Ripoti ya Nchi Maskini Sana Duniani ya Mwaka 20121,
yenye kichwa kidogo cha habari Kutumia Fedha Zinazotumwa na Raia
Wanaoishi Nga’ambo na Weledi Wao Kujenga Uwezo wa Uzalishaji, imetolewa
leo.
Mwelekeo wa uhamiaji
-Idadi
ya watu ambao wamehamia Ulaya kutoka Nchi Maskini Sana (LDCs)
iliongezeka kutoka milioni 19 mwaka 2000 kufikia milioni 27 mwaka 2010.
Hii ni sawa na 3.3% ya wakazi wote wa nchi hizo.
-Nchi
Maskini Sana Duniani zinatoa 13% ya wahamiaji duniani kote---idadi
ambayo inalingana na mgawo wa LDCs katika idadi ya wakazi wote duniani
(12.1%).
-Wahamiaji
wanne kati ya watano kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi zinazoendelea
(Kusini) na mmoja tu kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi
zilizoendelea (Kaskazini).
Utumaji fedha
-Kiwango
cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda kwenye nchi zao
kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011: Kutoka dola bilioni
3.5 kufikia dola bilioni 27. Tangu mwaka 2008 kiasi cha fedha
kimeendelea kuongezeka pamoja na kuwepo na anguko la kiuchumi duniani.
-Mwaka
2011 kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka
Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada dola milioni 3.2 na
kutoka Kenya dola milioni 2.5.
-Mwaka
2011, fedha zilizotumwa kwenda LDCs zilikuwa kama mara mbili ya thamani
ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) katika nchi hizi (dola milioni 15),
na kiwango hiki kilizidiwa tu na Misaada Rasmi Kutoka Nje, yaani ODA
(dola bilioni 42 mwaka 2010), kama chanzo cha fedha kutoka nje ya nchi.
-Kiwango
cha fedha zinazotumwa kutoka nje kama kingegawanywa kwa mwananchi mmoja
mmoja kiliongezeka kutoka dola 10 kama kila mtu angepokea hadi dola 30
kati ya mwaka 2000 na 2010.
-Fedha
zinazotumwa na raia wanaoishi nje zina umuhimu wa pekee kwa LDCs
ikilinganishwa na nchi zilizo katika makundi mengine. Katika LDCs, fedha
zinazotumwa na raia kutoka nje zinachangia 4.4% kwenye pato la nchi na
15% ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje. Kiwango hiki ni kikubwa kwa
mara tatu ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoendelea (ambazo siyo
LDCs).
-Kuanzia
mwaka 2008 hadi 2010, kiasi cha fedha kilichotumwa kutoka nga’mbo
kinalingana na zaidi ya moja ya tano ya pato la taifa la nchi za
Lesotho, Samoa, Haiti na Nepal.
-Tangu
mwaka 2009 hadi 2011, nchi za Nepal na Haiti zilipata fedha nyingi za
nje kutoka kwa raia wao walio ng’ambo kuliko zile ambazo nchi hizi
zilipata kutokana na mauzo ya bidhaa nje.
-Kwa
LDCs tisa, kiwango cha fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje kilizidi
kile cha uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na misaada rasmi
kutoka nje (ODA) kati ya mwaka 2008 na 2010. Hizi ni nchi za Bangladesh,
Haiti, Lesotho, Nepal, Samoa, Senegal, Sudan, Togo na Yemen. Kwenye
nchi nyingine nane za kundi la LDCs, katika kipindi hicho hicho, fedha
zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo zilizidi FDI: Benin, Burundi,
Comoros, Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Kiribati na Uganda.
-Theluthi mbili ya fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo kwenda kwenye LDCs zinatoka kwenye nchi zinazoendelea.
-Duniani
kote, gharama ya kutuma fedha zinafikia 9% ya kiwango cha fedha
kilichotumwa; kwa LDCs gharama ni kubwa zaidi kwa theluthi moja (12%).
