Friday, November 30, 2012

PICHA ZA ZANZIBAR HEROES UWANJANI JANA NA MATOKEO.


.
Shaffih Dauda ameripoti kwamba Znz Heroes wameshinda 2-1

KAULI YA DAVID KAFULILA KUHUSU MKUU WA MKOA WA KIGOMA.


David Kafulila.
Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini DAVID KAFULILA amesema anakusudia kupeleka hoja binafsi kwenye kamati ya maadili ili iweze kumchukulia hatua mkuu wa mkoa wa Kigoma luteni kanali mstaafu ISSA MACHIBYA kwa madai ya kulidhalilisha Bunge ambalo ni muhimili wa serikali.
Akiwa kwenye kongamano la kujadili masuala ya uwekezaji katika kanda ya ziwa Tanganyika lililofanyika mkoani Katavi hivi karibuni, mkuu huyo wa mkoa wa Kigoma anadaiwa kutoa kauli kuwa wabunge ambao hawatafuata maelekezo yake kama mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya watapigwa pingu kama raia wa kawaida.
Kanali mstaafu Issa Machibya.
Kauli hiyo imeonekana kuwakwaza wabunge wa mkoa wa Kigoma ambao wamesema huko ni kukiuka sheria na kuudhalilisha mhimili wa Serikali na hivyo mbunge huyo wa Kigoma kusini amemtaka mkuu huyo wa mkoa kuomba radhi vinginevyo atamshitaki.
Mbunge Kafulila Amesema anashangaa ni kwa nini spika wa bunge bi.Anne Makinda amekaa kimya bila kusema lolote juu ya kauli hiyo.

NYOKA WA AJABU AONEKANA NCHINI INDIA, ANA VICHWA VITATU, YADAIWA AMEISHI MIAKA 90.


NYOKA WA AJABU AONEKANA NCHINI INDIA, ANA VICHWA VITATU, YADAIWA AMEISHI MIAKA 90.

HUYU NDIYE MWANAMKE MWENYE ULIMI KUSHINDA WOTE HAPA DUNIANI


MAGAZETI YALIYOTUFIKIA ASUBUHI YA LEO IJUMAA YA TAR 30/11/2012.UDAKU NA SIASA



Ushahidi mpya wa mauaji ya Mau Mau


Baadhi ya wapiganaji wa Mau Mau waliodhulumiwa na wakoloni wa Uingereza
Stakabadhi za Serikali zilizotolewa huko Uingereza zinaonyesha kwa ukamilifu namna wafungwa wengi waliuawa wakati wa uasi wa kundi la Mau Mau nchini Kenya.
Wakenya kumi na mmoja walipigwa na walinzi hadi kufa katika kambi walikozuiliwa ya Hola huku wengine wakijeruhiwa mwaka 1959.
Mzee moja manusura wa mauaji hayo kwa sasa ameshtaki serikali ya Uingereza akidai aliteswa.
Stakabadhi hizo zinaonyesha mkutano uliongozwa na aliyekuwa gavana wa Kenya na maafisa wakuu wa magereza kumbukumbu zinazoonyesha kuwa maafisa hao walikiuka haki za binadamu lakini hawakufunguliwa mashtaka.

Thursday, November 29, 2012

BAADHI YA PICHA ZA WALIOJITOKEZA KUMZIKA MSANII SHARO MILIONEA.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

2
Gari alilokua analiendesha Sharo Milionea lilianza kutoka nje ya barabara kuanzia hapa.
Sehemu gari lilipokwenda kusimama ni pale kwenye watu wengi panaonekana kwa mbali.
.
.
.
Gari lilivuka hii sehemu na kubinukia kule mbele baada ya hilo daraja dogo ambako ndio liligonga huu mti hapa chini.
Huu ni mti ambao aliugonga katikati akaukata kuwa vipisi viwili, mwingine ukatupwa mbele ya huu kama unavyoonekana alafu gari ikaenda kubinuka kichwa chini miguu juu kwenye lile eneo la wazi unaloliona kwa mbali baada ya hayo matawi ya huo mti hapo mbele.
kipisi cha pili cha mti aliouvunja katikati.
.
Hapa ndipo gari lilikuja kusimama na Sharo Milionea akiwa peke yake kwenye gari alirushwa nje.
Hapa ndipo mwili wa Marehemu ulikutwa baada ya kutupwa kutoka kwenye gari, mashuhuda waliofika kwenye eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali wanasema walianza kuwatafuta majeruhi wakidhani ni wengi na hawakumuona mtu yeyote kwenye gari ila baadae mama mmoja ndio akamuona Sharo Milionea akiwa hapa muda mfupi kabla ya kukata roho.
Huyu shuhuda wa ajali amesema Sharo Milionea alifariki dunia baada ya dakika 15 za ajali na hiyo ilikua saa mbili usiku ndio ajali imetokea, hakukua na magari yanayopita kwa wakati huo hivyo walkosa pa kuomba msaada manake hata kwenye kijiji wanachoishi chenye watu kati ya 300 na 400, hakuna yeyote mwenye pikipiki wala gari.

Aliniambia pia kwamba Sharo Milionea hakuwa na uwezo wa kuongea chochote na baada ya hizo dakika 15 alitingisha tu mguu na kugeukia upande wa pili na kukata roho, mwili wake ulikuja kuchukuliwa saa nne usiku na askari.
Kingine alichoniambia huyu shuhuda ni kwamba kwenye hilo eneo huwa hakutokei ajali za mara kwa mara, kwa miaka zaidi ya 20 aliyoishi hapa ni ajali chache sana zimetokea, hakuna ajali mwaka huu zaidi ya Sharo Milionea ila mwaka jana ilitokea ajali moja ambapo mtoto wa shule aligongwa na basi la Raha Leo na kufariki.
Hili eneo liko umbali wa kama dakika 40 mpaka Tanga mjini na ni dakika 15 tu mpaka kufika nyumbani kwa kina Sharo milionea ambako ndiko Marehemu alikua anaelekea, rafiki yake wa karibu mwigizaji Kitale (anaeigiza kama teja) kasema mara ya mwisho Sharo aliongea nae na akamwambia anakimbia Tanga mara moja kumpelekea mama yake mtaji wa shilingi milioni sita za biashara ambazo alikua nazo wakati huo kwenye gari lakini imefahamika kwamba hizo pesa zimeibwa zote kwenye eneo la ajali.

.
.
.
Msibani.
PICHA ZA NYUMBANI KWA KINA SHARO MILIONEA KWENYE MSIBA

Hiyo nyumba mbele kushoto ndio nyumba ya kina Sharo Milionea ndipo alipozaliwa.

.
.
.
Mwenye t shirt nyeupe ni Mwigizaji Kitale, rafiki wa karibu sana wa Sharo Milionea.
Baadhi ya waigizaji kutoka Bongo Movie
.
.
Mjomba wa Marehemu ambae alisema Sharo Milionea atazikwa saa saba mchana.