KONDOMU ni kifaa/ zana iliyotengenezwa
mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana
kutokana na umbile la uume au uke.
Kondomu hizi
zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama
ifuatavyo:-
Awamu ya I –
zilizotengenezwa kwa mimea.
Hizi
zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa
wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]
Awamu ya II
– kutokana na utumbo wa kondoo.
Dr. Condom
alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme
Charles II.
Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa
kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.
Awamu ya III
– kutokana na mpira
Hizi
zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa
kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.
JE KONDOMU
NI SALAMA?
Tunaelezwa
kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba haziwezi kuruhusu kitu
chochote kupita.
Lakini
tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha kuwa kondomu zaweza kuvuja kutokana
na mazingira halisi ya utengenezaji wa latex.
Wengine
wanadai kuwa ili kuzifanya imara, kondomu zimetengenezwa kwa kupishanisha pande
mbili ili kuziba udhaifu wa kila upande.
Hata hivyo
watengenezaji wanasahau kuwa mazingira ya matumizi ya kondomu katika ngono
hayalingani na majaribio waliyofanya ya kujaza maji au hewa ili kupima kama
maji na hewa vinapita.
Katika tendo
la ngono ipo misuguano ya namna mbalimbali inayosababisha kubadilisha mazingira
ya kondomu na kuidhoofisha.
Kutokana na
tafiti hizo imefahamika kuwa kondomu hazina uwezo wa kuzuia mbegu za kiume
kupenya wakati wote.
Upana wa
kipenyo cha mbegu ni makroni 5 wakati upana wa kipenyo cha kirusi cha ukimwi ni
makroni 0.1
Kwa maneno
mengine mbegu ya kiume ni kubwa mara 50 ya kirusi cha ukimwi.
Vile vile
tafiti zimeonyesha kuwa kondomu haina uwezo wa kuzuia maambukizo ya magonjwa ya
zinaa vikiwemo virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia mia moja.
Hivyo tunaweza kusema kuwa, kondomu si salama
kwa asilimia mia moja.
Kondomu zina
kiwango cha kushindwa cha kati ya asilimia 10 na 15 na wengine wanasema hata
asilimia 20.
Wasambazaji
na wahamasishaji wa matumizi ya kondomu hawapendi kusikia ukweli huo na
wanafanya jitihada kubwa ya kuficha ukweli huo.
Matangazo
yatolewayo kupitia mabango ya barabarani, katika televisheni, radio na hata
magazeti yanawarubuni watu yakiwaaminisha kuwa kondomu humkinga mtumiaji kwa
kiwango cha asilimia 100%
Huko ni
kukengeusha ukweli na kukiuka maadili ya kitaaluma.
Wengi kama
sio wote wateteao matumizi ya kondomu hufanya hivyo kwa sababu ya maslahi ya
kifedha na kibiashara.
Tukiongozwa
na dhamiri safi, lazima tukiri ukweli uliopo na tuwaeleze watumiaji, ili
tusijekuwa sababu ya kifo chao.
Kila kondomu
inaposhindwa [itumikapo] kama kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya ukimwi ]
humaanisha kifo.
Udhaifu wa kondomu Kiufundi,Matumizi,
Kimazingira
Udhaifu wa kiufundi
Wasambazaji
wanatueleza kuwa kondomu zilizotoka kiwandani zikiwa na ubora unaotakiwa
zikitumika wakati wote na kwa usahihi zina uwezo wa kukinga kwa kiwango hadi
cha asilimia 97.
Zisipotumika
vizuri zina kiwango cha kushindwa cha asilimia 14.
Kiwango cha
kushindwa kwa kondomu kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa hutofautiana
kutokana na aina ya magonjwa ya zinaa.
Kondomu
zaweza kuzuia kwa kiwango fulani maambukizo ya magonjwa ya zinaa yanayosafiri
kwa njia ya ute, lakini haziwezi kuzuia magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa
mgusano wa mwili kama vile "herpes" na "human
papillomavirus"; au magonjwa yanayoambukizwa kutokana na vidonda au
malengelenge yaliyoko kwenye via vya uzazi kama vile kaswende.
Hali hiyo
inatokana na:
Watengenezaji
wameruhusu udhaifu wa kiufundi kama zao la kiwandani lililotengenezwa na kazi
ya mikono ya binadamu [acceptable quality limit] kwa kiwango Fulani kwa nchi
mbalimbali.
Mfano,
Marekani kiwango kilichokubaliwa ni asilimia 99.6 kwa kutoruhusu kondomu
kuvuja.
Uingereza asilimia 97, Uholanzi asilimia 96. 5. Hivyo katika kila idadi
ya kondomu itumikayo kwa wakati mmoja kuna kiwango cha kuvuja kati ya asilimia
0.4 (USA); 3% (Britania); 3.5% (Holland).
