MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKOA MPYA WA KATAVI LEO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na
mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa
Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu
kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi,
Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na
Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya
uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea
mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli
mbalimbali za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali
zikiendana na sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa
wa Katavi PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM.
Makamuwa
Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh.
Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na
kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo.
Makamu
wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu
wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa
Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw.
Mselem Said.
Mkuu wa mkoa wa Katavi akimkaribisha Makamu wa Rais Dt. Gharib Bilal ili kuongea na wananchi wa kijiji cha Kabungu.Msafara
wa magari ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal ukiwasili katika eneo
lilipowekwa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa mkoa wa Katavi katika kilima
cha kijiji cha Kabungu Mkoani Katavi.
Wazee
waasisi wa kijiji cha Kabungu wakinyanyua matawi ya miti juu kama
ishara ya kumpokea Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati alipowasili
katika kijiji hicho leo.
Makamu
wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa
Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia
Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya
Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda
tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
Makamu
wa Rais Dkt. Gharib Bilal akimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati
wa uzinduzi wa mkoa wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili kulia
ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt. Mary Nagu.
Kutoka
kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt.
Rajab Rutengwe, Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye,
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma
Kanali Issa Machibya wakiwa katika sherehe za uzinduzi huo.
Mkuu
wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka
salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
Waziri
wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na
kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la
uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na
wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
Kwaya
ya Vijana ya Moravian mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo
uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.
Martha
Mbogo mwimbaji wa kundi la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi
hilo lilipokuwa likitumbuiza katika uzinduzi huo mjini Mpanda.
Wananchi
wa Mpandawakinyanyua mkono yao juu kama ishara ya kushangilia
kuazinduliwa kwa mkoa wao wa Katavi uliofanyika kwenye viwanja vya
Kashaulili mjini Mpanda leo.
Watoto
Daniel Ntwangile na Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu
Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana
Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji
Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri
Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza
Makamu
wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa
Veta Chuo cha Veta Mpanda Trojemsi Bashato wakati alipotembelea banda la
Veta.
Makamu
wa Rais akisikiliza maelezo kutoka kwa Thomas Lemunge mfanyakazi wa
kampuni ya simu ya TTCL wakati alipotembelea Banda la kampuni hiyo,
kulia ni Bw Huphrey Ngowi mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Makamu
wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa huduma
Mwandamizi wa benki ya Wanawake TWB BiMargaret Msengi wakati
alipotembelea katika banda hilo leo.
Makamu
wa Rais Akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea
katika banda hilo leo njini Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi
Dkt. Rajab Rutengwe.
SHILINGI BILIONI 86 ZAIBWA WIZARA YA NISHATI/TANESCO, GRIDI YA TAIFA HATARINI
Na Zitto Kabwe
Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012
limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54
zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na
Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha
mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka
kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor
General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake
kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia
manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.
Itakumbukwa
kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na
Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa
mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa
manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).
Katika
mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni
kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na
baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya
Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii. Kamati ya Nishati
na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba ililitaka
Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili kwenye Taarifa
yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili mwaka 2012.
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika Hotuba yake
ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika kwa uchunguzi
kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi
hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu.
Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya
CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni
za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa
bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi. Hivi
sasa kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya
kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo
kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi
kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa
za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji
chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu
ya uwezo (installed capacity). Iwapo TANESCO wataendelea kutumia zaidi
maji yaliyopo Mtera, Mitambo itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama
maana Mtera ndio nguzo kuu ya Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana
kwa uchumi na ulinzi na usalama wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo
hatarini kutokana na kiwango cha Maji kilichopo Mtera hivi sasa na
kuendelea kupungua kwa kina hicho cha maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1.
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za
manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi
na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe
na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.
2.
Waziri wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme
nchini, uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la
Mtera na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa
mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama.
Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda
uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri
aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu
maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86
za kununua mafuta ya IPTL.
3.
Waziri wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina
imetoa kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya
Mwezi Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za
zabuni zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA
wamechukua dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya
mabilioni ya fedha kwa Serikali.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha
Dar es Salaam. Novemba 25, 2012
"ASANTENI WASAMALIA… KWA MSAADA WENU"
Na Devota Mwachang’a
Hatimaye Beatrice Shimende Kantimbo (48) pichani amefanikiwa kusafiri
kwenda nchini India kutibiwa mguu katika
hospitali ya Apollo, kutokana na michango ya wasamalia wema pamoja na Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa Julius
Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Beatrice, aliyeambatana na
Mumewe Emmanuel Kantimbo aliwashukuru sana wale wote walioguswa mara baada ya
kupata taarifa zake, na kuamua kumsaidia kwa pesa, ushauri na kwa sala, pia vyombo vya habari.