-Kama
nchi zilizo kusini kwa Jangwa la Sahara zingelipia gharama za
uhamishaji fedha kwa wastani wa gharama inayolipwa duniani kote, mapato
yao yangekuwa yaliongezeka kwa dola bilioni 6 mwaka 2010.
-Asilimia
66 ya fedha zilizohamishwa kwenda kwenye LDCs kati ya mwaka 2009 na
2011 ni za nchi tatu tu: Bangladesh, Nepal na Sudan.
-Matumizi
ya simu za mkono kwenye LDCs ni makubwa zaidi (368 kwa kila wakazi
1,000) kuliko idadi ya akaunti za benki (171 kwa wakazi 1,000). Simu za
mkono zinaweza vile vile kutumika katika kuhamisha na kupokea fedha
kutoka ng’ambo.
Kuhama kwa utaalam
-Mtu
mmoja kati ya kila watu watatu wenye ujuzi mkubwa (mwenye elimu ya chuo
kikuu) kutoka LDCs anaishi ng’ambo. Kwenye nchi zilizoendelea kiwango
ni mtu mmoja katika kila watu 25.
-LDCs
sita zina raia wao wataalaum wengi zaidi wanaoishi nje ya nchi kuliko
wale waliobakia nchini mwao: Haiti, Samoa, Gambia, Tuvalu na Sierra
Leone.
-Theluthi
mbili ya wahamiaji wenye ujuzi mkubwa kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi
zilizoendelea; theluthi moja wanaishi katika nchi zinazoendelea.
-Kiwango cha kuhama kwa watu wenye ujuzi kwenda ng’ambo ni kikubwa (20% ) kwa LDCs nyingi (30 kati ya 48).
-Wahamiaji kutoka LDCs wenye elimu ya chuo kikuu ambao wanaishi na kufanya kazi ng’ambo inafikia milioni 2.
-Idadi ya Watanzania waliohamia Uingereza kwa kumbukumbu za mwaka 2000 ni 10,535.
-Aina
ya wahamiaji inafuata ukubwa wa kipato wa nchi mwenyeji. Katika nchi
zilizoendelea, 35% ya wahamiaji ni wale wenye elimu ya chuo kikuu;
kwenye LDCs 4% tu ya wahamiaji wana kiwango hicho cha elimu. Viwango
hivi ni kwa wahamiaji kutoka nchi zote, japo viwango ni hivi hivi kwa
wahamiaji kutoka nchi za kundi la LDCs.
-Theluthi moja ya wahamiaji kutoka LDCs ambao wana elimu ya chuo kikuu wanaishi Marekani.
Uwezo wa kiuchumi (Uchumi mpana)
-Kiwango
cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka kwa LDCs tangu kipindi cha msukosuko wa
kiuchumi duniani (2009-2011) ni 4.7%, ambacho ni chini ya kiwango cha
kipindi cha miaka ya ukuaji mkubwa wa kiuchumi (2003-2008), yaani 7.9%.
Hii ina maana kwamba kiwango cha ukuaji wa kipato kwa mwaka kwa kila
mkazi kilishuka kutoka 5.4% miaka ya ukuaji mzuri wa uchumi hadi kufikia
2.4%.
-Wastani
wa ukuaji halisi wa pato la nchi katika LDCs mwaka 2011, yaani 4.2%,
ulikuwa chini ya 4.9% ya mwaka 2009 wakati wa anguko la uchumi duniani.
-Kile
kinachojulikana kama Gross fixed capital formation kwenye LDCs
kilipanda kidogo kutoka 20.7% ya pato la jumla la taifa mwaka katika
miaka ya 2005-2007 kufikia 21.6% miaka ya 2008-2010. Hata hivyo, bado
kilibaki chini ya viwango vya nchi nyingine zinazoendelea, ambazo
zilifikia kiwango cha 30.1%.
-LDCs
zinaendelea kutegemea sana raslimali kutoka nje. Pengo la pato
linalotokana na uagizaji bidhaa na uuzaji bidhaa nje lilikuwa kubwa kwa
20% ya pato la jumla la taifa katika nchi tano za kundi la LDCs mwaka
2011, wakati LDCs nyingine 13 pengo lilikuwa asilimia 10 ya pato la
jumla la taifa.
