PICHA 13 ZA ENEO ALILOPATA AJALI SHARO MILIONEA, TAZAMA AJALI ILIPOANZIA.
Posted: 28th November 2012 by MillardAyo in News
Gari lilivuka hii sehemu na kubinukia kule mbele baada ya hilo daraja dogo ambako ndio liligonga huu mti hapa chini.
Huu
ni mti ambao aliugonga katikati akaukata kuwa vipisi viwili, mwingine
ukatupwa mbele ya huu kama unavyoonekana alafu gari ikaenda kubinuka
kichwa chini miguu juu kwenye lile eneo la wazi unaloliona kwa mbali
baada ya hayo matawi ya huo mti hapo mbele.
Hapa
ndipo mwili wa Marehemu ulikutwa baada ya kutupwa kutoka kwenye gari,
mashuhuda waliofika kwenye eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali
wanasema walianza kuwatafuta majeruhi wakidhani ni wengi na hawakumuona
mtu yeyote kwenye gari ila baadae mama mmoja ndio akamuona Sharo
Milionea akiwa hapa muda mfupi kabla ya kukata roho.
Huyu
shuhuda wa ajali amesema Sharo Milionea alifariki dunia baada ya dakika
15 za ajali na hiyo ilikua saa mbili usiku ndio ajali imetokea, hakukua
na magari yanayopita kwa wakati huo hivyo walkosa pa kuomba msaada
manake hata kwenye kijiji wanachoishi chenye watu kati ya 300 na 400,
hakuna yeyote mwenye pikipiki wala gari.
Aliniambia
pia kwamba Sharo Milionea hakuwa na uwezo wa kuongea chochote na baada
ya hizo dakika 15 alitingisha tu mguu na kugeukia upande wa pili na
kukata roho, mwili wake ulikuja kuchukuliwa saa nne usiku na askari.
Hili eneo liko umbali wa kama dakika 40 mpaka Tanga mjini na ni dakika 15 tu mpaka kufika nyumbani kwa kina Sharo milionea ambako ndiko Marehemu alikua anaelekea, rafiki yake wa karibu mwigizaji Kitale (anaeigiza kama teja) kasema mara ya mwisho Sharo aliongea nae na akamwambia anakimbia Tanga mara moja kumpelekea mama yake mtaji wa shilingi milioni sita za biashara ambazo alikua nazo wakati huo kwenye gari lakini imefahamika kwamba hizo pesa zimeibwa zote kwenye eneo la ajali.
No comments:
Post a Comment