Beatrice amesumbuliwa na maradhi hayo kwa takribani miaka 12, vipimo vya
kitabibu vimegundua kuwa ni ugonjwa wa matende (elephantiasis).
Mwanamke huyu alikuwa ni 'mchakarikaji' kweli, aliendesha maisha yake kwa biashara kadhaa wa ikiwemo
biashara ya duka, grosari na saluni ya ususi wa nywele pia aliyekuwa akifanya kazi za ushereheshaji (MC)
kwenye sherehe akifahamika kama MC Kimbaumbau,
Hapa alisimulia namna alivyoanza kuugua…"Nakumbuka mwaka 1998 nikiwa
kwenye biashara zangu pale Ubungo, kuna kitu kilinichoma hapa (anaonyesh
pajani) maumivu yake yalikuwa mithiri ya sindano, hata hivyo hayakudumu sana
wala hapakuwa na alama yoyote.
"Baada ya dakika chache nikajihisi homa kali. nikaanza kutetemeka
mwili mzima, nikaamua kwenda hospitali ya Neema, hospili ya karibu na mahali
nilipokuwa nikiishi pale Ubungo. Daktari akanipima, akagundua nilikuwa na
malaria.
"Wakati huo mguu haukuonyesha dalili zozote za maumivu wala jeraha.
Malaria ilkuwa kali, nikalazwa kwa muda wa wiki mbili pale hospitali.
Nikaruhusiwa, nikarudi nyumbani na hapo ndipo nilipoanza kuona mguu unavimba.
Kaadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mguu nau unavimba"
Kuanzia mwaka 2010 mguu umezidi kuongezeka kuvimba na maumivu makali
yaliyotokana na kidonda kikubwa kilichosababishwa na kuondolewa kwa sehemu ya
nyama ya mguu wake wa kuume iliyokuwa imeoza.
Anasema: "Baadhi ya madaktari wa Muhimbili walinishauri nikubali
kukatwa mguu. Wanasema ya nyama imeoza na mfupa wa mguu umeharibika. Mimi
sikukukubaliana na ushauri wao kwa sababu baada ya kupigwa X-ray 2007
iligunduliwa tatizo kubwa lilikuwa matatizo kwenye mishipa ya kupitisha maji
kutokana na nyama kuharibika. Sio mfupa.
"Nilikataa kwa imani kuwa nitapona tu. Nikijiangalia nina uwezo wa
kusimama na kutembea isipokuwa tu kinachonipa taabu kwa sasa ni nyama za mguu
zimekua sana kiasi kwamba nikitembea zinagusa mguu wa kushoto" alisema.
WAISLAM WA DHEHEBU LA SHIA JIJINI DAR WAADHIMISHA SIKU YA ASHURA KUKUMBUKA KIFO CHA MJUKUU WA MTUME MOHAMMED (S.A.W)
Pichani Juu na Chini Waumini wa
dhehebu la Shia wakiwasili na kukusanyika katika eneo la makaburi ya
Washia Kisutu jijini Dar es Salaam wakijiandaa kuanza maandamano ya
kuadhimisha siku ya Ashura kukumbuka kifo cha Mjukuu wa Mtume Mohammed
(S.A.W) Imam Hussein yaliyofanyika jana.
Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamaat Shia
Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa waandishi wa habari amesema
katika kuadhimisha siku hii Waislam wa dhehebu la Shia watafanya
matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa
Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo ndani yake kutakuwa
kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za maombolezo
tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi kujipa uhai
kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa watu wake
na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya wenzake.
Imamu wa Msikiti wa Imam Ali wa
Magomeni Mapipa Msabaha Shaaban Ali Mapinga akizungumza na waandishi wa
habari amesema siku hii ni siku ya kukumbuka na kuadhimisha miaka 1473
ambapo katika nchi ya Iraq kwenye mji wa Karbala aliuwawa mjukuu wa
Mtume Mohammed (S.A.W) aliyekuwa akijulikana kwa jina la Imam Hussein
Bin Ali Bin Abutwalib.
Amesema katika nyakati hizo alitokea
mtawala dhalim aliyekuwa akitetea dhulma na kukiuka haki za binadamu
kitendo ambacho mjukuu wa Mtume Imam Hussein hakukubaliana nacho na
kuunda jeshi lake dogo kutetea haki na kupinga Batili.
Kwakuwa Imam Hussein alikuwa na
dhamana ya kutetea haki alikataa kuwa chini ya mtawala huo ndipo
alipotumiwa jeshi la watu kama 30,000 naye akiwa na jeshi la watu 72
walipambana katika mji huo na mjukuu wa Mtume aliuwawa kifo cha kikatili
cha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema siku hii ni muhimu sana kwa
Waislam kote duniani kwa sababu tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo
chake kilikuwa ni kifo cha kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso
wa ardhi.