-Kiwango
cha utegemezi wa rasilimali kutoka nje katika kulipia uwekezaji wa
ndani ya nchi kati ya mwaka 2008 na 2010 kilikuwa 15% ya pato la jumla
la taifa kwa LDCs ambazo hazisafirishi mafuta nje.
-Asilimia
62 ya mauzo ya bidhaa nje kutoka LDCs 48 yalikuwa ni kutoka nchi tano
tu: Angola, Bangladesh, Equatorial Guinea, Yemen na Sudan. Ukiacha
Bangladesh, nchi zote hizi zinauza mafuta nje.
-Mapato
ya LDC kwa mauzo ya bidhaa nje yanategemea zaidi mauzo ya bidhaa moja
(mafuta), ambayo yanaingiza 46% ya jumla ya mapato yote yanayotokana na
mauzo ya bidhaa nje.
-Zaidi
ya nusu ya mauzo ya nje kutoka LDCs (54%) yalikuwa yanakwenda kwenye
nchi zinazoendelea mwaka 2011, mwelekeo unaothibitisha umuhimu wa
biashara ya kusini-kusini. China ndiyo iliyonunua bidhaa nyingi zaidi
kutoka LDCs (26.4%) ikiwazidi Jumuia ya Ulaya (20.4%) na Marekani (19%).
ZIKO WAPI NCHI MASKINI SANA DUNIANI?
Umoja wa Mataifa unaziweka nchi 48 kwenye kundi la Nchi Maskini Sana Duniani (LDCs). Mgawanyo wao ni kama ifuatavyo.
Africa
(33): Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic,
Chad, Comoros, Jamhuri ya KIdemnokrasia ya Kongo(DRC), Djibouti,
Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau,
Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger,
Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan,
Togo, Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia;Asia (9):
Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal,
Timor-Leste na Yemen;Caribbean (1): Haiti;Pacific (5): Kiribati, Samoa,
Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu.
Mchoro 1 – Nchi 48 za kundi la LDCs
Imetolewa na UNCTAD
Kutengeneza list ya LDCs
List
ya LDCs inapitiwa upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Uchumi
na Jamii (ECOSOC) la Umoja wa Mataifa, kufuatana na mapendekezo ya
kamati ya Sera ya Maendeleo (CDP).
Katika mapitio ya hivi karibuni, Machi 2012, CDP ilitumia vigezo vifuatavyo:
1. Kigezo cha pato la kila mtu, kwa kufuata Pato la Jumla la Nchi (GNI) kwa kila kichwa (wastani wa miaka mitatu)
2. Kigezo cha raslimali watu ambacho kinatumia viashiria kama lishe, afya, kuandikishwa shuleni na kujua kusoma na kuandika
3.
Kigezo cha mazingira hatarishi ya kiuchumi. Ambacho kinatumia viashiria
kama mishtuko ya kiasili, mishtuko ya kibiashara, udogo na umbali.
Nchi
tatu tu zimefanikiwa kupanda daraja kutoka list ya nchi za kundi la
LDCs: Botswana Desemba 1994, Cape Verde Desemba 2007 na Maldivs Januari
2011. Samoa inategemewa kupanda daraja tarehe 1 Januari 2014.
ECOSOC
ilipitisha pendekezo la CDP kuipandisha daraja Equatiorial Guiones
mwezi Julai mwaka 2009 na mwezi Julai 2012 ikakubali pendekezo la CDP
kuipandisha Vanuatu. Hata hivyo ruhusa ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
bado itahitajika ili kuzipandisha daraja nchi hizi mbili.
