Maharusi wengi hutamani siku ya harusi
kuwa siku ya kitofauti zaidi katika maisha yao wakiamini ndio siku pekee
ambayo ni ya furaha zaidi huku wengine wakitumia kila aina ya njia
kuhakikisha sherehe yao inapendeza.
Utakuta wengine wanatumia usafiri wa
farasi au magari ya kifahari kuhakikisha tu sherehe inakuwa ya kipekee
zaidi kwao lakini kwa Jenny Buckleff ilikua tofauti kwani yeye alitumia jeneza kama usafiri wake.
Jenny alitaka kuwashangaza wageni
waliofika kwenye sherehe yake hata kwa mumewe pia kwani hakumwambia mtu
yoyote kuhusu uamuzi wake huo.
Siku ya sherehe aliingia ukumbini akiwa
ndani ya jeneza lililokuwa likisikumwa kwa pikipiki huku kila mmoja
akishikwa na butwaa kutokana na kitendo hicho ambacho si rahisi kutokea.
No comments:
Post a Comment