Amesema kifo cha Imam Hussein
kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo haki ilizimwa
na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka batil isimame , kwa hiyo
siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.
Aidha Sheikh Salum amesema kwa
Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa wajifunze kutoka
kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa haki, alikuwa
anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki na kutetea
uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo, kutetea wanyonge,
kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna yoyote ile ndio lililokuwa
jambo alilolipenda Imam Hussein.
Waumini hao wakiwa wamejipanga tayari kuanza maadamano kutoka makaburi ya Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia.
Pichani juu na chini msafara wa waumini wa Shia umeanza.
Hisia na Majonzi vilionekana.
Ni jambo jema watoto kujua dini
mapema, kama inavyoonekana pichani mtoto akiwa ameambatana na mzazi
wake katika maandamano ya siku ya Ashura.
Bango lenye Ujumbe maalum wa siku ya Ashura.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA MKOA MPYA WA KATAVI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, wakati wa hafla ya uzinduzi
wa uwanja huo iliyofanyika mkoa Mpya wa Katavi, leo Nov 24, 2012 katika
uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliogharimu kiasi cha Sh.
Bilioni 30. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mama
Zakhia Bilal (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Miundombinu, Omar
Chombo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.Charles Tizeba. Picha na OMR
ONYESHO LA KHANGA ZA KALE 2012 LILIVYOFANA JIJINI DAR
Mgeni Rasmi katika Onyesho la Khanga za Kale, Waziri wa Maendeleo
ya Jamii, Jisnia na Watoto Mheshimiwa Sophia Simba akisoma hotuba yake fupi
wakati wa kufungua rasmi Onyesho la Mavazi ya Khanga za Kale
2012 linaloratibiwa na Mamaa wa Mitindo Asia Idarous Khamsin (kushoto) chini
ya Kampuni yake ya Fabak Fashion. Onyesho hilo lilifanyika katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa Onyesho la Mavazi ya Khanga za Kale 2012, Mamaa wa
Mitindo Asia Idarous Khamsin akizungumza machache kabla ya kuanza Rasmi
kwa Onyesho katika Hoteli ya Serena, Jijini
Dar es Salaam.
Kiki fashions nao hawakukosa.
Mwanamitindo Martine Kadinda nae hakuwa nyuma kuonyesha vazi lake alilobuni.
Wanahabari nao hawakuwa nyuma kupata matukio.
Meza kuu wakishangilia.
Wageni wakifuatilia.
Vimwana wa Unique Modoz nao walikuwepo.
Wageni waalikwa wakiteta.
Mbunifu wa mavazi Gabliel Mollel akipita jukwaani na vazi alilobuni.
Mbunifu wa Mavazi Gymkhana Hilali anayemiliki Paka Wear akipita na vazi lake.
Mama wa Mitindo House Khadija Mwanamboka nae hakukosa.
Mshiriki wa shindano la EBBS 2012, Salma akitoa burudani.
Moja ya picha iliyofanyiwa mnada.
Muandaaji wa Onyesho la
Mavazi ya Khanga za Kale 2012, Mamaa wa
Mitindo Asia Idarous Khamsin akiwa na mumewe mzee Khamsin wakiwapungua
wageni waliohudhuria. Mavazi hayo yanayofuata katika picha za chini
yamebuniwa yeye.
Mmiliki wa Blog hii, Cathbert Angelo
Kajuna nae alipata nafasi ya kupanda jukwani akiwa amevaa vazi la shati
ya khanga aliyobuniwa na mama Asia Idarous Khamsin.
Pozi kidogo...
Mmilikiwa wa Blog ya Missie Popular, Bi. Mariam Ndaba nae alipita na vazi lilibuniwa na mama wa Mitindo Asia Idarours Khamsin.
Mmilikiwa wa
Blog ya Mtaa kwa Mtaa, Othman Michuzi nae hakuwa nyuma kuvaa vazi
lilibuniwa na mama wa Mitindo Asia Idarours Khamsin.
Matukio Chuma nae hakuwa nyuma.
Sarah mke wa Raqey Mohammed mmiliki wa I-View Media nae alipata nafasi.
Taji Liundi hakukosa.
Baby Madaha...
Magesa mwendeshaji wa shindano la Unique Modo nae alikuwepo.
Wageni wakishangilia.
Modoz wakipita kwa steji, wakiongozwa na Mtangazaji wa Star Tv,
Sauda Mwilima (kwanza Kulia), Mmiliki wa Mtaa kwa Mtaa Blog, Othman
Michuzi (kati) na Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo (kwanza
kushoto).
No comments:
Post a Comment