Kipa wa zamani wa Yanga, Yaw Berko
anatua nchini leo akitokea kwao Ghana akiwa kipa ghali zaidi kwa kuwa atalipwa
mshahara mkubwa hata kuliko Juma Kaseja wa Yanga.
Berko anatua nchini saa nne asubuhi
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na mara moja
atakwenda kumalizia mazungumzo na Simba na tayari wamekubaliana mshahara wake
utakuwa dola 1,500 (Sh 2,400,000), kwa mwezi.
Mabingwa Yanga wanamlipa Kaseja
aliyekuwa ameachwa na Simba Sh milioni 2, sawa na mshambuliaji mwingine wa
Yanga, Mrisho Ngassa ambaye pia aliichezea Simba msimu uliopita.
Lakini katika mazungumzo yake, kipa
huyo ameutaka uongozi wa Simba kumhakikishia kwamba kipa Abel Dhaira raia wa
Uganda anabeba virago vyake na kuondoka.
“Berko amesema yuko tayari kuja nchini
na kuanza kazi lakini asingependa hata kidogo kuona Dhaira yupo. Ndiyo kilikuwa
kitu cha kwanza ambacho hakihitaji kukiona na kweli tumefanya hivyo kwa kuwa
hata Dhaira mwenyewe ameonyesha anataka kuondoka,” kilieleza chanzo kutoka
ndani ya Simba.
Hata hivyo, Simba italazimika
kumsajili kwa nusu msimu tu kwa kuwa TFF tayari imetangaza kuanzia msimu ujao,
imepitisha sheria ya timu kutosajili makipa wa kigeni.
Berko aliondoka nchini Yanga ikiwa
inamhitaji, lakini ililazimika kumtumia Ally Mustapha ‘Barthez’ aliyekuwa kipa
wa pili baada ya kipa huyo kuonyesha usumbufu na maringo huku viongozi
wakilalamika alikuwa si mtu anayejituma.
No comments:
Post a Comment