Tuesday, November 27, 2012
Serikali yasisitiza kushirikiana na wadau kuendeleza kilimo
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam mara mara ya kuongoza mkutano maalum wa
Mpango wa kukuza kilimo kusini mwa Tanzania (SAGCOT), akizungumzia
umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya kilimo, kulia ni Waziri wan chi
Ofisi ya waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu na Kushoto
ni Waziri wa Kilimo, Bw. Christopher Chiza.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Serikali
ya Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta
binafsi na wadau wengine ili kufikia mapinduzi ya kilimo hapa nchini na
hivyo kupatikana usalama wa chakula na maendeleo.
Msimamo
huo umetolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano
mkubwa wa kilimo unaofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkutano
huo wa siku mbili umetayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Kituo cha mpango maalum wa
uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Mkutano
huo unalenga kuvutia wawekezaji katika maeneo ya kilimo, biashara na
miradi ya maendeleo kijamii na kiuchumi katika eneo la SAGCOT.
“Ushirikiano
uliopo kati ya serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo, wakulima na
wadau wengine wa kilimo umesaidia kuendeleza sekta hii hapa nchini,”
alisema.
Waziri
Mkuu aliyashukuru makampuni 20 ambayo tayari yameshatoa ahadi ya
kuwekeza katika sekta ya kilimo Tanzania katika miaka ijayo na wakati
huo huo akaitaka sekta binafsi kufanya uamuzi zaidi wa kuwekeza zaidi
katika sekta hiyo.
Hata
hivyo alisisitiza kwamba wawekezaji wote katika ukanda wa SAGCOT
watapewa kipaumbele pale ambapo uwekezaji wao unalenga pia kushirikisha
wakulima wadogowadogo..
“Ni
muhimu kusisitiza kwamba tunahitaji zaidi uwekezaji ambao utajali
kushirikiana na wakulima wadogo na wajasiriamali wadogo na wa kati,”
alisema.
Alisisitiza
kwamba hata mapendekezo ya sera za uwekezaji katika kilimo zitoe
kipaumbele kueleza jinsi wakulima wadogo na watanzania wa kawaida
watakavyofaidika na uwekezaji katika ukanda wa SAGCOT.
Waziri
Mkuu aliwahakikishia wawekezaji kwamba kupitia sheria mbalimbali
Tanzania inatoa vivutio vingi na vizuri kulinganisha na nchi nyingine za
Afrika.
“Kuwekeza Tanzania pia kunawahakikishia soko la uhakika katika eneo hili la Afrika,” alisema.
Alisema Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohakikisha usalama wa wawekezaji.
Akitoa
mada katika mkutano huo, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza alitaja baadhi ya maeneo yanayolengwa katika
uwekezaji SAGCOT kama kilimo cha miwa, matunda, ufugaji, nafaka na mazao
ya misitu.
Katika
siku ya pili ya mkutano huo wawekezaji watapata fursa ya kutembelea
maeneo maalum ya miradi pamoja na kuangalia miradi ya kuimarisha
miundombinu katika ukanda huo wa SAGCOT.
SAGCOT ni
mpango unaoshirikisha sekta binafsi na ya umma unaotegemewa kuleta
mapinduzi makubwa katika usalama wa chakula nchini kwa kushirikisha pia
wakulima wadogo wadogo katika mazingira endelevu.
WADAU WAJITOKEZA KUCHANGIA HARAMBEE YA UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI ILIYORATIBIWA NA TEA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka
(kulia) akiongozana na mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana, Naibu Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu, Dk. Asha Rose Migiro ambapo katika
harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 278 zilipatikana.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Dk. Naomi Katunzi akizungumza katika harambee hiyo.
Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Rex Energy, Francis Kibisa kwa mchango alioutoa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza wakati
wa harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.
Naibu Katibu
Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro akipokea mchango
wa shilingi milioni tatu kutoka kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa ukiwa ni mchangop wake kwa ajili ya
kusaidia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike wakati wa harambee ya
kuchangia ujenzi wa mabweni ya wasichana iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Inocent Mungi akikabidhi mchango wa shilingi milioni tano kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mstaafu,
Dk. Asha Rose Migiro wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili
ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es
Salaam.
