Saturday, September 21, 2013

MCT KWA KUSHIRIKIANA NA NACTE IMEKIFUNGIA CHUO CHA CITY MEDIA COLLEGE


Baraza la Habari Tanzania MCT kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), imekifungia Chuo cha City Media College baada ya kushindwa kukidhi vigezo vinavyohitajika katika Mitaala ya taifa yenye ithibati ya NACTE huku Vyuo vingine vitano vikipewa muda hadi Desemba, mwaka huu kuhakikisha vinafikia vigezo hivyo.
Vyuo vitano vilivyopewa muda huo ni Dar es salaam School of Journalism, Time school of Journalism, Royal College of Tanzania vilivyoko Jijini Dar es salaam, Institute of Social and Media Studies kilichopo Arusha na kile cha Zanzibar Journalism and Mass Media College kilichopo Visiwani humo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, KAJUBI MUKAJANGA amebainisha hayo wakati akitolea ufafanuzi kuhusiana na ukaguzi wa Vyuo vya Uandishi wa Habari nchini vilivyoruhusiwa kutumia mitaala hiyo, uliofanywa na Mabaraza hayo nchini.
Vigezo vinavyohitajika katika matumizi ya mitaala ya Taifa yenye ithibati ya NECTA kwa vyuo vya Uandishi wa Habari nchini ni pamoja na Vifaa vya mafunzo ya vitendo, taaluma, miundombinu na Uongozi wa chuo husika.

No comments: