Harry Redknapp, kama meneja,
aliitizama timu yake mpya ikichezea ugenini, ilipopata bao la kwanza
lakini Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford
ilifanikiwa kuishinda Queens Park Rangers 3-1.
Magoli ya kichwa kutoka kwa Jonny Evans na Darren Fletcher yaliweza kuinyanyua Man United.
Kwa muda wa saa nzima, Manchester United hawakucheza kama walivyotazamia mashabiki wengi, lakini kufuatia magoli matatu katika kipindi cha dakika nane, mambo yalibadilika kabisa.
Mchezaji wa zamu Javier Hernandez alifunga bao la tatu, na kuwawezesha vijana wa Sir Alex Ferguson kurudi kileleni katika ligi kuu ya Premier.
Shinikizo sasa ni kwa majirani Manchester City, ambao wakitaka kurudi kileleni itabidi sasa wajitahidi kuwashinda Chelsea katika mechi ya Jumapili.
QPR, ambao walimfuta kazi Mark Hughes siku ya Ijumaa, bado wanavuta mkia katika ligi, na mpaka sasa hawajapata ushindi katika mechi yoyote msimu huu, baada ya kucheza mechi 13.
No comments:
Post a Comment