Tuesday, March 4, 2014

UTAFITI !!!!: KUKOSA KIFUNGUA KINYWA ASUBUHI NI MOJA YA SABABU 5 ZA KUUDHURU UBONGO WA BINADAMU.


  1. Kukosa Kifungua Kinywa asubuhi
    Watu wanaokosa kifungua kinywa asubuhi wanapata upungufu wa kiwango cha sukari kwenye damu. Hii husababisha upungufu wa madini (nutrients) kwenye ubongo na hatimaye ubongo hudhoofika.
  2. Kula kupita kiasi:
    Inasababisha kukaza kwa misuli au mishipa ya Ubongo na hatimaye hupelekea kudhoofika kwa mfumo wa fahamu.Afya ya Ubongo
  3. Kuvuta Sigara:
    Kwenye sigara kuna kitu kinaitwa Nikotini ambayo ndani yake kuna chembechembe ambazo zina sababisha makunyanzi kwenye ubongo na kisha kudhoofu.
  4. Kutumia Sukari nyingi:
    Matumizi ya sukari nyingi husababisha matatizo katika mfumo wa unyonyaji wa Protini na Madini joto mwilini na kusababisha ugonjwa wa Utapiamlo ambao pia huingilia mfumo wa fahamu
  5. Kuvuta Hewa chafu:
    Ubongo ndio mtumiaji mkubwa wa Oxijeni tunayo ivuta. Unapovuta hewa chafu unapunguza mgawo wa Oxijeni kwenye Ubongo na hatimaye kupunguza ufanisi wake

No comments: