Wednesday, April 30, 2014

ANGALIA PICHA ZA AJALI ILIYOUWA WATU 19 MKOANI SINGIDA WAKIWEPO POLISI 4


Wednesday, April 30, 2014


Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-salaam. Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.

Watu 19 wa kijiji cha Utaho wilayani Ikungi wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry wakati wakiwa wana toa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliye gongwa na gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja .Mwandishi wa habari wa ITV alifika na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa  katika kituo cha polisi cha Ikungi bila ya kujua hatima yao ya  safari baada ya basi lao kuwakanyaga na kuuwa watu 19

Gari la polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya mkoa wa singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa
PICHA ZOTE NA :Elisante Mkumbo-Singida

Moja ya maiti ya ajali ya basi la sumry iliyo tokea katika kijiji cha Utaho Wilayani Ikungi ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.
 Baadhi ya miili ya wakazi wa kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi, waliogongwa na basi la Summry ikiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida mjini humo.

ANGALIA PICHA MAMBA MKUBWA WA AINA YAKEAKAMATWA NIGERIA

Mamba huyu anaurefu wa miter 7 na Inakadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 85, inasemekana kuwa mamba huyu amekula watu zaidi ya 200 katika umri wake.Kilio cha wanakijiji ndio kimesababisha mamba huyu kutegwa na kukamatwa kitaalam, hatahiyo