Friday, November 23, 2012

Jaribio la mapinduzi yatibuliwa Sudan


Salah Gosh
Salah Gosh

Watu kadhaa wamekamatwa na serikali ya Sudan, wakiwemo mkurugenzi mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi, Salah Gosh na maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo kufuatia madai ya kujaribu kupindua serikali ya nchi hiyo.
Raia kadha wamesema wameona magari kadhaa ya kivita na wanajeshi wakishika doria katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
Katika miezi ya hivi karibuni, Utawala wa Khartoum umeshuhudia kuongezeka kwa maandamano dhidi ya serikali, kupinga kuongezeka kwa bei ya chukula na pia kushinikiza mabadiliko ya kisiasa.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir amekuwa madarakani tangu mapinduzi ya serikali mwaka wa 1989.
Waziri wa habari wa Sudan Ahmed Belal Osman, amesema watu 13, wamekamatwa kuhusiana na njama hiyo ya kupindua serikali.






No comments: