Wafuasi wa rais wa Misri, Mohamed Morsi, wamesisitiza kuwa madaraka makubwa ambayo amejipatia ni ya muda.
Msemaji wa chama chake cha Freedom and Justice
ameiambia BBC, kuwa Bwana Morsi amejipatia mamlaka hayo kwa minajili ya
kulinda malengo ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani mtangulizi wake
Hosni Mubarak.Makundi ya upinzani nchini Misri, yameitisha maandamanao ya umma hii leo kupinga uamuzi wa rais wa nchi hiyo wa kujiongezea mamlaka kupindukia.
Kadhalika mmoja wa viongozi wa upinzani, Mohamed El Baradei, amemlaumu Moursi kwa kujiteua mwenyewe kuwa Pharao mpya.
Mamlaka hayo yanampa uwezo rais ambapo maamuzi yake hayawezi kubatilishwa na mamlaka yoyote na hata Mahakama kuu zaidi nchini humo.
No comments:
Post a Comment