Mwanasheria
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Vupe Ligate akipeana mkono na Naibu Katibu
Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Matifa, Dk. Asha Rose Migiro baada ya
kuchangia katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike
ambapo jumla ya shilingi milioni 278 zilipatikana katika harambee hiyo.Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro akimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Rex Energy, Francis Kibisa kwa mchango alioutoa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike
Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk.
Asha Rose Migiro (katikati) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi
milioni tano kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya KCB
Tanzania, Christiane Manyeye (kulia) na mwakilishi wa ubalozi wa Kenya,
Boniface Makao wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya
ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam
juzi. Wa pili kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.
Shukuru Kawambwa.
Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari akikabidhi mchango wa dola za kimarekani 1,000 kwa Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiromgeni ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mstaafu Dk. Asha Rose Migiro (kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani, Mkuu wa Kitengo cha mahusiano wa Shirika la Nyumba (NHC), Susan Omari baada
ya shiriki hilo kuchangia mabati 1,000 yenye thamani ya shilingi
milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa kundi la THT wakitumbuiza katika harambee hiyo.
Mkurugenzi wa Radio One, Deogratius Rweyunga akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk.
Asha Rose Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa mabweni ya
wanafunzi wa kike iliyofanyika jijini Dar es Salaam
MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI, KENYA
Mwanasheria
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki wakiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo.
Kushoto ni bwana Wilbert Kawa Katikati ni bwana Dr. Richard Sezibera na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano Uganda. Mkutano huu umefanyika
katika ukumbi wa Kimataifa wa Kenyetta jijini Nairobi
Waziri
wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samweli Sitta pamoja
na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyemba (wa pili kulia) , Waziri wa
nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika (kushoto) na
Mhe Ole Nangoro Naibu Waziri Kilimo na Mifugo (kulia) wakifuatilia kwa
makini jambo katika Mkutano wa Baraza la Mwawaziri wa Jumuiya Jijini
Nairobi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda
(kulia) akifuatilia kwa makini mkutano unaoendelea Nairobi katika
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya
SKYLIGHT BAND YAZIDI KUWAKAMATA MASHABIKI KATIKA KIOTA CHA THAI VILLAGE MASAKI-JIJINI DAR.
Vijana wa SKYLIGHT BAND wakiongozwa na Sam katika kuhakikisha mashabiki
wa SKYLIGHT BAND wanapata flava za ukweli zikiwemo Kwaito, Ragga,
Reggae, Dance Hall, Nigerian Flava, Sebene na zingine kibao. Kushoto ni
Joniko Flower na kulia ni SONY MASAMBA. Wanapiga show ya kufa mtu kila
Ijumaa katika ukumbi wa Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam.
Mary Lukas sambamba na Joniko Flower wakitoa burudani.
SONY MASAMBA akishusha mistari.
Msanii wa SKYLIGHT BAND Aneth Kushaba AK 47 akionyesha umahiri wake wa kucheza kwa mashabiki.
Aneth Kushaba AK 47 akiwapa raha mashabiki wake (hawapo pichani).
CEO wa Ndege Insurance Dkt. Sebastian Ndege sambamba na mashabiki wa SKYLIGHT BAND wakiserebuka.
Warembo wakisakata rhumba kwa raha zao.
Pichani
Juu na Chini ni Umati wa mashabiki waliojitokeza katika Kiota cha Thai
Village Masaki jijini Dar es Salaam kushangweka na SKYLIGHT BAND
mwishoni wa wiki, ni Kila Ijumaa wako hapo.
Namba ya Mashabiki ikizidi kuongezeka kama inavyoonekana pichani, palikuwa hapatoshi. Usikose Ijumaa hii.
Couples waliong'ara siku hiyo ni hawa hapa.
Blogger King Kif (kushoto), Mdau John Mwansasu na wadau wengi wakipozi kwa picha.
Mashabiki wapya All the way from Nairobi wakipata ukodaki na Msanii wa SKYLIGHT BAND Aneth Kushaba AK47.
Watasha nao ndani nyumba chezea SKYLIGHT BAND wewe......!!!
