka bayana kuwa haitaji tena kuwa nawe.
Maudhi
hayana budi kutokea pale inapobidi kwa bahati mbaya sana
na si kwa makusudi, lakini wapo wapenzi wanaowaudhi wenzao kwa makusudi
huku
wakiendelea kusisitiza maudhi hayo kama utani
na kujua kwa makusudi kuwa anamuumiza mwenzi wake bila kuomba msamaha.
Ingawa
kuomba msamaha ni kipaji na hasa katika mfumo dume ambao unaonesha kuwa
mwanaume anapoomba msamaha basi ujue katumia njia nyingi za kumaliza
tatizo hilo zimeshindikana hivyo kaomba msamaha kwa kulazimika sana na
kwa siri.
Mpenzi
msomaji wa safu hii, baada ya kuona dalili hizo za mpenzi asiyemwaminifu kwako,
je wajua kuwa tendo la ndoa lina faida kubwa katika afya yako? wiki ijayo
jiandae kujua faida nane za kufanya ngono kiafya.
No comments:
Post a Comment