Kondomu huzeeka
Kwa kadiri
zisivyotumika kwa muda mrefu ndivyo hivyo zinaaendelea kuzeeka.
Kwa hiyo
mtumiaji kondomu wa miaka 3 au 4 baada ya kondomu hiyo kutengenezwa yumo katika
hatari zaidi kuliko anayetumia kondomu mara tu baada ya kutoka kiwandani.
Utafiti
mmoja umeonyesha kuwa kiwango cha kupasuka kwa kondomu kiliongezeka kutoka 3.6%
kwa kondomu mpya hadi 18.6% kwa kondomu zilizotumika miaka kadhaa baadaye.
Kondomu hupasuka.
Kiwango cha
kupasuka hutegemea aina ya kilainisho kilichotumika na aina ya kondomu. Kwa
mujibu wa tafiti 15 zilizofanywa na "Contraceptive Technology"
yalionyesha kuwa katika kondomu 25,184 zilizotumika 4.64% zilipasuka.
Ingawaje
kondomu za latex zinaonekana kuwa na kiwango kidogo sana cha kupitisha virusi vya
ukimwi, hatari kubwa ya matumizi yake imo katika uwezekano wa kondomu kupasuka,
kuteleza na kuteleza.
Kwa hiyo
hata kama ni virusi vichache tu vinaweza kupenya, kiwango cha maambukizo
kitakuwa kikubwa kadiri kondomu zinavyosambazwa kwa wingi na kadiri watu
wanavyojihusisha na vitendo vya ngono wakiamini katika matumizi ya kondomu.
Udhaifu
katika matumizi
Matumizi mabaya: yaani kutovaa vizuri,
kuvaa nje ndani, aina ya ngono, urefu wa muda wa ngono, pia kutokana na uelewa
mdogo hasa kwa wasojua kusoma na kuandika na wale wakaao mbali na mijini.
Kuteleza na kuvulika kutokana na hali ya
uume kuwa mdindifu au la; upana au wembamba; mrefu au mfupi.
Pia kutokana
na tendo la ngono na hali ya mtumiaji na mazingira ya matumizi.
Kutokana na
umri wa mtumiaji, kama ni mtoto, kijana, mtu mzima au mzee.
Kutumia
kondomu ambazo muda wake umepita. Mfano wanaotumia gizani , katika hali ya
ulevi, kutokujua kusoma, kuchunguza na kugundua kama muda wake umepita.
Mazingira ya
kingono yakishawekwa, watu wanatawaliwa na mihemuko ya juu ya ngono kiasi
kwamba hawawezi kuchunguza tarehe ya ukomo wa matumizi ya kondomu.
Ingawa
watengenezaji wanashauri kutotumia kondomu iliyobadilika rangi au iliyokauka,
tabia za watumiaji hazina nafasi ya kuzingatia ushauri huo.
Lengo la
mtumiaji laweza kusababisha matumizi kuwa mabaya. Mtu mwenye virusi vya ukimwi,
anajiwekea lengo kwamba hataki kufa peke yake, atafanya jitihada za kutokutumia
vizuri ili mwenzake [ambaye anaamini hajaambukizwa] aweze kuambukizwa ili,
"nisife peke yangu".
Vilevile
katika siku hizi za dawa za kupunguza makali ya kuzaliana virusi vya ukimwi,
mtu anaweza kuonekana mwenye afya nzuri kabisa, na anaweza kumshawishi mwenzake
kuachana na kondomu kwa vile "wanaaminiana".
Kwa hiyo
mambukizi yanaweza kuwa makubwa kutokana na kutowadhibiti wale waliokwisha
ambukizwa.
udhaifu wa kimazingira
Huu
unatokana na hali zifuatazo:- kibinadamu,
kimaumbile na Kibinadamu.
Udhaifu wa
kondomu waweza kusababishwa na usafirishwaji, yaani muda unaotumika kusafiri
kutoka sehemu zinapotengenezwa hadi mahali zinapotumika;
ii.
Kimaumbile
Vyombo vya
usafirishaji na usalama wa vyombo hivyo;
Kondomu
zinazosafirishwa katika meli, zikiwa baharini kwa miezi kadhaa kabla hazijafika
katika nchi lengwa na katika hali ya joto ndani ya makontena zinakuwa na
kiwango hafifu katika ubora wake.
Udhaifu wa
sehemu ya kuhifadhi kondomu pamoja na vyombo vya kuhifadhia.
source.
Human Life International.
Gordon
Kalulunga
Information
and Media Consultant
P.O. Box
705, Mbeya-Tanzania
Tel: 255
(0)754 440749
e-mail:
kalulunga2006@gmail.com
www.kalulunga.blogspot.com