Bongo Movie Star Steve Nyerere, Mboni Masimba a.k.a Kim Kardashian wa Bongo na Mdau John Mwansasu wakipata Ukodaki.
Mdau akipozi na warembo.
Warembo katika pozi ndani ya SKYLIGHT BAND.
Adrian Hillary Stepp, Blogger Cathbert Angelo wa Kajunason Blog na Blogger King Kif.
The Don Shaban Mazua (kushoto) akila ukodaki na wadau.
Mh Naibu Balozi wetu wa Uingereza na Irene wameremeta
Maharusi wakivalishana pete baada ya kula viapo
Dendazzzzz......
Maharusi wakikabidhiwa cheti cha kumeremeta
Maharusi wakifungua mziki kwenye mnuso wa kumeremeta kwo
Maharusi na wanafamilia
Maharusi
katika picha ya pamoja na familia. Kutoka Kulia ni Mama wa Bwana harusi
Kilumanga, Maharusi, Mama Irene na Dada wa bwana Harusi Mariam
Kilumanga
Mashaaallah... |
Mh Chabaka akimlisha mai waifu wake Irene keki
Monday, November 26, 2012
WILDAF yaendesha Mkutano kwa Wadau wake wa Kupiga Vita Ukatili Dhidi ya wanawake nchini
Brass
Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili
dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na
Maendeleo ya Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
na kumalizikia kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam
leo.
Washiriki
wa Maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake yaliyoratibiwa
na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika
(WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya Mabango yenye Ujumbe wa Kupiga Vita Ukatili dhidi ya Wawanake.
Maandanamo
yakipokelewa na Muwakilishi wa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa
Mambo ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa,Balozi Dora Msechu (wa tatu kulia),Mwenyekiti wa Shirika la
Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi
Kaihula,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema
(pili kulia) pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Charles
Kenyera.
Balozi wa
Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan akikata utepe uliokuwepo kwenye
basi aina ya Toyota Coster,ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Safari ya Wadau wa
Wildaf wanaokwenda Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea
kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali katika mikoa ya kanda hiyo kuhusiana
Ukatili dhidi ya Wanawake.
Wadau wa
Wildaf wakipanda kwenye Basi hilo tayari kwa Safari ya Mikoa ya Kanda ya
Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali
katika mikoa ya Kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya Wanawake.
Mwenyekiti
wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika
(WILDAF),Mh. Naomi Kaihula akisisitiza jambo wakati akitoa neno la
Ukaribisho katika Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo
"FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike"
uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es
Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.
Mwenyekiti
wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika
(WILDAF),Mh. Naomi Kaihula (pili kupia) akitoa neno la Ukaribisho katika
Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea
Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema
leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na
kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.Wengine Pichani toka kulia ni,Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Mkurugenzi wa Mambo
ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa,Balozi Dora Msechu,Mkugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake Katika
Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Judith Odunga pamoja na Balozi
wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan.
Muongozaji wa Mkutano huo,alikuwa ni Bw. Deus Kibamba
Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini,DCP Rashid Omar akiwasilisha mada ya
aina mpya ya Karatasi maalum itolewayo na Polisi iwapo mtu anapatwa na
tatizo la Majeraha (PF 3) iliyofanyiwa Marekebisho na kuongezewa baadhi
ya Vipengele Muhimu,wakati wa Mkutano uliofanyika leo wa Kupiga Vita
Ukatili dhidi ya Wanawake,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
Mgeni
rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh.
Angella Kairuki akisoma Hotaba yake mbele ya Mamia ya Wadau wa Wildaf
waliohudhulia Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh.
Angella Kairuki akikata Utepe wa Kuashiria Uzinduzi rasmi wa aina mpya
ya PF 3 mara baada ya kutoa Hotuba yake huku akisaidiana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Kushoto
ni Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya
Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa Makini.
Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kipolisi ya Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano huo.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema akiteta jambo
na Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya
Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Mrisho Mpoti na Mjomba Band wakitoa Burudani wakati wa Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment