Wednesday, April 30, 2014
Basi hilo la kampuni ya Sumry hufanya safari zake kati ya Kigoma na Dar-es-salaam. Dereva wa basi hilo alikimbia mara tu na baada ya ajali hiyo na kulitekeleza basi hilo.
Watu 19 wa kijiji cha Utaho wilayani Ikungi wamepoteza maisha wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi, baada ya kugongwa na basi la Summry wakati wakiwa wana toa msaada wa kumpakia marehemu kwenye gari la polisi aliye gongwa na gari kubwa ambalo halikufahamika mara moja .Mwandishi wa habari wa ITV alifika na kuwakuta wasafiri walionusurika wakiwa katika kituo cha polisi cha Ikungi bila ya kujua hatima yao ya safari baada ya basi lao kuwakanyaga na kuuwa watu 19
Gari la
polisi likiwa limepakia maiti zaidi ya kumi zikipelekwa hospitali ya
mkoa wa singida kwa ajili ya kuhifadhiwa na kutambuliwa
PICHA ZOTE NA :Elisante Mkumbo-Singida
Moja
ya maiti ya ajali ya basi la sumry iliyo tokea katika kijiji cha
Utaho Wilayani Ikungi ikisubiri kupakiwa katika gari la polisi.
Baadhi ya miili ya wakazi wa kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi, waliogongwa na basi la Summry ikiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida mjini humo.
Baadhi ya miili ya wakazi wa kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi, waliogongwa na basi la Summry ikiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida mjini humo.
No comments:
Post a Comment